Kwanini waliotuletea mahindi wao hawali ugali?

Protein ni kitu unachotakiwa kula kila siku, ndiyo maana kuna viwango vya daily intake vya protein, hujui hilo?
Daily intake nchi hii au mnaongelea wapi? Maisha ya Tanzania tunatafuta ugali kwanza, yani kidume unahakikisha unga upo ndani, hizo protein ni matokeo tu. Kwa hiyo hizo protein daily value nchi hii ni mtihani sana wakuu.
 
Nakwambia ugali unaweza kuwa na protein, bado huelewi somo.
 
Cha mzungu na cha kwetu hakiwezi kuwa sawa especially kwenye vitu vya misaada. Wengi wetu tunafahamu kabisa mahindi yao yankuzwa artificially sana. Hivyo kiwango cha virutubisho asilia ni vidogo mno na vinavyopatikana hujakuongezewa tu na wanakemia.

Mwisho wa siku ugali wetu utabaki kuwa salama na bora zaidi. Mwisho wa siku ni hilo janga la njaa tu lituepuke la sivyo itatulazimu tule kemikali zao.

All in all Muthungu sio wa kumwamini
 
Ndio chakula pekee duniani ukiweka chumvi au mafuta hakiivi.Hata kwenye bible naona watu ,walikuwa wanatembea na ngano mwanzo mwisho.Si tatizo hili mjomba wangu.Pia hata kwenye tafrija za huku mkoani kwetu sijawahi kuona wageni wameandaliwa ugali.
 
Mimi nazungumzia ugali kama ugali wenyewe. Mfano viazi, ndizi na mihogo vinalika vyenyewe bila kutegemea kiambatanisho kingine ila ugali haiwezekani.
Unaweza kula mahindi Yakiwa mabichi ya kuchemshwa au kuchoma. Hao wazungu wanakula hivyo kabla ya kuprocess hatua ya kuwa ugali.
Ugali ni hatua ya mwisho usiseme viazi au mihogo hata vyenyewe vinaleta Unga. Kuna ugali wa muhogo, kuna matobolwa au michembe ya viazi nk
 
Kwa nini mzungu yeye hali huo ugali??
Mkuu mi nadhani Kila bara Lina asili ya chakula chake. Kwakweli ni ngumu sana sisi waafrika kuachana na ugali ukiendana na nature yetu na Wala Sioni tatizo la ugali na hata ukileta reason zako au madhara Yako hapa bila shaka utasema utafiti uliofanywa na chuo kikuu Cha oxford katika Nchi ya uingereza unasema una ugali una madhara haya na Yale!!

Hayo ndo aliyakataa kishimba kwamba hata utafiti tunaofanyiwa na kuutumia tunafanyiww na wale ambao huko hivyo vutu havijawahi kuwapo unategemea nn?

Ugali na baadhi ya vyakula vimetufanya tuwe na nguvu mara dufu na afya kamili na sambamba na vyakula vyetu vya asili.

Ukisema tule kama wao vile tu wao hawali kama sisi ni ujinga na upubavu wa Hali juu. Sisi si kama wao na wao sio kama sisi.
 
Ugali ni chakula cha kushangaza ambacho hupendwa sana na watu wengi Africa Mashariki, kati na magharibi. Tatizo la ugali ni kwamba hauna ladha, hauliki wenyewe bila chakula cha ziada.

Wazungu waliotuletea mahindi Africa karne ya 17 wao hawali ugali, wachache wanaokula wameendelea kula mahindi ya kuchemsha badala ya ugali.

Hakuna namna Waafrika tumeingizwa kingi kwenye hiki chakula kweli??
Ni survival food, bila ugali na vaccinations population ya Africa ingekuwa close to zero
 
Ugali ni chakula cha kushangaza ambacho hupendwa sana na watu wengi Africa Mashariki, kati na magharibi. Tatizo la ugali ni kwamba hauna ladha, hauliki wenyewe bila chakula cha ziada.

Wazungu waliotuletea mahindi Africa karne ya 17 wao hawali ugali, wachache wanaokula wameendelea kula mahindi ya kuchemsha badala ya ugali.

Hakuna namna Waafrika tumeingizwa kingi kwenye hiki chakula kweli??
Ni kama wale wanaoimbisha usiku kucha kwenye mikesha, ukifuatilia matendo yao utachoka
 
Cha mzungu na cha kwetu hakiwezi kuwa sawa especially kwenye vitu vya misaada. Wengi wetu tunafahamu kabisa mahindi yao yankuzwa artificially sana. Hivyo kiwango cha virutubisho asilia ni vidogo mno na vinavyopatikana hujakuongezewa tu na wanakemia.

Mwisho wa siku ugali wetu utabaki kuwa salama na bora zaidi. Mwisho wa siku ni hilo janga la njaa tu lituepuke la sivyo itatulazimu tule kemikali zao.

All in all Muthungu sio wa kumwamini
Aliyeleta mahindi Africa ni mzungu lakini huwa hali huo ugali wako, wanakula mahindi ya kuchemsha. Achana na hizo story kwamba mazao ya mzungu yanakosa Virutubisho kwa sababu yanayooteshwa artificially, mahindi yanayolimwa Africa yanawekwa mbolea na dawa hizo hizo zinazotumika Marekani na Ulaya.
 
Unaweza kula mahindi Yakiwa mabichi ya kuchemshwa au kuchoma. Hao wazungu wanakula hivyo kabla ya kuprocess hatua ya kuwa ugali.
Ugali ni hatua ya mwisho usiseme viazi au mihogo hata vyenyewe vinaleta Unga. Kuna ugali wa muhogo, kuna matobolwa au michembe ya viazi nk
Mimi naongelea ugali na mahindi
 
Ugali ni chakula cha kushangaza ambacho hupendwa sana na watu wengi Africa Mashariki, kati na magharibi. Tatizo la ugali ni kwamba hauna ladha, hauliki wenyewe bila chakula cha ziada.

Wazungu waliotuletea mahindi Africa karne ya 17 wao hawali ugali, wachache wanaokula wameendelea kula mahindi ya kuchemsha badala ya ugali.

Hakuna namna Waafrika tumeingizwa kingi kwenye hiki chakula kweli??
Chakula gani unaweza kula bila chakula cha ziaga? Embu niambie
 
Back
Top Bottom