Kwanini wanafunzi wasianze kidato cha kwanza na michepuo ya sayansi (Physics, Chemistry) au arts kwa kuzingatia matokeo ya Darasa la Saba?

Kwanini wanafunzi wasianze kidato cha kwanza na michepuo ya sayansi (Physics, Chemistry) au arts kwa kuzingatia matokeo ya Darasa la Saba?

Sikubaliani na hoja yako kwa sababu mimi binafsi shule ya msingi sikufanya vizuri masomo ya sayansi hata hisabati ila nilipopelekwa sekondari utoto uliponiisha nikapenda sayansi na hisabati na kufanya vizuri sayansi kuliko art kwenye matokeo ya O level.
Hongera sana mkuu...
 
Sikubaliani na hoja yako kwa sababu mimi binafsi shule ya msingi sikufanya vizuri masomo ya sayansi hata hisabati ila nilipopelekwa sekondari utoto uliponiisha nikapenda sayansi na hisabati na kufanya vizuri sayansi kuliko art kwenye matokeo ya O level. Hivyo nawaza mfumo wa sasa uendelee tu.
Kama mfumo wa sasa uendelee basi uende hivyo hivyo mpaka kidato cha nne kwa wanafunzi wote na sio kuwachuja ikifika form II kwamba huyo atasoma Physics na Chemistry lakini yule hasomi.

Kama tunataka michujo basi ianzie form I kwa kuzingatia matokeo ya darasa la saba...
 
Sikubaliani na hoja yako kwa sababu mimi binafsi shule ya msingi sikufanya vizuri masomo ya sayansi hata hisabati ila nilipopelekwa sekondari utoto uliponiisha nikapenda sayansi na hisabati na kufanya vizuri sayansi kuliko art kwenye matokeo ya O level. Hivyo nawaza mfumo wa sasa uendelee tu. Maana utafiti unaonyesha akili za watoto wa kiume zinaanza kutulia wakiwa kwenye advanced stage baada ya balehe ambayo ni huko O level. Watoto wa kike akili yao iko stable except kwa changamoto ndogondogo kama MP nk zingatia wao wanavunja ungo mapema wakiwa primary school wa kiume wanachelewa
Huu utafiti wako wa wanafunzi wa kike na kiume nina mashaka nao sana mkuu...
 
sekondari akili ya kijana wa kiume ndo inaanza kutulia....mimi wazo nalopendekeza miaka ya shule ya msingi ipunguzwe hadi miaka 6 au iongezwe hadi miaka 8 ya sekondari o level iwe 3 .
Asante kwa ushauri wako mkuu
 
Changamoto ni nyingi. Ufaulu unapimwa na storage capacity na sio thinking capacity.. Ukute mtoto wako ni 2GB na memory iko full tayari. iyo form 4 izo 4GB storage anazitolea wapi ?
 
Mkuu, sasa kwa hali hii wale wadogo zetu wenye thinking capacity nzuri si wanaonewa na mfumo wetu huu wa elimu...
Ni kweli kuna mambo ambayo viongozi wanahitajika wayape kipaumbele cha kwanza maana akili ikiwa vizur kutokana na msingi mzur wa elimu tunauhakika wa kuwa na maendeleo kwani tuna uhakika wa kuwa na wasomi wenye uwezo mkubwa wakufikiri...
 
Ni kweli kuna mambo ambayo viongozi wanahitajika wayape kipaumbele cha kwanza maana akili ikiwa vizur kutokana na msingi mzur wa elimu tunauhakika wa kuwa na maendeleo kwani tuna uhakika wa kuwa na wasomi wenye uwezo mkubwa wakufikiri...
Ninakubaliana sana na hii kauli yako mkuu
 
Changamoto ni nyingi. Ufaulu unapimwa na storage capacity na sio thinking capacity.. Ukute mtoto wako ni 2GB na memory iko full tayari. iyo form 4 izo 4GB storage anazitolea wapi ?
Unapanua harddisk katika ubongo wake mkuu. Hahahaaaaa I am just kiding bro.
 
Labda kwa sasa hivi. Miaka hiyo wale waliosoma sekondari za ufundi masomo kama History, Geography na Biology walikuwa hawasomi/haafanyii mtihani form four.
Wewe utakuwa ni mhenga sana mkuu...
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu watanzania eti;

Kwanini wanafunzi wasianze kidato cha kwanza "directly" na michepuo ya sayansi (Physics, Chemistry) au arts kwa kuzingatia matokeo ya darasa la saba na sio kusubiri mpaka afike kidato cha pili?

Yale masomo saba ya msingi yabaki palepale ambayo ni BIOLOGY, GEOGRAPHY, HISTORY, KISWAHILI, ENGLISH, CIVICS, BASIC MATHEMATICS.

Yaani kwanini mwanafunzi aliyepata ufaulu hafifu katika somo la sayansi katika matokeo ya darasa la saba bado analazimika kusoma tena sayansi hiyo hiyo (Physics na Chemistry) kuanzia form I mpaka form II? Huko sio kuwapotezea muda hawa wanafunzi?

Kama ni kweli tunataka kupiga hatua na kuwa na wanasayansi bora hapo mbeleni, kwanini somo la sayansi kwa shule za msingi lisivunjwe mara tatu kisha yakapatikana masomo matatu ya Baiolojia, Fikizia pamoja na Kemia yatakayofundishwa separately kama ambavyo Kiingereza na Kiswahili vinavyofundishwa?

Hayo ni mawazo yangu tu ndugu zangu na ninakaribisha ukosoaji (Constructive Critisism)

NB: Suala la lugha ya kufundishia kati ya Kiingereza na Kiswahili kwa shule za msingi na secondary sio lengo la mada hii ninaomba tusilizungumzie kwa sasa.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Naipinga hoja hii kwa sababu zifuatazo;

1. Huku mwanzoni unapata msingi tu wa masomo yote. Hivyo kupata msingi mzuri ndiyo kunafanya mtu awe na uelewa mzuri kwenye michepuo yake

2. Masomo hutegemeana, unaposoma somo hili, kuna pahala patakusaidia kwenye somo jingine, hasa huku mwanzoni. Hivyo basi kuwafanya wanafunzi waanze michepuo mapema, ni kuwaondolea misaada ya masomo mengine kwenye michepuo yao.

3. Ili kujua mwanafunzi aende mchepuo gani, kwanza inatakiwa apite kote ndipo atakapojua uwezo wake upo upande gani. Unaweza ukamuweka mwanafunzi kwenye PCM mapema lakini ujuwe huko pengine atakuwa anafuata mkumbo tu, usikute anaweza art zaidi kuliko PCM. Hajijui uwezo wake kamili upo wapi.
 
Back
Top Bottom