Sasa mbona hakuna kanisa lililoanzishwa Israel?
-anglican
-roman catholic
Simple logic ni kwamba, wale viongozi waliobaki baada ya yesu kufa walikuwa ni binadam kama wewe, wenye uoga na kuogopa kufa au kuuawa kama kiongozi wao yesu alivyouawa, hivyo isingekuwa rahisi kujenga kanisa maana wangeuawa kabla ya kufanikisha mpango wa ujenzi. Lakini yesu alitembea nchi mbalimbali kutangaza injili hivyo wale wanafunzi walienda kwenye mataifa kuitangaza injili na kujenga makanisa. Kwanini Israel ya sasa kwa asilimia kubwa sio wakristo!?? Jibu ni kwamba kabla ya yesu kuja wayahudi walikuwa na mahekalu Yao na walikuwa wanamuabudu mungu na mafundisho Yao waliyoyaamini, yesu akaja akafundisha wakakataa mafundisho na kumuua, nao wanafunzi wakatawanyika kuhubiri sehem nyingine kuhofia kuuawa hivyo kwa asilimia kubwa tamaduni zao na njia za kumuabudu mungu zilibaki vilevile.