Kwanini wananchi hawana imani na awamu ya 6, kila kitu wanahisi wanapigwa?

Kwa mambo yanayoendelea hapa nchini kwa sasa, Ni wazi kwamba wananchi hawana tena imani chini ya uongozi wa awamu hii ya sita. Kila unapoenda ni lawama na hali ya kutoridhika na utendaji wa serikali.Mambo haya yamekuwa yakilalamikiwa sana.

1: Uchumi wa Tanzania Umeporomoka.Laiti kama uongozi ungekuwa thabiti hakika uchumi ungekuwa wa kati daraja la juu tofauti na hali ilivyo sasa ambapo Tanzania imeporomoka kutoka nafasi yake ya 8 kati ya nchi 10 zenye uchumi bora Africa mpaka nje ya top 10 na kuzidiwa na vinchi kama Ghana na Angola

2: Laiti kama uongozi ungekuwa imara nidhamu na uwajibikaji kazini ungekuwepo.Leo hii tunashuhudia wananchi wakihoji kuhusu hali ya umeme nchini pasipokuwa na majibu au majibu yenye uwalakini. Lakini pamoja na hayo bado viongozi wamebaki wakiwa maofisini pasipo kuwajibika kwa namna yoyote.

3: Kwa miaka kadhaa Tanzania imekuwa ikiifanya juhudi kubwa kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha miradi mikubwa na ya kimkakati. Licha ya kwamba tangu awamu ya sita iingie madarakani hakuna mradi wowote wa kimkakati ulioanzishwa bali pia hata ile miradi iliyokuwa ikiendelea imekuwa ikisuasua

4: Serikali ingekuwa makini hakika Umeme usingekuwa wa mgao.Tangu Rais S.S.H aingie madarakani hali ya upatikanaji wa umeme nchini imekuwa mbaya sana.Hali hii imepelekea kurejea kwa mgao wa umeme ambao watanzania wengi walishausahau tangu miaka kadhaa iliyopita.Hali inayopelekea kuwatesa wananchi hususan wale wanaotegemea umeme kujipatia vipato katika shughuli zao za kila siku.

5; Hali ya upatikanaji wa maji imekuwa ya kusuasua.Kwa miezi kadhaa hususan katika jiji la Dar es salaam pamekuwa na mgao wa maji.Hali iliyopelekea kukosekana kwa maji kwa muda mrefu katika maeneo mengi.Hali ambayo hakuwahi kushuhudiwa hapo awali.

6: Tozo zisizokuwa na tija na zilizoua uchumi wa wengi.Serikali ya awamu ya sita imedhulumu na kunyang'anya kwa nguvu fedha za wananchi kwa kigezo cha tozo katika miamala ya simu.Mama mjane anapomtumia mgonjwa wake hospitali kwa ajili ya matibabu anakatwa fedha ambayo kimsingi haikuwa ya biashara. Kwa mujibu wa report kutoka Vodacom hivi karibuni miamala ya simu imepungua kwa asilimia zaidi ya 30!.Hili si jambo la kupuuza hata kidogo kwa uchumi wa nchi.Ni sawa na kutoa fedha mfuko wa kushoto na kuhamishia Kulia.

7: Kupanda kwa bei ya Mbolea.Mara tu baada ya awamu ya sita kuingia madarakani bei ya mbolea ilipanda karibu mara mbili ya bei ya awali.Hii ni imepelekea uchumi wa watanzania wengi ambao ni masikini na wanategemea kilimo kudhoofika.

8; Kupanda kwa bei ya mafuta ya kupikia
9; Kupanda kwa bei ya mafuta ya petrol
10; Kupanda kwa bei ya bidhaa za ujenzi kama cement,Nondo n.k
11; Teuzi za viongozi wasiokuwa na weledi kwa kigezo cha favour/Undugu/Kujuana (Mf. Riziwani Kikwete,Nape Nauye n.k) Tanzania ina vijana wasomi na wenye upeo mpana wa kifikra. Lakini cha kushangaza teuzi zimekuwa hazina matumaini ta kuipeleka Tanzania kule tunapotarajia.

12: Ukosefu wa uzalendo na ubadhirifu miongoni mwa watumishi wa umma.Siku si nyingi tumeshuhudia kiongozi mkuu wa serikali akiwaasa watumishi wake wale kwa urefu wa kamba zao.Hii inaashiria kwamba hata kiongozi mkuu anashiriki katika ulaji huo.Hali hii ni hatari kwa rasilimali za nchi.

13; Wananchi hususan wa hali ya chini kukosa nafasi katika nchi yao.Siku si nyingi tumeshuhudia wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga wakinyanyaswa kwa kuhamishiwa katika maeneo yasiyokuwa tija kwao.Vuta nikuvute hii imepelekea hali ya unyonge na sintofahamu miongoni mwao na kupelekea kuongezeka kwa umasikini miongoni mwa watanzania

14; Mikopo isiyokuwa na tija kwa taifa.Tangu Tanzania ipate uhuru viongozi wake wote walisisitiza kufanya mambo yetu kwa fedha zetu wenyewe bila kutegemea wahisani. Tanzania imebarikiwa rasilimali za kila aina.Mito,Maziwa,Bahari,Madini kama Tanzanite,Mbuga za wanyama,Gesi n.k Inashangaza Sana kuona kiongozi badala ya kusisitiza au kubuni namna ya kuzitumia rasilimali hizi ziweze kuwa na tija kwa watanzania,Badala yake tumekuwa tukijivunia mikopo!

15 ; Kuongezeka kwa gharama za uunganishaji umeme kutoka 27,000 iliyokuwepo mpaka zaidi ya 300,000 ya hivi sasa.Hali hii imepunguza mno kasi ya usambaaji wa umeme

16 ; Muingiliano baina ya mihimili kwa kigezo cha uchama.Inasikitisha kuona kiongozi wa mhimili mmoja anakosa uwezo wa kuikosoa na kuurekebisha mhimili mwingine kwa kuhofia kibarua chake.hili tumelishuhudia baada ya kuona spika wa bunge la JMT kujiuzulu baada ya kuhoji kuhusu mikopo na tozo.

17 ; Safari zisizokuwa na tija wala umuhimu kwa taifa.Tumeshuhudia safari nyingi mno za nje ya nchi,Safari hizi zimekuwa zikiigharimu nchi fedha nyingi.Safari za vikao visivyokuwa na tija kama mkutano wa kujadili athari za gesi ya ukaa sidhani kama ina tija hususan kwa nchi ambazo bado uchumi wake ni mdogo

18 ; Kukosekana uhuru na ukandamizaji wa demokrasia. Tunaweza kusema kwamba pia hata katika awamu zilizopita hili lilikuwepo, Lakini hili la sasa limekuja kwa namna tofauti.Wakati mwingine baba anaweza kumpa mtoto adhabu ya kulima shamba,Mtoto akalia na kulaumu sana,Lakini shamba hilohilo baadaye likaleta chakula mezani wote wakala na kufurahia. Ila tofauti iliyopo sasa,Hakuna chakula kinachokuja mezani!

19 ; Kushughulikia zaidi mambo yasiyokuwa na tija kwa wananchi kuliko yale yenye umuhimu na tija kwa watanzania. Imekuwa jambo la kawaida kwa awamu hii kujihusisha zaidi na makongamano,Semina elekezi,Birthday Party pamoja na hafla mbali mbali badala ya kujikita katika kufufua na kubuni miradi ya kimaendeleo itakayosaidia kuwapunguzia wananchi mzigo wa umasikini na kuinua uchumi.Hafla ya machifu na watemi si muhimu kama hafla ya utiaji saini mradi wa uchimbaji na usambazaji wa gesi ya Mtwara!

20 ; Kukosekana ajira. Ubunifu na uibuaji wa miradi mipya si tu umekuwa na tija kiuchumi Bali umekuwa ukiajiri vijana wengi.Kukosekana kwa ubunifu na sera mbovu za serikali zimesababisha kukoseka kwa ajira miongoni mwa vijana wengi

21 ; Kuongezeka matukio ya uhalifu.
Mara tu baada ya awamu ya sita kushika hatamu sote tumeshuhudia jinsi wimbi la uhalifu lilivyoongezeka.Sio tu matukio ya wizi na ujambazi bali mpaka uchomaji wa masoko kama Kariakoo, mchikichini n.k wizi mauaji na utekaji nyara vimeongezeka kwa kasi mno. Hii inaonyesha udhaifu katika usimamizi wa majeshi yetu ya ulinzi na usalama

22 ; Kuongezeka gharama za simu
Kutokana na kodi za miamala Kuongezeka kampuni za simu zimejikuta zikilazimika kupandisha gharama za muda wa maongezi na huduma zinginezo za simu kama vile huduma za vifurushi ili kuweza kubalance gharama za uendeshaji. Hali hii imesababisha mzigo mzito kwa wananchi hasa ukizingatia mawasiliano ni nyenzo muhimu sana katika shughuli zao za kila siku

Hakika ni mambo mengi ambayo yamekuwa yakifanyika kinyume na matarajio ya watanzania wengi ambao waliwaamini viongozi wao na kuwaweka madarakani huku wakiwa na matumaini makubwa ya kuondokewa na maradhi, ujinga na umasikini ambao ndio maadui wakuu wa taifa kama ilivyobainishwa na Mwl Nyerere badala yake watanzania hao ambao wengi ni masikini na wameteseka kwa umasikini kiasi cha kusahau tarehe zao za kuzaliwa huku wakishuhudia wale waliowachagua wakikata keki ikulu!

Wacha kazi iendelee!
Umenena vyema lakini ingekuwa vyema zaidi kama huu ujumbe ungefunguliwa uzi wake binafsi maana umejitosheleza sana.
 
Huyo mnemuita mama mwenyewe bado anahangaika na mitandao, labda kama umezoea kukutana na wazee wasiokuwa na kipato.
Kama Hakuna kipato chochote unachopata kupitia mitandaoni, usiipe sana mitandao umuhimu maishani mwako.
 
ivi wakuu sekeseke la katiba mpya la sasa lilianza lini
 
Acha kulia lia,ondoa uvivu.Fanyakazi.Mtu mvivu ndio analia lia.
 
serikali ya jumong inanuka harufu mbaya ya rushwa kubwakubwa
 
Kwenye siasa kuna Cartel, hata wewe tukikupa madaraka leo huwezi kuwatosa wana.

Magufuli alifanya hivyohivyo pia kuwajaza kanda ya ziwa

Dr Slaa akiwa katibu mkuu wa Chadema kazi za kutangazwa tenda za kutengeneza software alikuwa akimpa demu wake Josephine Mushumbushi, hadi ID ya Dr slaa hapa JF akawa anaitumia Josephine na watu wakamdharau kabisa Dr.
Umemalizia vizuri kabisaa, kwamba "...watu wakamdharau.. "
Kwahiyo, unakubaliana kwamba, kwa kiongozi kuteua watendaji wasiokubalika na wengi, au viongozi wasio waadilifu, inasababisha huyo aliyewateua kushindwa kuaminiwa na wananchi.

Na kwa wengi leo hii ni kama bado hawaelewi kusudi hasa la kuwapa nafasi viongozi walewale walioonekana hawafai kwa wakati uliopita! Tena nafasi nyeti
 
Kama Hakuna kipato chochote unachopata kupitia mitandaoni, usiipe sana mitandao umuhimu maishani mwako.
Wewe kuna kipatao unachopata kwa kudhurura kwenye kila nyuzi za jf kuanza asubuhi hadi usiku???
 
Kila nikijaribu kupitia maoni ya wananchi katika mitandao ya kijamii ni dhahiri wananchi wengi wanaonekana kukosa imani na serikali ya awamu ya sita. Ukiwasoma kwenye mitandao utaona wamekaa kimashaka-mashaka tu hivi. Kila serikali ikisema hivi kuhusu matumizi ya fedha na miradi basi wao wanahisi kuibiwa ibiwa tu.

Hali hii pia ipo katika maisha ya kawaida. Wameweka imani ndogo sana na uongozi wa mama.

Hali hii inachochewa sana na serikali kupinga katiba mpya. Wananchi wanajiuliza kwa nini hawataki katiba mpya, au wanataka wakiiba wasiulizwe?

Eti jamani kwa nini raia wamekataa mkao wa kuibiwa tu?
Usitusemee
 
Ni udini na ubaguzi unaowasumbua watu wengi. Nchi hii ina matatizo tangu ipate uhuru lakini Muislamu au Mzanzibari akiingia ikulu watu wanapagawa. Ndiyo historia ya nchi hii. Hao hao wananchi waliokuwa wanakufa njaa wakati wa Nyerere, walimpigia kelele Mwinyi aliposaidia kuinua uchumi.
 
Kila nikijaribu kupitia maoni ya wananchi katika mitandao ya kijamii ni dhahiri wananchi wengi wanaonekana kukosa imani na serikali ya awamu ya sita. Ukiwasoma kwenye mitandao utaona wamekaa kimashaka-mashaka tu hivi. Kila serikali ikisema hivi kuhusu matumizi ya fedha na miradi basi wao wanahisi kuibiwa ibiwa tu.

Hali hii pia ipo katika maisha ya kawaida. Wameweka imani ndogo sana na uongozi wa mama.

Hali hii inachochewa sana na serikali kupinga katiba mpya. Wananchi wanajiuliza kwa nini hawataki katiba mpya, au wanataka wakiiba wasiulizwe?

Eti jamani kwa nini raia wamekataa mkao wa kuibiwa tu?
Wala sio katiba mpya ila ni vijembe na vitendo vya awamu ya mama ndio vinatia shaka sio mtetezi wa umma kama magufuli. Kashasema vigogo wale kwa urefu wa kamba zao. Hapo ndio kawadhihirishia wananchi yeye ni kiongozi sampuli gani.
 
Wananchi wengi wanaona nchi inarudi kwenye enzi za fisadi Kikwete ambapo upigaji, ufisadi, wizi, uzembe, nk vilikuwa ndiyo mwendo wa kila siku.
 
Zimetengwa Trilioni 4 za maintenance Tanesco.

Na anayezisimamia ni mtu anayeimendea Ikulu.

Hizi pesa zitakuwa diverted kwenye safari ya Ikulu ya mtu.
 
Serikali hii ata mtoto mdogo atakumbia kuwa ni majizi yamejikusanya pamoja kutulindia mali zetu.
 
Kila nikijaribu kupitia maoni ya wananchi katika mitandao ya kijamii ni dhahiri wananchi wengi wanaonekana kukosa imani na serikali ya awamu ya sita. Ukiwasoma kwenye mitandao utaona wamekaa kimashaka-mashaka tu hivi. Kila serikali ikisema hivi kuhusu matumizi ya fedha na miradi basi wao wanahisi kuibiwa ibiwa tu.

Hali hii pia ipo katika maisha ya kawaida. Wameweka imani ndogo sana na uongozi wa mama.

Hali hii inachochewa sana na serikali kupinga katiba mpya. Wananchi wanajiuliza kwa nini hawataki katiba mpya, au wanataka wakiiba wasiulizwe?

Eti jamani kwa nini raia wamekataa mkao wa kuibiwa tu?
Mshauri wako Mkuu akiwa na Historia ya kuwa Fisadi, Mla Rushwa Mwandamizi, Mzururaji, Mswahili Mswahili, Mnafiki, Mshirikina wa Kutupwa na mpenda Anasa na Ujana uliomtupa mkono unategemea na Wewe Mkuu kuwa tofauti nae?
 
Mbona Magufuli alipokuwa hai wote mliufyata?

Msimchukulie powa kihivyo, katiba mpya ni muhimu ila si uungwana mtu amechukuwa nchi iliyoharibiwa na kichaa ukampachika Agenda zote kwa wakati mmoja, wananchi sasa tunapumuwa.
Mku. #ndu kwel wee jamaa... Kama ulivyomwita kipenz changu kichaa namim sina budi kukuita nitakavyo.. mk..** ndu kabisa wewe
 
Wanasiasa kuweni WAWAZI.

Wekeni WAZI mnachotaka Ni KITI CHA URAIS.

Samia akiwaachia hicho hata hiyo Katiba Mpya mnayopigia kelele hamtaitaka tena.

Na hata kama ikipatikana hiyo Katiba Mpya na mwisho wa siku ISIWE SULUHISHO la Nyie kupata Madaraka bado MTAPIGA KELELE Mnooooo kuwa hamtendewi HAKI.

Na ndio maana nyi SIKU ZOTE hamjawahi KUSHIDWA UCHAGUZI.

CHAGUZI zote huwa MNAIBIWA yaani.
Maon yako ni nin haswa... Kwan katiba mpya kuwepo kuna tatzo gan...?
 
Ni wajinga lakini pia ni athari za dikteta uchwara kudhibiti taarifa na kuwaaminiaha ujinga.

Hii ndiyo Hali pia iliyojitokeza kipindi cha Nyerere na kuwaathiri viongozi waliofuatia.

Mwisho,ukichukua leo utendaji wa Samia mwaka 1 vs Mwendazake mwaka 1 ,Samia kampita mbali Mwendazake.
Ndugu yangu, wewe kula tu kwa urefu wa kamba yako na si kuanza kuandika upumbavu hapa!
 
  • Thanks
Reactions: nao
Kwahali aliyotufikisha Magufuli kuujaza hofu umma, mtu anakufa na Corona wataalam wanalazimika kusema ni changamoto za upumuwaji, sasa Mungu ametenda na kuliponya Taifa leo tuanze kumlaumu huyu mama wakati ndio anarekebisha uharibifu uliofanywa na yule mwehu tutakuwa watu wa ajabu sana.

Au tuambiwe tatizo ni jinsia yake, dini yake au Uzanzibar wake? watu wawe wawazi wasifiche rangi zao halisi.
Ni mpumbavu pekee na mjinga tuu mwenye kukuunga mkono ktk ujinga huu uliotukukuka

Kula kwa kamba yako na utokomee na si kuandika upumbavu kama huu
 
Back
Top Bottom