NostradamusEstrademe
JF-Expert Member
- Jul 1, 2017
- 3,402
- 4,532
Blogger sio kweli ila ngoja nikupe tofauti za waliosoma shule za ufundi na shule za kawaida ila mizania yangu itajikita kwenye aliye na FTC au Diploma na mwenye degree.Tuchukulie kwenye somo la ujenzi au CIVILUnaruhusiwa kumuamisha mwanao Mkuu..
Ila hakuna elimu bora duniani kama inayopatikana shule za ufundi.
Waliosoma ufundi FTC au Diploma wako very well kwenye know HOW
Waliosoma shule za kawaida wakasoma hadi degree wako vizuri kweye know WHY
Mtu wa FTC ukampa mchoro umefanya design kila kitu ukampa materials ya kazi atakufanyia kazi nzuri mno mambo ya WHY hayajui wala sio issue zake wala levels zake.
Aliyesoma civil engineering yeye kabla jengo halijanyanyuka atakaa mezani ataweka mambo sawa na kujua kitatumika nini na nini ila kiukweli kiutendaji hayuko vizuri kuliko mtu wa FTC unaweza kuta hata kushika kijiko hajui ila anajua theory ya kushika kijiko.
Ila hili halimfanyi aliyesoma Civil engineering kuwa ni mweupe la hasha.Mambo yote makubwa sana yanaanzishwa na watu waliobobea kwa elimu kubwa kisha wa level za chini wanakabidhiwa kiutendani na kazi inakwenda huo ndo mgawanyiko wa kazi.
Hili limefanya sehemu nyingi FTC waonekane wako vizuri hata migodini kuliko wenye shahada ila kiukweli kabla mgodi kuanza waliofanya setting design na kila kitu hadi kufikia hatua ya kuchimba ni watu wenye elimu zilizotukuka.
Ness anayempiga sindano mgonjwa au kumfunga kidonda mgonjwa kwa ufasaha hakumfanyi Nesi anaonekane kuwa ni bora kuliko daktari.