Kwanini wanashauri usivute gari lenye Automatic Gearbox ukipata break down, badala yake upakie kwenye Flatbed Truck

Hii ina maana haitakiwi kulisukuma gari (automatic gearbox) hata kama umeharibikiwa katikati ya barabara ?
 
Mimi nikadhani clutch inatenganisha Engine na Gear BOX ,kwamba engine inaweza kuwa inazunguka usipo engage clutch Drive shaft (iliyoungwa kwenye mfumo wa gear) kwenda kwenye differential (tairi za nyuma) inakuwa free kuzunguka tu,naomba unisahihishe mkuu.

Asante.
 
Gearbox automatic haipo kama gearbox ya manual, anzia kubadili mtazamo wako hapa.

Automatic gearbox inakuwa na clutch pack kadhaa, na kila pack inakuwa na viclutch vyembamba sana, na eneo ambalo hivyo viclutch vinazunguka ni eneo dogo sana.

Na ama engine iwe on au gari ikiwa inavutwa engine iko off lazima kuna clutch pack moja au zaidi iwe inazunguka.

Ndio maana tunashauri usivute sababu engine ikiwa off oil pump nayo haizunguko hivyo oil haipandi, clutch zitazunguka bila oil kitu ambacho kinaweza kuziharibu, hapo sijagusia bearings nk.
 
Shukran
 
Ni ngumu kuelewa joto linazalishwaje kwa elimu ya mtaani.

Converter tu ndio inatunza oil hizo sehemu zingine zilizobaki hazina mahali pa kutunza oil. Ndio maana gari ikipaki masaa mengi oil nyingi inashuka chini.
Yani hata shepu yagiabox ulio idanlod na kutuwekea hapa huioni?
unapo jaza oil sampo Ina jaaa oil Hadi kipita valvu ches Sasa hebu gugo Tena uone umbali wa valvu ches na clutch ni kias Gani kama sio púa na mdomo.
 
wee jamaa muongo sana.hivi ushawahi kufanya sevis ukaona jinsi oil inavyo Toka?au ushawahi kufungua sampo ukaona oil inavyo Toka?au ushawahi kufungua valvu ches ukaona oil inavyo Toka?
kama ushawahi kufanya vyote nilivyo kuuliza hapa basi Acha kuropoka lakini kama hujawahi basi nihaki Yako kuropoka
 
wee
Haya maelezo ni kwa gearbox ambazo hazina dipstick, tushazoea kwenye gari za mjerumani. Ila gari yenye dipstick weka oil kiasi kinachotakiwa washa gari katembee ikipata moto njoo upime tena.
wee nishajua nibwege kumbe.yani uweke oil ukatembee ndio uludi kupima Tena kama ipo levo au haipo levo?

automatic ukiweka oil yagia box unaiwasha hapo ikae sailensa ukipima ndio unapata kipimo sahihi.sio Hadi uende kutembea ndio urudi kupima.
kajifunze Tena ufundi mkuu bado hujaiva.
 
dah naona nitatumia muda mwingi kumpigia mbuzi gitaa.✋
 
Yani hata shepu yagiabox ulio idanlod na kutuwekea hapa huioni?
unapo jaza oil sampo Ina jaaa oil Hadi kipita valvu ches Sasa hebu gugo Tena uone umbali wa valvu ches na clutch ni kias Gani kama sio púa na mdomo.
Ukijaza oil haipiti valve body, na kudhihirisha hilo gari zisizokuwa na dipstick unajaza oil mpaka tundu la sample lianze kudondosha matone ndio inakuwa imejaa,

Utafunga koki utaenda kupiga misele ikishapata joto utarudi utafungua tena koki itamwagika tena kidogo, baada ya hapo itakuwa ipo kwenye level yake.

Clutch na sump haviko pua na mdomo pia kigodoro cha oil filter kinazuia oil kuja free sehemu ya juu ya gearbox.
 
Siyo kufungua tu hivyo ulivyotaja hapo, naweza kufanya vitu vingi kwenye hizo gearbox mpaka kufanya rebuild,

Screenshot nimepost asubuhi ni manual ambazo wanazo Automatic Transmission Service Group hawa jamaa wamebobea kwenye hizo gearbox tu. Na ndio wanaotoa hizo manual.

We ukifungua gearbox unaangalia clutch kama zimeisha kwa macho ila wenzako wana gauges, clearance ya 0.5mm huwezi kuona kwa macho.
 
toka hapa.automatic giabox zikiunguza clatch zinatengenezeka au hazitengenezeki?
 
daa wee jamaa kwamaelezo haya nimegundua kuwa kumbe uko mweupe kabisa kwenye fani ya ufundi magari.

nyie ndio vijana makinda mnao ya giabox zawatu.

narudia mara yamwisho kukuelekeza kijana nihivii👉

ukitaka kuweka oil ya giabox kwenye auto cars unaweka oil kama inaingia Litasita unaweka nne then unaiwasha gari ikae sailensa unamaliza oil iliyo bakia
hapo ukipima oil dipstick itakuonesha kuwa oil ipo levo wee bwana mdogo sAwa?

Hamna haja yakwenda kupiga misele ndio urudi kupima🤣🤣🤣

unanichekesha kifala yani.

halafu unasema kitako Cha oil filter kinaziba valvu ches body yote kiasi chakuzuia oil isipenye juu kwenye valvu ches?uko Silias mjomba?
 
wee nishajua nibwege kumbe.yani uweke oil ukatembee ndio uludi kupima Tena kama ipo levo au haipo levo?
Kwa hiyo mtu akiwa anafahamu kitu ambacho wewe hufahamu anageuka kuwa bwege?
automatic ukiweka oil yagia box unaiwasha hapo ikae sailensa ukipima ndio unapata kipimo sahihi.sio Hadi uende kutembea ndio urudi kupima.
kajifunze Tena ufundi mkuu bado hujaiva.
Nisije nikawa nabishana na mtu anarekebisha gari za miaka ya 80, siku, sheria ya kuweka oil ya auto gearbox siku zote ni weka oil kiasi kinachotakiwa washa gari nenda kazurule likishapata moto, rudi angalia kwenye dipstick kama Oil iko level, kama imezidi punguza kama iko chini ongeza,

Kwa gari ambazo hazina dipstick, na ndio na ndio gari za sasa, unaweka oil kiasi kinachotakiwa unawasha gari unaenda kuzurula, likipata moto unafungua drain valve, oil itakayomwagika ndio iliyozidi.

Na kuna gearbox hazina drain valve, lazima uwe na pump kudrain au kuweka Oil, na level ya Oil utacheck ndani kwenye gari au kwa mashine.

Kitu cha mwisho oil level ya gearbox inapimwa baada ya gari kuwa imetembea na ni ya moto, na siyo baada ya kuwasha. Kuna sababu juu ya hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…