Nangu Nyau
JF-Expert Member
- Jul 1, 2022
- 5,015
- 14,139
Eti mtoa mada kwa fikra hizi za viongozi, wapambe wao na wananchi kwa ujumla unafikiri ubongo wa mwafrika na hususani Mtanzania umekomaa vya kutosha kuleta maendeleo ya kweli?.
Maana nchi hii hata serikali ikijenga vyoo kwa fedha za misaada Rais anapongezwa kwa mabango na umati wa watu utafikiri amefanya jambo la kipekee.
hahahaha umenichekesha sana hapo kwenye ubongo wa Mwafrica hususani Mtanzania kuwa na ukomavu wa kutosha kuleta maendeleo.
Huwa nikiangalia viongozi wa mataifa makubwa yaliyoendelea hususani huko nyuma walipokuwa kwenye mapambano ya kiuchumi halafu nije nifananishe na hizi akili zetu huwa naumia sana.
Hivi kweli USA, Russia, Japan, Uingereza, Germany nk, huko nyuma wangekuwa na viongozi kama hawa sijui ingewachukua miaka mingapi kufika hapo walipo leo.