Kwanini wananchi hawana imani na awamu ya 6, kila kitu wanahisi wanapigwa?

Kwanini wananchi hawana imani na awamu ya 6, kila kitu wanahisi wanapigwa?

Binafsi mimi bado namshukuru Mungu kuingilia kati na kutuondolea ibilisi Magufuli.

Nitakuwa namkufuru Mungu nikianza ulalamishi sasa hivi, dhamira ya mama inaonekana kwa macho wala huitaji propaganda kujuwa ana utu.
Hao wanaolia lia,sio watanzania,na wengi ni wavivu wakufanyakazi.
 
Kila nikijaribu kupitia maoni ya wananchi katika mitandao ya kijamii ni dhahiri wananchi wengi wanaonekana kukosa imani na serikali ya awamu ya sita. Ukiwasoma kwenye mitandao utaona wamekaa kimashaka-mashaka tu hivi. Kila serikali ikisema hivi kuhusu matumizi ya fedha na miradi basi wao wanahisi kuibiwa ibiwa tu.

Hali hii pia ipo katika maisha ya kawaida. Wameweka imani ndogo sana na uongozi wa mama.

Hali hii inachochewa sana na serikali kupinga katiba mpya. Wananchi wanajiuliza kwa nini hawataki katiba mpya,au wanataka wakiiba wasiulizwe?

Eti jamani kwa nini raia wamekataa mkao wa kuibiwa tu?
Binafsi naamini watu walitegemea nyayo mpya ila kivuli cha Msoga kinamuharibia na kitamuharibia mno.

Kivuli ni dhahiri ukiuliza yeyote anayempenda au asiyempenda anaona kivuli ambacho watu wasingependa kurudi huko.
 
Picha linaanza..wale waliotumbuliwa kipindi cha magu kwa kuonekana hawafai na hawana weredi..wote wamerudishwa mzigoni..pia yule mtoto wa kubwa ambaye alisifika sana kwa dili na kuuza nchi yupo mzigoni.

Serikali kutwa kutembeza bakuli..wakuambiwa wasitembeze bakuli wanakuNdugai.

Kingine porojo nyingi sana..kila kukicha hasa upande wa wizara ya mwezi wa kwanza.

Hali ya maisha haishikiki hali si swali..ila serikali inakuja na propaganda na vichaka vya kujificha ambavyo ni kovidi na vita vya urusi.

#MaendeleoHayanaChama
Acheni kulia lia,Fanyeni kazi.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Ni wakati muuafaka sasa ile silaha ya msaada ya kumtegemea Mungu inayo tumia MAOMBI NA KUFUNGA ikatumiwa kusadia msukumo wa kutafuta Katiba mpya. Wako wapi wacha MUNGU Tanzania wakasimama kwa maslahi ya Taifa lao.
 
Wengi bado hawajazinduka kwenye ndoto za alinacha za mwendazake.
Au ni hangover ya mwendazake.
 
Hao wanaolia lia,sio watanzania,na wengi ni wavivu wakufanyakazi.
Kwahali aliyotufikisha Magufuli kuujaza hofu umma, mtu anakufa na Corona wataalam wanalazimika kusema ni changamoto za upumuwaji, sasa Mungu ametenda na kuliponya Taifa leo tuanze kumlaumu huyu mama wakati ndio anarekebisha uharibifu uliofanywa na yule mwehu tutakuwa watu wa ajabu sana.

Au tuambiwe tatizo ni jinsia yake, dini yake au Uzanzibar wake? watu wawe wawazi wasifiche rangi zao halisi.
 
Mimi sio "age go sana", ila nina makaka na dada wanampita mbali na wengine wanalingana na huyo SHH.

Hivi wewe huoni kuna shida sehemu mtu kama Mbowe au Lissu kumuita SSH mama??

Nimekataa huo mkumbo, kwakua anapendwa kuitwa mama badala ya Rais basi mimi nitamwita dada.
Basi achana na mitandao, LEA WAJUKUU kama umebahatika kupata.
 
Kwahali aliyotufikisha Magufuli kuujaza hofu umma, mtu anakufa na Corona wataalam wanalazimika kusema ni changamoto za upumuwaji, sasa Mungu ametenda na kuliponya Taifa leo tuanze kumlaumu huyu mama wakati ndio anarekebisha uharibifu uliofanywa na yule mwehu tutakuwa watu wa ajabu sana.

Au tuambiwe tatizo ni jinsia yake, dini yake au Uzanzibar wake? watu wawe wawazi wasifiche rangi zao halisi.
Umemaliza mjadala,kama wanajifanya hawakuelewi,waache wameshakuelewa.
 
Kwasababu awamu hii ya 6 inafanana kwa kila kitu na awamu ya 4

Kilichonishanganza zaidi ni mpaka kafara zilizotumika za kushikiria uongozi zinafanana,sahiv kila siku magari yanachinja
 
Achana na propaganda ndugu. Magufuli hakuwa SI unit ya nchi kuhusu nani anafaa au hafai. Walioshika nafasi hizo ni watanzania na wana haki hiyo. Mengineyo ni porojo tu.
Kupanda kwa hali ya maisha ni porojo?wewe jamaa upo Tanganyika ama?


#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom