Kwanini wanafunzi wasianze kidato cha kwanza na michepuo ya sayansi (Physics, Chemistry) au arts kwa kuzingatia matokeo ya Darasa la Saba?

Lengo la mwanafunzi wa O'level kusoma masomo yote nikupata foundation knowledge ya somo husika ebu fikiria mtoto atakapoanza kidato cha kwanza asisome biolojia, mwisho wa siku utakuta huyo mwanafunzi hawezi ata kujua makundi ya chakula na kazi zake mwilini, mfumo wa kusoma masomo yote kwa vidato vya chini nikumpa mtoto ile general views ya somo husika ambayo itakuwa faida yake mwenyewe katika maisha ya kila siku,
uko sahihi
 
Ndio nilitaka kukisema hiki ila umenisemea tayari.
Kwa mfano mimi shule ya msingi masomo ya sayansi nilikuwa siyapendi na nilikuwa mdhaifu lakini nilivyofika sekondari nikawa mtabe kwenye masomo ya sayansi na ndio yanayonipa msosi hii leo.
Mimi wapo ninaowajua walikuwa hatari sana katika somo la sayansi primary na mpaka secondary wakawa bado wanatesa.

Vp wanao-fail masomo ya sayansi katika mtihani wa mchuyo wa kidato cha pili na kuambiwa kwenye mchepuo wa arts? Ina maana licha ya ku-fail kwako wanaweza kubadilika huko mbeleni na kufanya vema katika matokeo ya kidato cha nne?...
 
Ndio hvyo.
Kufeli kwa mwanafunzi hutegemea condition tu ya wakati huo wa mtihani sio kitu permanent.
Kufaulu mtihani hutegemea vitu vifuatavyo
1.Maandalizi wakati huo wa mtihani
2.Confidence wakati huo wa mtihani,mwanafunzi anaweza kujiandaa vizuri na kuelewa concepts zote lakini akakosa confidence akafeli.
3.Mood ya wakati huo wa mtihani,mwanafunzi anaweza akajiandaa vizuri lakini akashindwa kufaulu kutokana na stress alizonazo wakati huo.
Wewe hujawahi kuona mwanafunzi anafeli darasa la 7 kisha anafeli form 4 Lakini anapasua form 6 na kuingia chuo kikuu.
Halafu mwanafunzi mwingine anafaulu darasa la 7,anafaulu form 4 Lakini anafeli form 6 anakwama kuingia chuo kikuu.
Wewe unafikiri sababu ni nini?
 
Nimechelewa kwenye mjadala.

Kabla hujaamua hivyo inabidi kwanza ujiulize lengo kuu la elimu katika maisha ya binadamu ni nini hasa? Kama ni kumpatia ajira tu basi uko sahihi. Specialization zianze mapema kadri inavyowezekana.

Kama lengo mojawapo la elimu ni kumpatia binadamu maarifa ya jumla kuhusu mazingira yake na yeye mwenyewe basi kuchelewesha specialization kama inavyofanyika sasa ni sahihi. Kila mtu anahitaji angalau maarifa ya msingi katika sayansi ili angalau awe na fununu kuhusu mambo yalivyo hapa duniani. Biology inampa fununu kuhusu mfumo wa maisha kwa ujumla, Kemia juu ya mambo mbalimbali yanayomzunguka na Fizikia kanuni za msingi zinazoendesha ulimwengu na vitu anavyoviona na visivyoonekana. Kama akinogewa basi kidato cha tatu na kuendelea huko akazane zaidi na high school basi anaachiwa kabisa.

Kuhusu masomo ya sanaa sasa. Kila binadamu pia anahitaji kujua historia yake - alikotoka na anakokwenda. Jiografia inamwonyesha mambo mbalimbali katika mazingira yake na katika Civics anajifunza mifumo ya kiutawala inayoendesha maisha yake. Lugha na fasihi lengo lake kuu ni kupanua wigo wake wa kufikiri na kuchambua mambo. Ndiyo maana hata katika Academy za akina Plato na Pythagoras, somo kuu lilikuwa ni hesabu lakini fasihi na sarufi yalikuwa pia masomo ya lazima. Mtu aliyesoma sayansi kuanzia la saba/nne sijui atakuwa mtu wa aina gani. Ndiyo maana kuna hoja kuwa wanasayansi wengi huwa siyo wanasiasa/viongozi wazuri kwa sababu mfumo wao wa kufikiri umejibana katika misingi ya sayansi wakati binadamu wanayetaka kumtawala na kumwongoza ni kiumbe tata sana mwenye mahitaji mengi kijamii, kisiasa, kiuchumi na hata kiroho.

Isitoshe, darasa la 7 wanafunzi wanakuwa bado wadogo sana na ubongo wao ndiyo uko katika makuzi ya haraka. Wengi wao wanakuwa bado hata hawajui wanachokipenda na uwezo wao wa kuchanganua mambo ni hafifu mno. Kuendelea kuwafundisha masomo yote ni kuwapa nafasi ya kukua kidogo kabla hawajachukua jukumu kubwa na zito la kuchagua nini cha kusomea.

Kwa ujumla tu ni kwamba; kama unataka kuzalisha watu ambao angalau wana elimu kidogo kuhusu mambo ya msingi na wanaoyaelewa mazingira yao na ulimwengu huu basi wape maarifa ya jumla kwanza kabla hawajajibana katika vitaaluma vyao. Na karibu dunia nzima watoto hupewa nafasi hii. Ila kama unataka kuzalisha maroboti - watu ambao hawajui kingine cho chote isipokuwa kaeneo kao kadogo tu walikosomea basi anzisha specialization hata wakiwa darasa la kwanza au la nne ila tambua tu kuwa utakuwa na taifa la ajabu sana!
Nakazia
 
Sawa mkuu...
 
Mkuu, kwa maelezo yote haya uliyoyatoa ina maana basi wanafunzi woooote wa secondary wasome masomo sawa mpaka form 4. Hii ndio mantiki niliyoipata katika huu ufafanuzi wako mrefu.
 
ahsante sana
 
Mkuu, lengo la elimu hapa Afrika ni lipi haswa katika ya kumpatia mtu ajira na kumpa maarifa ya kimaisha?
 
Kwanini wanafunzi wasianze kidato cha kwanza "directly" na michepuo ya sayansi (Physics, Chemistry) au arts kwa kuzingatia matokeo ya darasa la saba na sio kusubiri mpaka afike kidato cha pili?

Umesahau Bookkeeping na Commerce mkuu....au hawa tuachane nao???
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu watanzania eti;

Kwanini wanafunzi wasianze kidato cha kwanza "directly" na michepuo ya sayansi (Physics, Chemistry) au arts kwa kuzingatia matokeo ya darasa la saba na sio kusubiri mpaka afike kidato cha pili?

Yale masomo saba ya msingi yabaki palepale ambayo ni BIOLOGY, GEOGRAPHY, HISTORY, KISWAHILI, ENGLISH, CIVICS, BASIC MATHEMATICS.

Yaani kwanini mwanafunzi aliyepata ufaulu hafifu katika somo la sayansi katika matokeo ya darasa la saba bado analazimika kusoma tena sayansi hiyo hiyo (Physics na Chemistry) kuanzia form I mpaka form II? Huko sio kuwapotezea muda hawa wanafunzi?

Kama ni kweli tunataka kupiga hatua na kuwa na wanasayansi bora hapo mbeleni, kwanini somo la sayansi kwa shule za msingi lisivunjwe mara tatu kisha yakapatikana masomo matatu ya Baiolojia, Fikizia pamoja na Kemia yatakayofundishwa separately kama ambavyo Kiingereza na Kiswahili vinavyofundishwa?

Hayo ni mawazo yangu tu ndugu zangu na ninakaribisha ukosoaji (Constructive Critisism)

NB: Suala la lugha ya kufundishia kati ya Kiingereza na Kiswahili kwa shule za msingi na secondary sio lengo la mada hii ninaomba tusilizungumzie kwa sasa.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
(Education Curriculum ) me nadhan mtaala wa elimu upo sawa Ila unahitaji marekebisho makubwa yanayoendana na mahitaji
 
Sawa mkuu upo sahihi. Tunaomba mchango wako zaidi kama hutojali ndugu yangu ili na sisi tuzidi kujifunza
Ninachotaka kusema na uelewa wangu juu ya maendeleo na elimu mwanzon nchi nyingi za ulaya walikuwa Wana community centered education curriculum hapa ni kwamba mwanafunzi anasoma apate elimu aisaidie jamii inayomzungunguka later on wakaboresha ili kuruhusu ubunifu katika ujuzi wakahama kwenda kwa learner centered curriculum ambapo tunasema kuwa Kila mtoto anazaliwa na kipawa chake kwa hio kazi ya mwalimu ni kugundua kuwa huyu mtoto interest yake ipo katika nn na kuhakikisha una msubject huko ili kukuza kipaji chake na ndio maana unaona innovation katika kazi zao
 
Hizi shule za technical zinaua talents za watoto maana pale utasoma ufundi kumbe huyo mtu angesoma shule za kawaida angekuwa mwanasheria mzuri au mchumi mzuri ungeandaliwa mfumo mzuri wa kuwapata wale watoto wenye talents za ufundi ndiyo wapelekwe huko siyo kulazimisha watoto kusoma ufundi
Turudi katika maada mtoto anatakiwa asome masomo mbali mbali ambayo yatamsaidia kuwa na atleast basic knowladge ili kupata hao wataalam wanasayansi inabidi pawe na uwekezaji mkubwa katika elimu kuanzia ngazi ya elimu ya msingi mpaka vyuoni pia waencourage zaidi learner centered curriculum ambayo ni very expensive
 
Turudi katika maada mtoto anatakiwa asome masomo mbali mbali ambayo yatamsaidia kuwa na atleast basic knowladge
Sawa mkuu. Pia nimependeza namna ulivyotumia hilo neno "at least basic knowledge" bila shaka ulikuwa una maana kwamba sio kila knowledge inapatikana shuleni bali ni ile ya msingi...
 
Back
Top Bottom