Kwanini walioshangilia kujeruhiwa kwa Tundu Lissu hawakukamatwa?

Kwanini walioshangilia kujeruhiwa kwa Tundu Lissu hawakukamatwa?

Katika hizi siku kadhaa za kifo cha magufuli kumeonekana kutokea kwa vitendo kadhaa vya kuonyesha furaha kwa baadhi ya watu na masikitiko kwa baadhi ya watu. Kwa kifupi kumekuwepo na hisia mseto juu ya kifo cha kiongozi Magufuli.

Lakini pamoja na hili kujitokeza tujaribu kurudi nyuma kidogo mwaka ambao Tundu Lisu alipigwa risasi nyingi huko Dodoma eneo la area D makazi ya viongozi wa serikali mchana kweupe na jua kali likiwaka watu wakabeza na kushangilia kwamba Lissu ni msaliti alitakiwa auwawe kabisa.

Katika hali isiyo ya kawaida na ya kusikitisha sana ni kwamba wale wote walioonesha hali ya kufurahi juu ya msiba huu wa Magufulu wamekuwa wakikamatwa na polisi na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria wakati huohuo wale wote waliofurahia Lisu kujeruhiwa wapo huru kukejeli popote pale na wakati wowote ule.

Inasikitisha kuona Tanzania hii chini ya serikali iliyokuwa ya Magufuli kuendeshwa kwa misingi ya uchama yaani polisi badala ya kufuata kanuni na sheria zinasemaje wao wanafanya mambo yao ili kuwafurahisha viongozi wao waliowaweka mamlakani. Ni mara nyingi kama sio mara zote tumeona namna ambavyo hao polisi wakitumika kuwakandamiza wale ambao wanasherehekea msiba wa Magufuli.

Ifike mahali serikali na polisi watambue waziwazi kuwa sherehe za namna hii zina root yake ambayo ni kutoka hukohuko serikalini Mbona alipokufa Mkapa watu hawakusherehekea? Mbona alipokufa Nyerere watu hawakusherehekea? Inakuwaje kifo cha Magufuli kiwaburudishe watu sana mioyoni mwao mpaka kufikia hatua ya kuandaa party kila kona?

Ifike mahali tukubali kuna mahali Magufuli aliteleza katika uongozi wake badala ya kuwaunganisha watu yeye akawagawa na haya ndio matokeo ya hilo pandikizo lake. Kwahiyo wala hata haishangazi kuona watu wakifurahia kifo cha mkuu magufuli hadharani maana ndio roho aliotaka watanzania wawe nayo.

Hatujasahau kauli zote za kina Cyprian Musiba, Paul Makonda, Bashiru Ally, Job Ndugai, Musukuma, na wengine wengi zote hizi zime precipitate kutokea hali tunayoiishi sasa hivi.

Natoa maoni yangu kwa mama Samia Suluhu apambane kwa hali na mali kuhakikisha Tanzania na Watanzania inarudi katika nyakati zile za upendo na mshikamano pasi na kuwa na itikadi za aina yoyote ya kupelekea uvunjivu wa amani miongoni mwetu. Ifike mahali tujifunze kwa kuamini kuwa Kiongozi unatakiwa uwe muunganisha watu sio mtenganisha watu.
so far mpaka sasa magufuli ndo rais mbovu kuwahi kutokea Tanzania.chadema walivyotaka kumuombea tundu lissu polisi waliwapiga na kuchukua mashine zao za kuprint t shirt.ameligawanyisha sana taifa yule mzee.alipomgiga risasi tundu lissu ccm wakawa wanachekelea na kumwita tundu lissu mabaga fresh.je chadema wakimwita magufuli mzoga uliooza watakuwa wanakosea?
 
Lissu ni kama Huriah wa Biblia tu. Hii haikumzui Daudi kumzaa Suleimani Mfalme na mke wa Huriah mhiti.

Hii haikuzuia Watanzania kupitia familia ya Hayati JPM kutuambia kuhusu Neema ya Toba ya Bwana Yesu iliyomshukia JPM. Hata katika kitanda cha kifo chake tumeambiwa JPM alikuwa akimba nyimbo za kumtukuza na kumsifu Mungu na Bwana Yesu akiwahinikiza walio karibu naye kufanya hivyo.

Unajua maandiko ya Mungu yanavyo sema ?, "Wawapo wawili au watatu kwa ajili ya jina langu Mimi Mungu wa Mbinguni niko kati yao."
Jua fika wakati wanaimba nyimbo za kumsifu Mungu yeye JPM na walio mzunguka hapo katika death bed/room Mungu alikuwa kati yao.

Tengeneza njia yako achana na JPM yeye Vita kapiga vizuri na Imani aliilinda. Ushuhuda uko wazi. Usije ukakutwa na kifo ukiwa umezungukwa hapo utakapofia na jopo la walozi wakiwa wamesindikizwa na mizimu yao wanayo iabudu.
Pia Biblia inasema mshahara wa dhambi ni mauti.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu sentence ya mwisho umetupiga kamba, hiyo sentence ipo kwenye kitabu cha "The animal Farm " hiki kitabu kiliandikwa na mwandishi wa Kiingereza (I stand to be corrected) na wala hakikuwalenga waafrika.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
Daaa! Kukariri shida sana mara nyingi hawanaga akili.
Sasa huo msemo uko kwenye kitabu hicho tuuu!!
Misemo unaweza tumia popote na ukaisoma popote.kakitabu kako kamoja hako ndo unakuja kutukoga hapa.!!! Eeen!!
watu wenye akili fupi sana ni pamoja na wewe.mnawazaga nini
 
Ukiangalia kwa makini wanaoshangilia ni kama tone la maji baharini . Mafisadi na wapiga madili , wasio wazalendo . Mzalendo mwenye akili TIMAMU hawezi kushangilia . Walioshangilia watakutana na MAMA ambae ameahidi kuendeleza alipoachia JPM ,nawashauri wahame nchi .

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
Mama ni mkali na hataki ujinga, ila hana viashiria vya kutumia magenge ya kihalifu kupambana na raia, waswahili wana werevu na staha za kudeal na maadui zao, jifunze kutoka kwa JK.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Daaa! Kukariri shida sana mara nyingi hawanaga akili.
Sasa huo msemo uko kwenye kitabu hicho tuuu!!
Misemo unaweza tumia popote na ukaisoma popote.kakitabu kako kamoja hako ndo unakuja kutukoga hapa.!!! Eeen!!
watu wenye akili fupi sana ni pamoja na wewe.mnawazaga nini
Huu ni msemo maarufu katika hicho kitabu, sasa tuambie jina la huyo mzungu na ni wapi alizungumza hiyo kauli, ujinga na kubishana na vitu vilivyo dhahiri, ulifikiri unawadanganya watoto wa chekechea??

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Lissu ni kama Huriah wa Biblia tu. Hii haikumzui Daudi kumzaa Suleimani Mfalme na mke wa Huriah mhiti.

Hii haikuzuia Watanzania kupitia familia ya Hayati JPM kutuambia kuhusu Neema ya Toba ya Bwana Yesu iliyomshukia JPM. Hata katika kitanda cha kifo chake tumeambiwa JPM alikuwa akimba nyimbo za kumtukuza na kumsifu Mungu na Bwana Yesu akiwahinikiza walio karibu naye kufanya hivyo.

Unajua maandiko ya Mungu yanavyo sema ?, "Wawapo wawili au watatu kwa ajili ya jina langu Mimi Mungu wa Mbinguni niko kati yao."
Jua fika wakati wanaimba nyimbo za kumsifu Mungu yeye JPM na walio mzunguka hapo katika death bed/room Mungu alikuwa kati yao.

Tengeneza njia yako achana na JPM yeye Vita kapiga vizuri na Imani aliilinda. Ushuhuda uko wazi. Usije ukakutwa na kifo ukiwa umezungukwa hapo utakapofia na jopo la walozi wakiwa wamesindikizwa na mizimu yao wanayo iabudu.
Bahati mbaya uneandika mambo ya Kikristu kwa mtu ambaye hakuwa Mkristu. Ukristu ni kumkubali Bwana yetu Yesu Kristu na kumuishi kimatendo.

Magufuli hakuwa Mkristu kwa vitendo vyake bali alitumia jukwaa la Kikristu kujijenga kisiasa. Angekuwa Mkristu asingefanya vitendo vya KIFEDHULI ambavyo tumeviona kwenye Utawala wake Kama Wizi, uuaji, utekaji, chuki, kubambikiza kesi watu na uwongo.

HASIRA ya Mungu imemteremkia hasa baada ya kuiba uchaguzi wa 2020 na kutaka awe Rais wa maisha. Yule ni wa Shetani tu
 
so far mpaka sasa magufuli ndo rais mbovu kuwahi kutokea Tanzania.chadema walivyotaka kumuombea tundu lissu polisi waliwapiga na kuchukua mashine zao za kuprint t shirt.ameligawanyisha sana taifa yule mzee.alipomgiga risasi tundu lissu ccm wakawa wanachekelea na kumwita tundu lissu mabaga fresh.je chadema wakimwita magufuli mzoga uliooza watakuwa wanakosea?
Mambo ya mabaga fresh na mzoga si mazuri
 
Kwa sababu aliyetakiwa kutoa amri ya kuwakamata ndio aliyetoa amri ya Tundu Lissu kupigwa risasi
 
Bahati mbaya uneandika mambo ya Kikristu kwa mtu ambaye hakuwa Mkristu. Ukristu ni kumkubali Bwana yetu Yesu Kristu na kumuishi kimatendo.

Magufuli hakuwa Mkristu kwa vitendo vyake bali alitumia jukwaa la Kikristu kujijenga kisiasa. Angekuwa Mkristu asingefanya vitendo vya KIFEDHULI ambavyo tumeviona kwenye Utawala wake Kama Wizi, uuaji, utekaji, chuki, kubambikiza kesi watu na uwongo.

HASIRA ya Mungu imemteremkia hasa baada ya kuiba uchaguzi wa 2020 na kutaka awe Rais wa maisha. Yule ni wa Shetani tu

Jidanganye wewe mamlaka zote za wanadamu hutoka kwa Mungu. Ndio maana nikasema Mfalme Solomoni alijenga madhabahu kwa wake zake wa amini mabaal. Mungu huangalia mwisho wa mtu wake. Tumeshuhudiwa mwisho wa Mh JPM ulikuwa vipi.
 
Sina uhakika kama unaelewa ni mauti yapi yanayo zungumziwa na hii Biblia?
Msaidie Lissu apate hekima ya kwa nini mpaka leo anaishi? Haja alewa kusudi la Neema ya Mungu juu yake.
Mkishashiba mihogo kama nguruwe pori huwa mnajiona smart sana, hivi wewe una akili zipi za kumshauri TL?

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Hawa watu wanajiona wao ni bora kuliko Watanzania wenye mitazamo na itikadi tofauti na wao.

Uzuri wote tutaishia kaburini na tutaoza na kubaki mavumbi matupu.
Wakamate au kama una ushahidi upeleke polisi ufungue kesi
 
Back
Top Bottom