Kwanini Wakristo hawavui viatu wakiingia Kanisani? Mbona Musa aliambiwa avue viatu?

Kwanini Wakristo hawavui viatu wakiingia Kanisani? Mbona Musa aliambiwa avue viatu?

Najua utakuja na Hoja kuwa Sinagogi ni msikiti.

Sinagogio SIO msikiti.
Yesu hakuingia msikitini.

tofauti moja wapo ndio hiyo kuwa Msikitini watu wanavua viatu wakat kwenye Sinagogi hawavui.

Pia Sinagogi ni kwa Wayahudi tu.

Ufunuo 3:9
"Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda."

Baadae sasa masinagogi yakawepo mengi had kwa watu ambao Sio wayahudi. Ila wakaanzisha Ya kwao kuiga yale ya Kiyahudi.

Mtume alikuta pia masinagogi. Ila la Kiarabu. (Ambapo watu walikuwa wanakusanyika kwa dini zao nyingne ).

Mtume alijenga msikiti wa Kwanza "masjid Quba"
Msikiti ni sinagogi sema ni sinagogi kwa wale wanaokusanyika na Kumuamini Allah.

Kanisa kwa namna ni nyingine ni Sinagogi sema wanakusanyika kwa wanaomuamini Kristo.
Na kila sinagogi ina setup yake.
 
Katika kitabu cha Kutoka 3:5, Mungu alimwambia Musa: "Usikaribie hapa, vua viatu vyako miguuni, maana mahali unaposimama ni ardhi takatifu." Kwanini basi Wakristo wa leo hawatii agizo hilo la kuvua viatu wanapoingia kanisani, ilhali Musa aliambiwa hivyo?

Sababu ya Musa kuambiwa avue viatu imetajwa wazi na Mungu mwenyewe:
“Maana mahali unaposimama ni ardhi takatifu.” Ardhi ile ilikuwa takatifu kwa sababu ya uwepo wa Mungu. Nyakati hizo viatu vilionekana kuwa na uchafu kwa sababu ya kutembea juu ya mavumbi, tope, na uchafu wa kila aina. Kwa hiyo, kuvua viatu kilikuwa ni kitendo cha kujitakasa.

Labda unajiuliza tena: kanisani si kuna uwepo wa Mungu? Kama ndivyo kwanini Wakristo hawavui viatu? Ni kweli, kanisani kuna uwepo wa Mungu. Lakini katika Agano Jipya Mungu hakai mahali maalum tu. Anakaa ndani ya kila aaminiye. Yesu anasema katika Ufunuo 3:20
"Tazama, nasimama mlangoni nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nitakula naye, naye atakula pamoja nami."

Ili Yesu (ambaye ni Mungu) aingie na kukaa ndani yetu, ni lazima kwanza tuyavue matendo ya giza (Warumi 13:12). Kwa hiyo katika Agano Jipya, utakatifu unaonyeshwa siyo kwa kuvua viatu, bali kwa kuvua tabia za dhambi na kuvaa utakatifu wa moyo.

Ndiyo sababu tunaambiwa “Heri wenye moyo safi, maana hao watamwona Mungu.” (Mathayo 5:8)

Katika 1 Kor 6:19 tunajifunza pia kwamba hekalu la Mungu sio la matofali na mawe, miili yetu ndiyo hekalu la Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ni nafsi ya tatu ya Mungu. Ili aingie ndani yetu ni lazima mioyo yetu iwe safi. Hii ina maana kwamba utakatifu sasa unahusiana zaidi na moyo wa mtu, sio ardhi anayokanyaga au viatu anavyovaa.

Kwa maneno mengine, katika Agano Jipya, kuvua viatu hakumfanyi mtu kuwa mtakatifu. Mtu ambaye hajavua matendo ya dhambi, akivua viatu kabla ya kuingia kanisani, bado tu saa ya kutoka kanisani atavaa viatu na kuitumia miguu yake kwenda kuiba, kufanya uzinzi, kulewa, na kufanya dhambi nyingine.
Yule hamis mpenda kupost mambo ya dini ni mwenzio!?
 
MATENDO YA MITUME 17:1
"Akiisha kupita kati ya amfipoli na Aporonia akafika Thesalonike ambapo palikuwa na Sinagogi la Wayahudi na Paulo akaingia mle walimo akahojiana nao kwa maandiko ...."
 
Swali zuri na Fikirishi.

Kwanza jua kuna hema, Hekalu, sinagogi na Kanisa.
Na ni vitu vinne tofauti.

Ingawa vyote Lengo ni kukutana kwa ajili ya Kumuomba Mungu.
Utofauti uko kwenye Ukubwa na setup pamoja na vilivyomo ndani yake.

Musa alijenga Hema la Mungu.
Suleiman alijenga hekalu.
Wayahudi wakajenga Sinagogi.
Na baada ya Yesu wakaanzisha Kanisa.

Yesu aliingia Sinagogi.
Jumba kubwa ambalo Wayahudi walikuwa wanakusanyika kuongea kuhusu tamaduni mila na desturi zao

So kanisa limekuja after yesu
 
Makafiri si mmeahidiwa mtaimba na kukata viuno? Naona imekuuma sana😄😄😄. Chuki imekujaa mpaka unaona wivu kobazi kupata bikra 72. Soma mathew 19 29 kuna wanaopata wake 100 ila hawajasema kama bikra.
Mbona unazunguka sana mkuu, sema tu kuwa kama wewe siyo kobazi basi hupati hao mabikra 72
 
Ila Yesu mnaemfata alivua viatu kabla ya kuingia kwenye sehemu ya ibada... sasa kama yeye licha ya kujua usafi n nafsi na sio mwili mbona alivua viatu??

Yani Mungu wako mwenyew kavua viatu alipoenda kumuomba Mungu wake, wewe mkerewe unagoma kuvua,,,, aliyekuandikia hicho kitabu pia kavua viatu, wewe mletewaji hutaki kuvua
Kama sio Bangi n nn😂😂😂

Taifa teule takatifu la Mungu wako ambao n watoto wa Mungu wako (Israel)
Wanavua viatu.... wewe Babu yako muabudu miti, ukaja na Sheria zako hutaki kuvua viatu

Walokole bhana🚶
 
Yesu alivua viatu Lini?.

Hakuna andiko linalosema hivyo kwenye Biblia.

Mussa alivua viatu hapo tu.
Sehem nyingne zote wakat anakutana na Mungu hakuwah vua viatu.

Musa alitengeneza Hema na watu walikuwa wanakusanyika kumuabudu Mungu .
Ila hakuna sehemu imeandikwa kuwa WaliVua viatu wakat wanaingia kwenye hema.

Kutoka 33:7
"Basi desturi ya Musa, ilikuwa kuitwaa ile hema, na kuikita nje ya marago mbali na hayo marago; akaiita, hema ya kukutania. Hata kila mtu aliyekuwa akitaka neno kwa BWANA, akatoka, akaenda hata hema ya kukutania, iliyokuwa nje ya marago. "

Hakuna sehemj waliambiwa waingie Hemani wakiwa wamevua viatu.

Pia Wayahudi hawavui viatu wakat walivyokuwa wanaingia Sinagogi.
 
Swali lako linaonyesha kana kwamba hujaelewa mantiki ya kwa nini jina la Musa limetajwa katika mada hii.

Sijamtaja Musa kwa sababu tunamfuata au tunataka kuiga kila alichofanya. La hasha. Nimemtaja Musa kwa sababu kuna watu wanaojaribu kuhalalisha utaratibu wa kuvua viatu kanisani kwa kutumia mfano wa Musa. Kwa maneno mengine, wao wanasema: “Mbona Musa alivua viatu aliposimama kwenye ardhi takatifu? Basi hata sisi tuvue.”

Kwa hiyo, nimetoa mfano wa Musa kwa lengo la kubatilisha hoja hiyo, si kwa lengo la kumfanya Musa kuwa kielelezo cha Ukristo. Musa hakuwa Mkristo, na hakuna mahali katika Agano Jipya ambapo Wakristo waliagizwa kuvua viatu kama utaratibu wa ibada. Yesu hakufundisha hilo. Mitume pia hawakulisisitiza hilo. Hivyo basi: kama sababu pekee ya kuvua viatu ni kwamba “Musa alivua,” basi sababu hiyo haina mashiko. Umenipata?
Ukipata bwana wa kukukuna vizuri utaacha usumbufu huku jf.
 
Ila Yesu mnaemfata alivua viatu kabla ya kuingia kwenye sehemu ya ibada... sasa kama yeye licha ya kujua usafi n nafsi na sio mwili mbona alivua viatu??

Yani Mungu wako mwenyew kavua viatu alipoenda kumuomba Mungu wake, wewe mkerewe unagoma kuvua,,,, aliyekuandikia hicho kitabu pia kavua viatu, wewe mletewaji hutaki kuvua
Kama sio Bangi n nn😂😂😂

Taifa teule takatifu la Mungu wako ambao n watoto wa Mungu wako (Israel)
Wanavua viatu.... wewe Babu yako muabudu miti, ukaja na Sheria zako hutaki kuvua viatu

Walokole bhana🚶

Alivua viatu kama tamaduni ya wahayahudi

Ni kama sisi tunavyosema shikamooo ni utamaduni tu
 
Makafiri si mmeahidiwa mtaimba na kukata viuno? Naona imekuuma sana😄😄😄. Chuki imekujaa mpaka unaona wivu kobazi kupata bikra 72. Soma mathew 19 29 kuna wanaopata wake 100 ila hawajasema kama bikra.

Yuda 1:4 (Biblia takatifu).
kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo. ”
Nakisaidia ujue maana ya 'kafiri
 
Hakuna pia Sehemu kwenye mafundisho ya Kiyahudi yanasema Vua viatu ukiingia Sinagogi.

Wayahudi walikuwa wanaingia na Viatu kwenye Sinagogi na ndio maana Yesu pia hakuvua.

Ndio maana nikasema kuna tofauti ya Hema, Hekalu , Sinagogi na Kanisa.
Lakini Yesu alikuwa akiwafundisha maandiko ya torati ya Musa pamoja na mila nyingine za Musa, je yakuvua viatu haikuwepo?
 
Back
Top Bottom