Kwanini wananchi hawana imani na awamu ya 6, kila kitu wanahisi wanapigwa?

Ulichokiandika ndo kinaakisi ujinga wako

Kula kulingana na urefu wa kamba yako kima wewe!

Nakuona ulivyotengewa chakula haramu mezani na unakitetea!!

Fangasi Mkubwa wewe
Kwani wewe hutaki kula? Nakuona ulivyopauka kwa kupigwa na jua so una hasira Sana 😁😁
 
Tatizo ni kwamba hawa hawa waliotuambia tunajenga miradi kwa pesa yetu wenyewe ndio hao hao wanaotuambia tunakopa ili kuendeleza miradi ya mkakati, waliotuambia kuwa kupga nyungu ni kinga ya korona ndio hao hao wanaotuambia chanjo ni bora kuliko nyungu, waliotuambia kuwa rais kutosafiri nje ni kubana matumizi ndio hao hao wanaotuambia rais asiposafiri hatutapata pesa. Hao hao waliotuaminisha kuwa wazungu ni mabeberu ndio hao hao wanatuambia kuwa rais anajenga mahusiano na nchi za nje
 
Kwani tuliokua tukimponda JPM kuharibu uchumi hivi sasa bado tunakula msoto tu. Mkanye mjinga akuchukie
 
 
Timu aliyoichagua yeye mwenyewe kwa hiari na mapenzi yake ndio inatoa taswira kwamba jinsi walivyo ndivyo alivyobariki ifanyike. Most of the team members have questionable integrity
 
Heri ya mtu anaekukaripia na mkali ilihali unajua anasimamia misingi gani kuliko mtu mpole mtulivu na mwenye maneno laini ila hujui Ana misimamo gani! Wengi wetu tulitarajia ajira zitatoka na kipato Cha watu kuongezeka. Tulitarajia mabadiliko kiutawala (katiba mpya ili tusirudi kuwa na viongozi km bashite) na tulitarajia mifumo Kama ya Elimu kuboreka Mana rais Samia aliingia na mbwembwe hizo Ila mpaka Sasa Mambo Ni sufuri. Mbali na hapo akatupiga na kitu kizito kichwani(tozo), akaleta udini kwa kutoa mashekhe kesi za ugaidi ila kampachika Mbowe kesi hiyo wakati kila mwenye akili timamu anajua Ni kesi ya mchongo. Alaf rais Ana siasa za kitoto Sana (kudanganya mtoto ntakuletea pipi usinifate alaf haleti). Teuzi za kifala Kama Mwigulu na Ridhiwani. Inshort Mambo Ni ovyo sana isipokuwa siasa za kitoto Kama kudhani Sasa hivi Kuna Uhuru wa maoni na democracy nchini wakati hakuna (ameruhusu watu waongee tu, ila ukikwaza utaona Mambo Kama mchungaji wa kanisa la Efatha na kuita watu was mitandao sio watanzania) niendelee
 
Mimi nathamini upeo na uwezo wa SSH,Mungu amepe nguvu na upeo Amen
 
Binafsi mimi bado namshukuru Mungu kuingilia kati.

Nitakuwa namkufuru Mungu nikianza ulalamishi sasa hivi, dhamira ya mama inaonekana kwa macho wala huitaji propaganda kujuwa ana utu.
Wapigaji wanawapenda sana watu wapole na wenye Utu, ndio tatizo la nchi hii, kiongozi akiwa mpole watu wanapiga madili si mchezo! Matokeo yake vitu vitapanda sana bei ! Na watakaoumia sana ni watu wa kipato cha chini, hilo ndilo tatizo la watu wa nchi hii upigaji ni mwingi sana !!
 
Haina meno na wapigaji, pili majizi yote yamerejeshwa kutafuna
 
Jambo gan la maana kafanya au hiyo tour marekani ndio jambo kubwa
 
Awamu ya Sita alichaguliwa lini?. Yeye ni kiongozi wa mpito kuelekea 2025 kwenye awamu ya Sita wala asijinasibu kwa lolote maana nchi imeshamshinda huyu bibi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…