Kwanini waliotuletea mahindi wao hawali ugali?

Post #3 ina ugali samaki na mboga.

Mimi nazungumzia ugali. Siongelei samaki na mboga.

Ugali mweupe hauna protein. Ni wanga mtupu.

Tunapokoboa tunatupa protein yote.
Nilikuelewa, lakini huwa hatuli ugali mkavu, ndio maana nikakwambia kuna picha ina nishati, protein na fibers hapo juu.
 
Ugali ni varieties tu ya Mahindi. Hata wazungu wanakula sana vyakula vinavyotokana na Mahindi

Moja ya Sababu watu wa Ughaibuni wanakuwa wanene na kupata magonjwa ya kisasa ni hayo mahindi.

Sisi tuna afadhali sana compare na hao walioyaleta.
Ugali sio aina ya mahindi bali ni bidhaa ya kuchakata itokanayo na mahindi, ikiwa sembe inakuwa ni mahindi yaliyochakatwa zaidi kwa kuondoa virutubisho vingi zaidi.
 
5aa607ac773fd9865370554217a706e1.jpg

karibuni wadau...
 
Nilikuelewa, lakini huwa hatuli ugali mkavu, ndio maana nikakwambia kuna picha ina nishati, protein na fibers hapo juu.
Mimi nazungumzia ugali kama ugali wenyewe. Mfano viazi, ndizi na mihogo vinalika vyenyewe bila kutegemea kiambatanisho kingine ila ugali haiwezekani.
 
Na mimi najua hamli igali mkavu.

Ila nasema kuwa mnatupa protein kwa kukoboa mahindi.

Thread inaongelea ugali, si ugali samaki na mboga.
Mleta uzi alikosea, Ugali hauliwi mkavu. Labda kama alimaanisha Uji. Anyway unaeleweka.
 
Post #3 ina ugali samaki na mboga.

Mimi nazungumzia ugali. Siongelei samaki na mboga.

Ugali mweupe hauna protein. Ni wanga mtupu.

Tunapokoboa tunatupa protein yote.
Mkuu hakuna tatizo kula wanga kwani wanga ni moja kati ya mahitaji ya miili yetu.
 
Mimi nazungumzia ugali kama ugali wenyewe. Mfano viazi, ndizi na mihogo vinalika vyenyewe bila kutegemea kiambatanisho kingine ila ugali haiwezekani.
Sawa, ugali wa mahindi unaweza kulika mkavu, ila ila isiwe ligi sasa ila unalika, na pia kama hakuna kiambatanisho tulikuwa tuna pika uji.
 
Ugali ni chakula cha kushangaza ambacho hupendwa sana na watu wengi Africa Mashariki, kati na magharibi. Tatizo la ugali ni kwamba hauna ladha, hauliki wenyewe bila chakula cha ziada.

Wazungu waliotuletea mahindi Africa karne ya 17 wao hawali ugali, wachache wanaokula wameendelea kula mahindi ya kuchemsha badala ya ugali.

Hakuna namna Waafrika tumeingizwa kingi kwenye hiki chakula kweli??
Mkuu ugali si ni wanga,na wanga ni moja ya hitajio la mwili,hivyo ugali unatupa wanga na logically basi tunauhitaji.

hivyo mkuu ugali ni salama kabisa kuula na wala hauna tatizo lolote na mara nyingi ugali huliwa na mboga pembeni.
 
Mleta uzi alikosea, Ugali hauliwi mkavu. Labda kama alimaanisha Uji. Anyway unaeleweka.
Wewe ndiye hujaelewa hoja.

Kama ugali unaweza kukupa protein, ukaitupa protein ukala wanga tu, hilo ni tatizo.

Huelewi wapi?

Tanzania ina matatizo makubwa ya malnutrition, hao samaki na nyama ya kutoa protein sehemu nyingine ni anasa. Badala ya gharama za ziada kupata protein kwenye samaki na mboga na nyama, protein ingeweza kupatikana hata kwenye ugali.

Mbona nimesema nimekuelewa? Nilichoongeza ni kwamba hakuna jamii inayokula ugali mkavu, jamii zetu zote hula ugali na kiambatanisho fulani siyo lazima iwe samaki.

Kwa hoja yako nikasema labda upikwe uji.
 
Na uji sio ugali tena
 
Mbona nimesema nimekuelewa? Nilichoongeza ni kwamba hakuna jamii inayokula ugali mkavu, jamii zetu zote hula ugali na kiambatanisho fulani siyo lazima iwe samaki.

Kwa hoja yako nikasema labda upikwe uji.
Sasa ukila sembe na mchicha au mlenda protein unaipataje??
 
Mkuu ugali si ni wanga,na wanga ni moja ya hitajio la mwili,hivyo ugali unatupa wanga na logically basi tunauhitaji.

hivyo mkuu ugali ni salama kabisa kuula na wala hauna tatizo lolote na mara nyingi ugali huliwa na mboga pembeni.
Kwa nini waliotuletea mahindi wao hawali ugali??
 
Mbona nimesema nimekuelewa? Nilichoongeza ni kwamba hakuna jamii inayokula ugali mkavu, jamii zetu zote hula ugali na kiambatanisho fulani siyo lazima iwe samaki.

Kwa hoja yako nikasema labda upikwe uji.
Hujaelewa hoja ni ugali, si ugali na mboga.

Kwa nini somo hili linakuwa gumu sana kuelewa?

Kama unaweza kupata protein kwenye ugali na mboga kwa nini utupe protein ya kwenye ugali?
 
Sidhani kama watakula sembe na mchicha kila siku, naamini kunasiku protein ya aina yoyote itakatiza mitaa hiyo.
Protein ndio inatakiwa ule kila siku na karibia kila mlo, wanga ukisubiria ukatize mitaa yako au hata usipokula kabisa hakuna shida yoyote kubwa unayoweza kupata.
 
Back
Top Bottom