Kwanini wanamziki wa Twanga Pepeta wamepukutika?

Baba Diana alifariki kwa ajali ya kugongwa na gari akiwa anaendesha pikipiki kama sikosei. Hilo la vifo hata MSONDO limeathiri sana bend wanamuziki wengi wamefariki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je huyo dada Lilian Internet yupo hai au yuko wapi na anafanya nini siku hizi kama bado yupo hai?
Kama kuna mtu anakipande cha video atuwekee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shahib Mapajero. Hawa jamaa haya majina ulikuwa ukiimba unayakariri kabisa kwenye kufuatisha lyrics zao. Ilikuwa raha sana.
 
Baba Diiiiiiiii, baba Diana. Hawa jamaa walikuwa hatari sana kwenye burudani.
Baba Diana hakufa kwa HIV wala matumizi ya unga ispokuwa ni kwa .ajali ya gari. Hivyo sioni sababu ya yeye kujumuishwa ktk orodha ya mleta uzi maana haiendani na mada anayotaka kuzungumzia.
 
Baba Diana hakufa kwa HIV wala matumizi ya unga ispokuwa ni kwa .ajali ya gari. Hivyo sioni sababu ya yeye kujumuishwa ktk orodha ya mleta uzi maana haiendani na mada anayotaka kuzungumzia.

Yes mkuu. Wadau walishaweka record sawa kwenye replies za mwanzo.
 
Siyo "Kadie Katanga" ni Gabby kwa maana ya Gabriel. Huyu alifariki kwa ajali ya gari maeneo ya Oysterbay karibu na Mbuyu wa matambiko pale karibu na nyumba za mabalozi akiwa ni mwanamuziki wa Chuchu Sound mwanzoni mwa miaka ya 2000.
 


Baba Diana alikanyagwa na gari akiwa anaendesha pikipiki yake.Madawa ya kulevya ni majanga kwa taifa, we angalia Chidi Benz na kijana mwingine wa bongo fleva kalostika ile mbaya (nimemsahau jina)....watu wanabwia unga si kwa ajili ya stress ila wanatafuta kick wakiwa stejini na matokeo yake wanajikuta wanakuwa wateja mpaka unawaonea huruma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…