Kwanini wanataka kuzuia Rais Samia Suluhu asiende kinyume na Hayati Magufuli?

Kwanini wanataka kuzuia Rais Samia Suluhu asiende kinyume na Hayati Magufuli?

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Posts
40,455
Reaction score
73,145
Ni ukweli usiofichika kuwa kuna mkakati wa ndani ya Bunge na baadhi ya Mawaziri wakiongozwa na PM mwenyewe kum pre empty Rais Mama Samia ili ajikute anafanya kazi bila kwenda kinyume na mtangulizi wake JPM.

Mkakati huo unaoendeshwa kimahesabu sina hakika kama Rais ameshaushtukia au kwa vile timu ya wasaidizi wake ni ileile anaweza kuwa anafunikwa na blanketi na halioni hilo?

Je, ni kwa nini mbinu hizo chafu zinafanywa? Je, mama haoni kuwa kuendelea na wasaidizi wasio kubaliana kifikra kuwa yeye ni Rais kwa sasa itakwamisha mipango yake?
 
Kwa maoni yangu ni kuwa Mama samia Amerithi serikali ambayo yeye alikuwa sehemu yake na ilikuwa na malengo kulingana na ilani ya uchaguzi iliyowaweka madarakani pale, kwa hiyo swala ni ukamilishaji wa ilani ile.

Ni maoni yangu tu, siyo kuwa kwa vile karithi serikali na yeye ndiyo bosi basi ilani yao haina maana tena ila yeye ataleta ya kwa kwake tofauti; sidhani kama kweli mambo yanatakiwa yawe hivyo. Wenzetu husema elections have consequences, ambazo yeye atatakiwa azisimamie siyo kuwa azifute.
 
Nanaamini kila mmoja anahitaji kufanya kitakachomjenga kiutendaji na kihistoria.

Kwa uelewa au matendo asilazimishwe mtu kuyaridhi kwani sio kila cha kuridhi ni hekima kama sio hivyo hakuna haja ya kuufuata mfumo wa mwenye mamuzi yake.
 
Hoja yako itakuwa vilid ikiwa tu JPM angelikuwa akitekeleza miradi ambayo ilikuwa kwenye ilani iliyokuwa imemuweka madarakani.
 
Back
Top Bottom