Kwa watu wa vijijini ,ugali ni muhimu sana katika mlo wa kila siku kwasababu unawapa nishati ya kufanya kazi ngumu kama kulima,kutembea umbali mrefu kukata kuni,kuteka maji n.k ila kwa watu wa mjini ambao kazi nyingi ni za kukaa na hawatembei sana kwa miguu, ugali kwao sio muhimu sana kwani unaweza kuwaletea vitambi