CORAL
JF-Expert Member
- Jun 26, 2011
- 2,813
- 1,827
Shida ni kwamba mitihani ya kuchagua majibu haimpimi vema mwanafunzi. Si lazima mtu ajue kuandika ili aweze kuchagua majibu na kushade kwa penseli.Kama mitihani ya darasa la saba haiaminiki, sasa kwanini tuendelee kuamini ubora wa mitihani ya kidato cha pili na cha nne?
Angalau sekondari kuna maswali ya kutumia akili na kujieleza ingawa pia kuna mapungufu yake.
Halafu tambua kuwa wanafunzi wanasakwa sana wakati wa mitihani ya mwisho. Hata mwanafunzi aliyeacha shule anafanya umachinga au kaolewa, wakati wa mtihani atanyofolewa huko aliko kuja kufanya mitihani. Halafu utakuta kapasua sana eti unampanga darasa la sayansi wakati anatakiwa kurudi kwa mume au kibaruani imara moja.