Kwanini walioshangilia kujeruhiwa kwa Tundu Lissu hawakukamatwa?

Kwanini walioshangilia kujeruhiwa kwa Tundu Lissu hawakukamatwa?

Kisasi cha mnyonge hulipwa na Mungu.

Ukipata madaraka, utambue kuwa huo ni wajibu tu, wala madaraka hayabadilishi ubinadamu wako. Wewe bado ni binadamu.
 
Katika hizi siku kadhaa za kifo cha magufuli kumeonekana kutokea kwa vitendo kadhaa vya kuonyesha furaha kwa baadhi ya watu na masikitiko kwa baadhi ya watu. Kwa kifupi kumekuwepo na hisia mseto juu ya kifo cha kiongozi Magufuli.

Lakini pamoja na hili kujitokeza tujaribu kurudi nyuma kidogo mwaka ambao Tundu Lisu alipigwa risasi nyingi huko Dodoma eneo la area D makazi ya viongozi wa serikali mchana kweupe na jua kali likiwaka watu wakabeza na kushangilia kwamba Lissu ni msaliti alitakiwa auwawe kabisa.

Katika hali isiyo ya kawaida na ya kusikitisha sana ni kwamba wale wote walioonesha hali ya kufurahi juu ya msiba huu wa Magufulu wamekuwa wakikamatwa na polisi na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria wakati huohuo wale wote waliofurahia Lisu kujeruhiwa wapo huru kukejeli popote pale na wakati wowote ule.

Inasikitisha kuona Tanzania hii chini ya serikali iliyokuwa ya Magufuli kuendeshwa kwa misingi ya uchama yaani polisi badala ya kufuata kanuni na sheria zinasemaje wao wanafanya mambo yao ili kuwafurahisha viongozi wao waliowaweka mamlakani. Ni mara nyingi kama sio mara zote tumeona namna ambavyo hao polisi wakitumika kuwakandamiza wale ambao wanasherehekea msiba wa Magufuli.

Ifike mahali serikali na polisi watambue waziwazi kuwa sherehe za namna hii zina root yake ambayo ni kutoka hukohuko serikalini Mbona alipokufa Mkapa watu hawakusherehekea? Mbona alipokufa Nyerere watu hawakusherehekea? Inakuwaje kifo cha Magufuli kiwaburudishe watu sana mioyoni mwao mpaka kufikia hatua ya kuandaa party kila kona?

Ifike mahali tukubali kuna mahali Magufuli aliteleza katika uongozi wake badala ya kuwaunganisha watu yeye akawagawa na haya ndio matokeo ya hilo pandikizo lake. Kwahiyo wala hata haishangazi kuona watu wakifurahia kifo cha mkuu magufuli hadharani maana ndio roho aliotaka watanzania wawe nayo.

Hatujasahau kauli zote za kina Cyprian Musiba, Paul Makonda, Bashiru Ally, Job Ndugai, Musukuma, na wengine wengi zote hizi zime precipitate kutokea hali tunayoiishi sasa hivi.

Natoa maoni yangu kwa mama Samia Suluhu apambane kwa hali na mali kuhakikisha Tanzania na Watanzania inarudi katika nyakati zile za upendo na mshikamano pasi na kuwa na itikadi za aina yoyote ya kupelekea uvunjivu wa amani miongoni mwetu. Ifike mahali tujifunze kwa kuamini kuwa Kiongozi unatakiwa uwe muunganisha watu sio mtenganisha watu.

Unaweza kutuwekea ushahidi wa hizo shangwe?
 
Kwenda zako kwani lissu alikua rais? Upumbavu wake wa kujibizana na kukejeli mamlaka ya rais hadi akawaaminisha maamuma wafuasi wake yeye ni sawa na rais [emoji23][emoji23]
Kwa mujibu wa katiba yetu, kila MTU ana haki ya KUISHI bila Kujali Ni Kiongozi Ama ni Raia Wa kawaida.
 
Tumepitia kipindi kigumu sana cha kuoongozwa na mwendawazimu. Ndiyo maana hata mission yake ili bumba big-time.

Still kwa kukataza watu wasimuone Lissu Nairobi Hospital, na kumnyima mshahara na kumnyang'anya ubunge na marupurupu inaacha ushahidi wa Mazingira kuwa Magufuli ndiye mhusika Mkuu wa operation ya kumuua Lissu.

All in All Mungu ameonyesha uwapo kwa Watanzania. Aliyetaka kumuua Lissu amekufa yeye na maiti yake inatembezwa kama biashara ya machinga mitaani

Aisee inafanyanywa nini? kama nini?
 
Ukiangalia kwa makini wanaoshangilia ni kama tone la maji baharini . Mafisadi na wapiga madili , wasio wazalendo . Mzalendo mwenye akili TIMAMU hawezi kushangilia . Walioshangilia watakutana na MAMA ambae ameahidi kuendeleza alipoachia JPM ,nawashauri wahame nchi .

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
 
Kwanza sio uungwana wala ubinadamu kushangilia kifo ama mateso ya mtu mwingine no matter what.

Pili kuna mzungu mmoja aliwahi kutudhihaki kuwa huku Afrika

"all animals are equal, but some are more equal"
Acha kubagua wa wazi mbona yeye alishangilia Mo kutekwa,?? hakutoa kauli za uchungu!!
Watu waishi km mashetani hivi hii ni haki kweli?tundu lisu ilikuwa amuue!!

Anzoli gwanda ana watoto ebu fikiria. Yule hata wewe ukimkalia vibaya hajali kuwa eti unampenda
Kuna mengi alikuwa anashangilia km Rais nimekupa kwa kifupi tu!!

Kumbuka mla kuku wa mwenziwe miguu humuelekea
 
Kwanza sio uungwana wala ubinadamu kushangilia kifo ama mateso ya mtu mwingine no matter what.

Pili kuna mzungu mmoja aliwahi kutudhihaki kuwa huku Afrika

"all animals are equal, but some are more equal"
Mkuu sentence ya mwisho umetupiga kamba, hiyo sentence ipo kwenye kitabu cha "The animal Farm " hiki kitabu kiliandikwa na mwandishi wa Kiingereza (I stand to be corrected) na wala hakikuwalenga waafrika.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Tumepitia kipindi kigumu sana cha kuoongozwa na mwendawazimu. Ndiyo maana hata mission yake ili bumba big-time.

Still kwa kukataza watu wasimuone Lissu Nairobi Hospital, na kumnyima mshahara na kumnyang'anya ubunge na marupurupu inaacha ushahidi wa Mazingira kuwa Magufuli ndiye mhusika Mkuu wa operation ya kumuua Lissu.

All in All Mungu ameonyesha uwapo kwa Watanzania. Aliyetaka kumuua Lissu amekufa yeye na maiti yake inatembezwa kama biashara ya machinga mitaani
Tena bila kujali!! wala chembe ya Huruma kuwa Lisu ana watoto mke na msomi.shindilia binadamu mwenzio km una ua nyoka!!!??? Aaaahh! Hapana.

vitoto vinasoma, vinakula.vinalia baba!!! Baba!!kuna nini!!
Jamani ebu mfikilie hili nalo.kisa mtu unataka madaraka??,
je sasa unayo? kwa Mungu utajibu nini??
Mbaya zaidi hukupata nafasi ya kutubu!!
 
Wewe ni zero brain sana,wapiga deal awamu ya JPM ndio walizidi sana. JPM alichofanya ni kuwaondoa wapiga dili wa Kikwete na kuweka wapiga deal wake, Makonda amekuwa bilionea kipindi cha Magufuli.
Tena amekuwa bilionea ndani ya kipindi cha miaka 3, mshahara wake ni around MIL 5, huyu anapaswa aandaliwe utaratibu afikishwe mahakama za mafisadi atuambie alipopata utajiri wa usiku mmoja

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom