Kwanini wakristo tunaamini Israel ni taifa la Mungu wetu huku Waisrael hawamuamini Yesu wala dini ya ukristo?

Boss ni slave master anayekulipa zaidi tu.
Muajiriwa anaweza kuacha kazi, mtumwa hawezi kwasababu ile kwake sio tu kazi bali amemilikiwa.

Muajiriwa anaweza kufanya kazi tu kwasababu ya passion lakini akawa anakipato kikubwa ambacho anakimiliki kuliko kile anacholipwa.

Hivi mtumwa anaweza kufanya application ya kuomba kazi ya utumwa?

Kuna mchezaji wa mpira anaitwa Faiq Bolkiah huyu aliwahi kucheza pale Chelsea timu ya vijana ila kwa sasa nadhani yupo kwenye ligi za Asia.

Huyu ndio mchezaji mwenye utajiri kuliko wote hata wakijichanga Messi na Ronaldo hawafiki robo ya utajiri wake.

Lakini kwasababu passion yake ni soka basi amejikuta amekuwa muajiriwa kwenye hiyo kazi na mashahara wake ni mdogo tu.

Kwa hiyo sio kweli kuwa muajiriwa ni mtumwa
 
Hapo kwenye Kumuamini Yesu Kristo na Kubatizwa unakua umeokoka, umeitoa katika Mstari gani?
 
Ok sawa kijana, uko vizuri kwa ujenzi wa hoja, lkn chunga sana maana watu wa fact walimkosa Mungu. Yesu anasema "nakushukuru Mungu kwakuwa neno hili umewafunulia masikini". Kutumia neno YUPO isikutishe sana maana tayari nimeshahakiki kwamba yupo. Alafu akili yangu haipo kuchunguza makosa yauandishi ikiwa nitatambua kwamba msomaji lazima atapata mantiki.kikubwa tujadili hoja husika. Inasikitisha kuona mjenzi mzuri wa hoja Kama wewe kutetea Jambo lisilo na maslahi kwa maisha ya wengi. Hakuna unalopata zaidi yakushusha imani za wengi, heri kufungwa jiwe nakutoswa baharini. Kumbuka bila imani hizi za dini dunia haiwezi kuwa mahala salama pakuishi.
 
Thibitisha Mungu na Yesu wapo

Kwasababu hata mimi naweza kuja na masimulizi ya Unicorn hapa nikayasimulia kama yalivyoaandikwa lakini haina maana kuwa yana uhalisia
 
Mbona mpaka leo hii wa israel kizazi cha leo hawamtambui Yesu wala dini ya ukristo?
Swali gumu kulijibu kwa vile linakinzana na hurka, utashi, mamboleo na mantiki!

Dini aliyoihubiri Yesu na ile inayohubiriwa zama za baada ya kuondoka kwake duniani ni tofauti kama ilivyo usiku na mchana!
 
Thibitisha Mungu na Yesu wapo

Kwasababu hata mimi naweza kuja na masimulizi ya Unicorn hapa nikayasimulia kama yalivyoaandikwa lakini haina maana kuwa yana uhalisia
Kuliishi neno lake na kufata sheria zake Ni uthibitisho tosha kwamba yesu yupo. Kingine labda kufunga na kuomba japo njia hii huwa Mara chache kajidhihirisha. Onyo! Isiwe kwakumjaribu.
 
Yesu kwa kinywa chake kasema hajatumwa ila kwa wana wa Israel waliopote, wengine ni kujipendekeza tu
 
indoctrinations inaweza kuondolewa kwa hoja mbadala zenye ushawishi, mashiko na zilizojengwa kwa mantiki.
Vinginevyo unabaki kuwa mateka wa propanga potofu za mamboleo zinazojengwa kwa kuzingatia zaidi maslahi ya kidunia.
 
Kuliishi neno lake na kufata sheria zake Ni uthibitisho tosha kwamba yesu yupo. Kingine labda kufunga na kuomba japo njia hii huwa Mara chache kajidhihirisha. Onyo! Isiwe kwakumjaribu.
Unapataje guts za kudai ni neno lake kwenye jambo ambalo bado hujalifanyia tafiti?

Kufata sheria sio uthibitisho kuwa kitu fulani kipo.

Sheria inaweza kuwepo tu kwasababu mtu fulani mwenye power kataka iwe hivyo.

Kuna jamii ya Aztec ilikuwa ina abudu Mungu wa mvua ambapo kulikuwa na miongozo na sheria za kuzifuata ili kwenda sawa na yeye.

Watu wa jamii hiyo waliamini mafuriko yanatokana kwasababu ya hasira za huyo Mungu wao na namna pekee ya kutuliza hasira yake ni kutoa kafara ya watoto bikra.

Sasa kwasababu kuua watoto wadogo ni sehemu ya sheria ya huyo Mungu, je hiyo inafanya huyo Mungu mvua awepo??
 
indoctrinations inaweza kuondolewa kwa hoja mbadala zenye ushawishi, mashiko na zilizojengwa kwa mantiki.
Vinginevyo unabaki kuwa mateka wa propanga potofu za mamboleo zinazojengwa kwa kuzingatia zaidi maslahi ya kidunia.
Heavily indoctrinated religious people kimsingi ni ngumu sana kudili nao kwasababu ubongo wao unakuwa tayari umebadilika na watafanya kila kitu kutetea irrational beliefs.
 
Kwahiyo unaamini Kama kuwatoa watoto kafara Ni kosa? Kivipi Ni kosa. Kama mtu Fulani mwenye power aliandika ninachoamini basi anafaa kuzingatiwa sana maana sio wakawaida huyo.
 
Heavily indoctrinated religious people kimsingi ni ngumu sana kudili nao kwasababu ubongo wao unakuwa tayari umebadilika na watafanya kila kitu kutetea irrational beliefs.
Ni stress kudhani hakuna Mungu, sababu amani ya moyo usioamini Mungu inaleta uadui kati ya mtu na nafsi yake.
 
Naamini kuna mungu ila yesu sijui mhamaed wote walikuwa na akili nyingi tu wakati ule kama kina masanja tu tunaowaona leo
 
Kwahiyo unaamini Kama kuwatoa watoto kafara Ni kosa? Kivipi Ni kosa. Kama mtu Fulani mwenye power aliandika ninachoamini basi anafaa kuzingatiwa sana maana sio wakawaida huyo.
Usitoke nje ya key

Thibitisha Mungu na Yesu wapo
 
Usitoke nje ya key

Thibitisha Mungu na Yesu wapo
Unajua ndugu, wewe tayari unafikra tofauti juu ya uthibitisho wa Mungu na yesu hivyo kilichokufanya kutokuamini ndicho kinachokuongoza kwa Sasa. Zaidi tu nikukuhimiza kutafakari kwakina maneno matakatifu huenda ukapata neema. Maana sidhani Kama takuwa na maneno mazuri kuzidi Yale yaliyo ndani ya imani yangu na ambayo yananiongoza Mimi kwa Sasa. Au basi namwomba Mungu aingilie Kati labda kwakukutokea Kama alivyotokewa Paulo mtume. Nakusihi usisubiri Hilo kwani Ni wachache wanaopata neema hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…