Kwanini wakristo tunaamini Israel ni taifa la Mungu wetu huku Waisrael hawamuamini Yesu wala dini ya ukristo?

Kwanini wakristo tunaamini Israel ni taifa la Mungu wetu huku Waisrael hawamuamini Yesu wala dini ya ukristo?

Kwann hakuna hata dhehebu moja la ukristo limeanzia Jerusalem?
sasa ukristo umeanzia wap??
wewe ndo unajadiri usichokijua
Ukristo ulianzia israel amboko ndo yesu aliishi baada ya kufa ndio ukasambazwa duniani.
Waisrael kutomuamini kristo ni kitu kingine
lakini pia ujue si wote waisrael wakristo wapo.

alakin biblia imeandika pia kuhusu hilo
 
The bible and its prophecy is mostly about Israel.
The original,old and first covenant in the old testament is with Israel.
Jesus came for the house of Israel.
THese are the undeniable facts. Ukibisha, soma vizur bible.

We the other christians are plainly known as GENTILES na sisi we enter into God's covenant through Christ baada ya Israel kumkataa Mesiah.

This new covenant is for us Gentiles na ndio maana as believers out of Israelites, we are not bounds with most of jewish traditions.

This is deeply explained in the Book of Hebrews in the New testament.
Kwahiyo wayahud kumkataa Kristo, haituzuii sisi kumuamini na kuhesabiwa haki kwa kutii maagizo yale yale ambayo wanapaswa wayahud nao kuya obey, na zaid sana kwa neema tuliyo kirimiwa through Christ.
 
Mjinga ni nani hapo?
Wewe uliyepost huo ujinga. Na uache kuhadaa watu. Kama umechagua kuwa mpagani Baki huko huko usubiri adhabu yako. Maana huna namna ya kuiepuka hukumu itakayotolewa na Yesu unayemkana hapa duniani.
 
Mtiririko wa ujumbe wa biblia kwa ujumla Ni wakina sana na umekamilika kujibu maswali yote ambayo mwanadamu anaweza kujiuliza kuhusu maisha na chanzo chake. Biblia imefaulu kwa msingi wake wa imani kutibu fikra dhaifu kuwa zenye nguvu. Binafsi Kuna wakati nilianza kuwaaminisha watu kwamba tatizo la kifo litatatuliwa na mwanadamu mwenyewe kwakutoa hoja na mifano thabiti. Lkn kumbe nilikuwa mjinga Mimi, kwakuwa sikuwa nimeisoma biblia vizuri. Nilichukua hatua kuichimba vizuri nakubaini ukweli. Kilichfata Ni toba kwakupotosha wengi. Hata Hawa ambao wanapinga kuhusu yesu na biblia, wengi wao hawaijui kabisa Wala hawajui maudhui yaliyomo. Hawajui kwakina Ni namna gani yesu aliukomboa ulimwengu. Hawajitambui pia, Wala hawazihurumii nafsi zao. Kama wameshindwa kuzihurumia nafsi zao, wanawezaje kumuhurumia yesu kwakazi nzito yakuutoa uhai wake kwaajili ya nafsi zao? Ni wachache sana wanaoijua njia maana mwili huu uko connected na dhambi ilivyo ngumu kuishi kinyume na takwa la mwili. Neema ndio jibu. Tukisema wayahudi wote hawamjui yesu Ni uongo. Kwani neno la injili lilitoka wapi? Ni kwa baadhi yao waliobahatika kuijua kweli.
Ila tambua kuwa Warumi walivamia Jerusalem 70 AD wakauwa wasomi wote waliohifadhi mandiko ya Mungu Kisha wakachukua vitabu vyote vya manabii wakaenda navyo Roma wakavifungia miaka 300

Utawala wa Constantino ndio ukaandika upya hayo maandiko na hatimaye hapo ndio ikazaliwa bibilia na ukristo

Hiyo bibilia kutoka Roma na huo Ukristo ulipopelekwa Israel wayahudi wakavikataa vyote

Wewe ukisoma bibilia unadhani unasoma maandiko ya Mungu kumbe Warumi walisha yachakachua

Wewe nani alikuambia Jumapili ni siku ya ibada kama sio Mfalume Constantino?
 
Ni kwasababu ushakuwa indoctrinated toka utotoni.

Mtoa mada inawezekana akawa ni mtu mzima mwenye familia yake. Lakini fikiria hii tu kuwa babu yake enzi za utotoni mwake naye alikuwa akifundishwa kuwa Yesu anarudi.

Babu yake akaja ku pass hayo mafundisho kwa baba yake na mtoa mada kuwa Yesu anarudi.

Baba yake na mtoa mada naye akamzaa huyu mtoa mada kaja kumrithisha mafundisho hayo hayo kuwa Yesu anarudi.

Na huyu mtoa mada pengine tayari kasha warithisha wanae au anatarajia akipata watoto aje kuwaambia kuwa Yesu anarudi.

Umeona mlolongo ulivyokuwa mrefu huo?

Infact ni kitu ambacho sio rahisi kuweza kukiepuka kwasababu kinakufanya uwe emotional zaidi kuliko realistic.

Mfano wa mtu aliyekua affected na indoctrinations hata akipewa hoja bilion zenye logic ili kum-shape arudi kwenye njia sahihi atakupinga tu kwa maneno machache tu kuwa "biblia imeandika hivyo na haiwezi kupotosha"

Kitabu chochote ambacho kimeandika kuwa mtumwa anapaswa kumsujudia slave master je hiyo katika perception ya kawaida haikupi mwangaza kuwa kitabu hicho kimeandikwa na slave master?

Hata kama utakuwa umempa ushahidi kuonesha Biblia imeandikwa na hao waliojipakulia minyama, bado hiyo haitatosha kumuondoa gizani huyo mtu kwasababu ya toxic aliyoipandikizwa tangu akiwa mtoto.
kwani hata makazini si mna maboss zenu mnatakiwa kuwanyenyekea kikazi!!!hilo halipindui kwamba boss pia ana wajibu juu yako.
 
kwamtazamo wayeyote mwenye akili lazima atakubali kwamba kulingana na dunia ilivyo Ni lazima yupo au alikuwepo
Umeona jinsi unavyojitangizia mpira mbele?

Umefikiaje conclusion ya kujua chanzo ni lazima kiwe na identity inayopimika kwa yupo au alikuwepo?

Kwanini isiwe kipo au kilikuwepo?
 
Wewe jibu mada, wachana na ujinga wa kumjadili mleta mada.
Unapojadili ujinga huwezi kumuacha kumjadili muathirika wa ujinga, kufanya hivyo itakuwa ni ujinga zaidi.

Utam-shape vipi kumuweka kwenye njia au kufanya wengine wasiingie kwenye hilo shimo kama utakuwa unaweka hoja ambazo zitakuwa zinam exclude victim wa ujinga?
 
kwani hata makazini si mna maboss zenu mnatakiwa kuwanyenyekea kikazi!!!hilo halipindui kwamba boss pia ana wajibu juu yako.
Sijaelewa

Yani kwamba Boss unataka kumfananisha na slave master?
 
Unapojadili ujinga huwezi kumuacha kumjadili muathirika wa ujinga, kufanya hivyo itakuwa ni ujinga zaidi.

Utam-shape vipi kumuweka kwenye njia au kufanya wengine wasiingie kwenye hilo shimo kama utakuwa unaweka hoja ambazo zitakuwa zinam exclude victim wa ujinga?
Wewe ni kondoo au siyo?
 
Ila tambua kuwa Warumi walivamia Jerusalem 70 AD wakauwa wasomi wote waliohifadhi mandiko ya Mungu Kisha wakachukua vitabu vyote vya manabii wakaenda navyo Roma wakavifungia miaka 300

Utawala wa Constantino ndio ukaandika upya hayo maandiko na hatimaye hapo ndio ikazaliwa bibilia na ukristo

Hiyo bibilia kutoka Roma na huo Ukristo ulipopelekwa Israel wayahudi wakavikataa vyote

Wewe ukisoma bibilia unadhani unasoma maandiko ya Mungu kumbe Warumi walisha yachakachua

Wewe nani alikuambia Jumapili ni siku ya ibada kama sio Mfalume Constantino?
Wasingeweza andika ujumbe mzito vile. Kusanya watu jamii forum ambao unaamini Ni vichwa then muanzishe upagani wenu tuone Kama mtaweza. Hatufuati neno la Mungu eti kwakuwa yameandikwa hasha! Tunafuata kwa sababu Kuna evidence kuwa neno linaishi. Imeandikwa kwamba ukimkiri yesu nakufuata maagizo yake atajidhihirisha kwako. Sasa Mimi nimefuata agizo lake na kweli kajidhihirisha, bado tu niwe kiburi? Au unataka kuniambia Ni mzimu wa constantino ndio uliojidhihirisha kwangu? Wanapofeli wanaopinga Ni kwamba pindi wanapotoa povu zao kwetu ndivyo Mungu anavyozidi kajidhihirisha, vinginevyo tungeshakuwa wapagani kitambo Kama wao.
 
Umeona jinsi unavyojitangizia mpira mbele?

Umefikiaje conclusion ya kujua chanzo ni lazima kiwe na identity inayopimika kwa yupo au alikuwepo?

Kwanini isiwe kipo au kilikuwepo?
Hujui kiswahili vizuri au kipo au kilikuwepo inamaana ya kitu Fulani but yupo inamaana ya mwenye uhai. Sio Jambo lakujadili hili au pointi zimekata mzee!
 
Hujui kiswahili vizuri au kipo au kilikuwepo inamaana ya kitu Fulani but yupo inamaana ya mwenye uhai. Sio Jambo lakujadili hili au pointi zimekata mzee!
Katika research ya jambo usilolifahamu huwezi kuanza na start point yenye bias.

Neno "kitu" au "nini" ni start point linalokupa uwanja mpana wa kiufumbuzi kuweza kupata majibu sahihi kwasababu hayajifungi kwenye eneo moja.

Baada ya research ndio unaweza kupata data zinazokufikisha kwenye "yupo"

Kupitia "nini" na "kitu" unaweza kupata "nani" kwasababu ni maneno ambayo yame generalize vitu vyote, ila ukitumia nani utaishia ku-stick kwenye sehemu ndogo kwasababu ni neno liko fixed eneo dogo.

Kwa hiyo nikirudi kwenye kauli yako kuwa neno "yupo" ni kauli ya kiswahili inayowakilisha uhai bado nitatia shaka knowledge yako ya kiswahili.

Nikisema Hospitali ya Temeke pale Mochwari yupo marehemu aliyekufa kwa ajali jana. So kwa mujibu wa kiswahili chako ni kuwa hiyo statement itaonesha uhai wa marehemu?

Halafu kitu kingine uhai haupimwi tu kwa watu hata vitu pia vina uhai, miti, mimea navyo pia vina uhai.

Sasa unapotaja miti unaweza kutumia reference ya neno "yupo" kwasababu mti una uhai?
 
Back
Top Bottom