Kwanini Wakristo wanaishabikia sana Israeli? Sababu hizi hapa

Kwhy sasa wana Israel haya yote wanayofanya ni wanapotoka ili waje wamkiri Yesu baadaye kwa mujibu biblia?
Sijui kama nimelielewa vizuri swali lako, ndugu yangu mswaki mbuyu
Biblia haisemi kuwa Waisraeli haya yote wanayofanya, wanapotoka ili baadaye waje wamkiri Yesu. Badala yake, inasema kwamba 'kwa sehemu ugumu umewapata Israeli' (Warumi 11:25)—yaani hawamtambui Yesu kuwa ni Masihi. Hali hiyo ya upofu wa kiroho haimaanishi kwamba Mungu ndiye anawafanya wapotoke ili waje wamkiri Yesu baadaye. La hasha. Makosa yao, kama ya watu wa taifa lolote, yanatokana na hiari yao wenyewe. Hata hivyo, mpango wa Mungu ni kwamba baada ya kipindi fulani, hasa hasa baada ya dhiki kuu, Waisraeli watamkiri Yesu kwa toba ya kweli. (Zekaria 12:10; Warumi 11:26).
 
Ukristo unatokana na injili ya Kristo .....je ni kweli siku ya sabato tusimtoe punda shimoni...huyo mwandishi anatuandikia ushirikina
 
Ooh kumbe mbeleni huko taifa la Israel litapatwa na jangaa la njaa ndo watamkiri Yesu?
Ila kwa haya wanayo yafanya ni upotofu wao tuu waliojitakia?
 
Hayo mafundisho wenzetu mnayatoa wapi, harafu unajulimlisha Wakristo wote, kana kwamba sisi sote ni bahokoli . Katika liturujia yetu sijaona maelekezo ya kuombea taifa fulani ndipo tupate waokovu au baraka.

Hayo unayoyaelekeza hapa tukianza kufafanua hatu uhuru tusingedai Kwa maana imeamuliwa umtii bwana wako ambaye ni mkoloni. Na wazungu wamekua kwa miaka maelfu wanatumiksha watu weusi Kwa kutafsri mistari na vifungu katika biblia kama wanavyofanya bahokoli/walokole . Inawezekana tafsri yako ilikuwa na maana katika wakati huo agano la kale , ujio wa Yesu kristo ulibadilisha mambo mengi ndo maana Leo kuna Ukristo duniani badala ya kuwa dini ya kabila fulani. Ruksa kukosoana kushauliana. Kama Kuna waroma hapa wanipe mwongozo liturujia yetu I'll hiyo Sala au maelekezo.
 
Huyu @satfree sijui hata maandiko yake anayatoa wapi?
 
Huwajui Mayahudi wewe ni watu wasioutaka ukristo kabisa na ni kosa la jinai kujaribu kumbadili Myahudi kuwa Mkristo huko Israel.
Miaka zaidi ya elfu mbili hawajamkubali Yesu sasa hiyo yako ya ".itakuja" siku ni Hekaya tuu.
 
Mafundisho mbona yapo kwenye bibilia na mtoa mada ameweka maandiko ya biblia kusindikiza hoja zake. Au nyie wakatoroka huwa hamsomi biblia mmeishia kukariri sala ya salam maria tu?!
 
We nawe hunaga mada za maana.
Mada ni zile zile uteule wa wayahudi na ushabiki wa wakristo kwao.
 
Achana na fikra tegemezi
 
Tangu lini ukawa upande wa waislamu, na mwisho wenu ni mbaya sana enyi mnaowasapoti wanywa damu za watoto, wamama na wazee.
 
Achana na fikra tegemezi
Siyo tegemezi kama unataki mimi nijiunge na dini yako nithamini kama binadamu lakini kama unaniona mtumwa au nyani kwa nini niswali swala tano na nihangaike na kupiga rakaa usiku mzima ?
 
Kwahiyo wachina wajapani na wakolea wamebalikiwa baada ya kuwasujudia wazungu/waisrael, hizo ndizo fikra potofu zinazorudisha nyuma waafrika na Africa. Au hiyo amri inakuhusu wewe mweusi tu?
 
wazungu wamejua kutunga mambo/maneno kumdanganya mtu black aisee!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…