Kwanini waliotuletea mahindi wao hawali ugali?

Kwanini waliotuletea mahindi wao hawali ugali?

Ugali sio aina ya mahindi bali ni bidhaa ya kuchakata itokanayo na mahindi, ikiwa sembe inakuwa ni mahindi yaliyochakatwa zaidi kwa kuondoa virutubisho vingi zaidi.
Haibadilishi maana, ingredients tunazo Consume kula ugali na ingredient wanazo consume wazungu ni zile zile, wao zinawasumbua na sisi pia zinatusumbua.
 
 
Ugali huwa haupiti kabisa, tena ukishakobolewa ndio kabisaa

Chakula changu kikuu ni wali
 
Nakwambia ugali unaweza kuwa na protein, bado huelewi somo.
Asilimia kubwa ya watu wanakula vitu pasipokujua vina virutubisho vya aina aina gani na vina kazi gani!
Wanachozingatia ni ladha mdomoni, kumbe mtu unaweza ukala ugali mkavu usiokobolewa na maji na ukaishi
Afu mfano unaweza kula mende au mijusi na ukapata protein tu kama samaki
 
Wao wanalima halafu wanalishia mifugo
Wewe ukilima ukawapa mifugo bongo waswahili watakuuwa wakati shamba lako, unalima wewe, na mifugo ya kwako

Niliwapa matikiti kuku wangu jamaa akawanyang'anya na kusema eti kufuru 😄
 
Mbona nimesema nimekuelewa? Nilichoongeza ni kwamba hakuna jamii inayokula ugali mkavu, jamii zetu zote hula ugali na kiambatanisho fulani siyo lazima iwe samaki.

Kwa hoja yako nikasema labda upikwe uji.
Tunaongelea ugali pekee mkuu
 
Cha mzungu na cha kwetu hakiwezi kuwa sawa especially kwenye vitu vya misaada. Wengi wetu tunafahamu kabisa mahindi yao yankuzwa artificially sana. Hivyo kiwango cha virutubisho asilia ni vidogo mno na vinavyopatikana hujakuongezewa tu na wanakemia.

Mwisho wa siku ugali wetu utabaki kuwa salama na bora zaidi. Mwisho wa siku ni hilo janga la njaa tu lituepuke la sivyo itatulazimu tule kemikali zao.

All in all Muthungu sio wa kumwamini
Salama kivipi wakati mahindi mengi yanayokuja kuzalisha ugali ni mbegu za GMO sasa huo usalama uko wapi? Watu tunajali uzalishaji mwingi hivyo mahindi yanayopendwa ni GMO ili kupata uzalishaji mkubwa mahindi ya asili sijui unaweza yapata wapi kwa sasa.
 
Hawali ugali ila wanayatumia kutengeneza cornflour ambayo inakuja kutumika kwenye mapishi yao(pamoja na yetu) hasa kwenye pastry
1723455213586.png
1723455258975.png

Tunatofautiana matumizi tu
 
Back
Top Bottom