Kwanini wanataka kuzuia Rais Samia Suluhu asiende kinyume na Hayati Magufuli?

Aisee tulieni kidogo, mama anailani mkononi ambayo anatakiwa kuitekeleza kama walivyo ahidi yeye na Magu kwenye uchaguzi ulioisha. Asipo tekeleza walicho ahidi atakuwa ma maswali ya kujibu 2025.

Kwasasa sio rahisi kwenda kinyume na mipango ya jpm ambayo waliahidi pamoja kwenye kampeni.
Hivi matendo maovu yaliyo jitokeza baada ya 2015 ndizo ahadi walizoweka kwa pamoja Magu na mama?
Sidhani kama ni kweli, hayo hayakuwepo kwenye ilani bali yalikuwa yake mwenyewe JPM na mama kesha onyesha hayataki lakini wasaidizi wanataka ayaendeleze
 
Kama ningekuwa mimi Samia nafukuza wote hao vidudu mtu wa Magu kwenye system, yeye ndio ana power sasa hivi hakuna sababu yeyote ya kukaa pamoja na watu wanaotaka aeneleze mabaya ya mtangulizi wake, Samia fukuzia mbali hao wakora watakuharibia kazi, miaka minne ya urais inatosha sana wasikubabaishe na 2025 yao
 
Ukiona mtu anang'ang'ania kwenye gari bovu ujuwe ana mzigo wake. Wanajifanya eti wanalinda "legacy ya Magufuli". Wanataka hata kutulazimisha tuigize kuhuzunika wakati hatuna majonzi. Kumbe wanataka tuwasindikize kwenye masilahi yao.

Legacy na majonzi havilazimishwi, vinatokea tu vyenyewe. Magufuli amefanya uovu mwingi akitumia vyombo vya dola kuliko 'yale wanayoyaita mafanikio' ndiyo maana zinatumika nguvu nyingi kulazimisha watu waone kuwa kinyesi ni keki.
Ni ukweli usiofichika kuwa kuna mkakati wa ndani ya Bunge na baadhi ya Mawaziri wakiongozwa na PM mwenyewe kum pre empty Rais Mama Samia ili ajikute anafanya kazi bila kwenda kinyume na mtangulizi wake JPM.
Mkakati huo unaoendeshwa kimahesabu sina hakika kama Rais ameshaushtukia au kwa vile timu ya wasaidizi wake ni ileile anaweza kuwa anafunikwa na blanketi na halioni hilo?
Jee ni kwa nini mbinu hizo chafu zinafanywa? Jee mama haoni kuwa kuendelea na wasaidizi wasio kubaliana kifikra kuwa yeye ni Rais kwa sasa itakwamisha mipango yake?
 
Kamanda hivi mnafikiri kwa upuuzi mnaweza kuifitinisha serikali?muda unakuja,hamtapata mnayoyata mrudie kazi yenu ya ramli na matusi
Daaaaaaaaa, mkuu upo? Nikajua UMEZIKWA NAYE kule Chato! Au, baada ya JINI kuangamizwa kwa MAOMBI, basi mliokuwa LIMEWAVAA hilo jini MNAKUWA MMEPONA, kumbe waaaapiiii!
 
Ni ukweli usiofichika kuwa kuna mkakati wa ndani ya Bunge na baadhi ya Mawaziri wakiongozwa na PM mwenyewe kum pre empty Rais Mama Samia ili ajikute anafanya kazi bila kwenda kinyume na mtangulizi wake JPM.
Mkakati huo unaoendeshwa kimahesabu sina hakika kama Rais ameshaushtukia au kwa vile timu ya wasaidizi wake ni ileile anaweza kuwa anafunikwa na blanketi na halioni hilo?
Jee ni kwa nini mbinu hizo chafu zinafanywa? Jee mama haoni kuwa kuendelea na wasaidizi wasio kubaliana kifikra kuwa yeye ni Rais kwa sasa itakwamisha mipango yake?
Nilishaonya kuwa hili Sukuma Gang ni genge hatari sana,lisipodhibitiwa Mama atakuwa na wakati mgumu kutekeleza majukumu yake. Limepewa jina Sukuma Gang kwa vile waasisi wake ni wa kanda hiyo lakini sasa limepanua wigo wake na kuhusisha watu nje ya kanda hiyo lakini wenye mtazamo hasi kwa uongozi wa Rais Samia.
 
Ni ukweli usiofichika kuwa kuna mkakati wa ndani ya Bunge na baadhi ya Mawaziri wakiongozwa na PM mwenyewe kum pre empty Rais Mama Samia ili ajikute anafanya kazi bila kwenda kinyume na mtangulizi wake JPM.
Mkakati huo unaoendeshwa kimahesabu sina hakika kama Rais ameshaushtukia au kwa vile timu ya wasaidizi wake ni ileile anaweza kuwa anafunikwa na blanketi na halioni hilo?
Jee ni kwa nini mbinu hizo chafu zinafanywa? Jee mama haoni kuwa kuendelea na wasaidizi wasio kubaliana kifikra kuwa yeye ni Rais kwa sasa itakwamisha mipango yake?
Naendelea kusisitiza jamani Samia tusimpangie!. Anajitambua, anajielewa na anajua anafanya nini, huu wasiwasi kwanini?!. Kama amemtoa Bashiru kwenye ukatibu mkuu kiongozi na kumtupa kule kapuni, atamshindwa nani?!. Changes is a gradual process, mpeni mama Samia muda wa kutosha kuipanga timu yake, tusimpangie na tusimuharakishe. Hata kwa wasaidizi wake, sio lazima awabadili wote kama kusafisha nyumba, wale atao waona wana fit, wataendelea, wa kubadilishwa watabadilishwa it's just a matter of time.
P
 
Ni ukweli usiofichika kuwa kuna mkakati wa ndani ya Bunge na baadhi ya Mawaziri wakiongozwa na PM mwenyewe kum pre empty Rais Mama Samia ili ajikute anafanya kazi bila kwenda kinyume na mtangulizi wake JPM.
Mkakati huo unaoendeshwa kimahesabu sina hakika kama Rais ameshaushtukia au kwa vile timu ya wasaidizi wake ni ileile anaweza kuwa anafunikwa na blanketi na halioni hilo?
Jee ni kwa nini mbinu hizo chafu zinafanywa? Jee mama haoni kuwa kuendelea na wasaidizi wasio kubaliana kifikra kuwa yeye ni Rais kwa sasa itakwamisha mipango yake?
Toa mfano angalau wa mambo matatu tu.

Maana kama ilani inayotekelezwa ni ile ile ya 2020 - 2025 sijui unategemea apite njia ipi.

Kwa yale ambayo sio ya ki- ilani ni lipi amelazimishwa kulifanya?
 
Kelele zimekuwa aendeleze ya Magufuli!! Mama sanuka, unaingizwa mkenge
 
Legacy ya shujaa wa Afrika kwa taifa letu, itabaki kizazi na kizazi.
Ni kweli tutaendelea kukumbuka watu wasiojulikana, maiti za kwenye viroba, wapinzani kutekwa,kuteswa,kupotezwa,kuuwawa, kubambikiwa kesi,wizi wa kura,kura za kwenye mabegi nk nk nk............
 
Kwa maoni yangu ni kuwa Mama samia Amerithi serikali ambayo yeye alikuwa sehemu yake na ilikuwa na malengo kulingana na ilani ya uchaguzi iliyowaweka madarakani pale, kwa hiyo swala ni ukamilishaji wa ilani ile. Ni maoni yangu tu, siyo kuwa kwa vile karithi serikali na yeye ndiyo bosi basi ilani yao haina maana tena ila yeye ataleta ya kwa kwake tofauti; sidhani kama kweli mambo yanatakiwa yawe hivyo. Wenzetu husema elections have consequences, ambazo yeye atatakiwa azisimamie siyo kuwa azifute.

Rekebisha hapo hakuna ilani ilowaweka madarakani ila walipora madaraka na kulazimisha ushindi.
 
Ni ukweli usiofichika kuwa kuna mkakati wa ndani ya Bunge na baadhi ya Mawaziri wakiongozwa na PM mwenyewe kum pre empty Rais Mama Samia ili ajikute anafanya kazi bila kwenda kinyume na mtangulizi wake JPM.

Mkakati huo unaoendeshwa kimahesabu sina hakika kama Rais ameshaushtukia au kwa vile timu ya wasaidizi wake ni ileile anaweza kuwa anafunikwa na blanketi na halioni hilo?

Je, ni kwa nini mbinu hizo chafu zinafanywa? Je, mama haoni kuwa kuendelea na wasaidizi wasio kubaliana kifikra kuwa yeye ni Rais kwa sasa itakwamisha mipango yake?
Acheni bunge liwe huru kubadili.

Mnataka liwe linaongea as if liko ikulu?
 
Ni ukweli usiofichika kuwa kuna mkakati wa ndani ya Bunge na baadhi ya Mawaziri wakiongozwa na PM mwenyewe kum pre empty Rais Mama Samia ili ajikute anafanya kazi bila kwenda kinyume na mtangulizi wake JPM.

Mkakati huo unaoendeshwa kimahesabu sina hakika kama Rais ameshaushtukia au kwa vile timu ya wasaidizi wake ni ileile anaweza kuwa anafunikwa na blanketi na halioni hilo?

Je, ni kwa nini mbinu hizo chafu zinafanywa? Je, mama haoni kuwa kuendelea na wasaidizi wasio kubaliana kifikra kuwa yeye ni Rais kwa sasa itakwamisha mipango yake?
Mdau unaweza kukuta mama mwenyewe ndio kataka kuendeleza pale alipoanza mwenzie
 
Ni ukweli usiofichika kuwa kuna mkakati wa ndani ya Bunge na baadhi ya Mawaziri wakiongozwa na PM mwenyewe kum pre empty Rais Mama Samia ili ajikute anafanya kazi bila kwenda kinyume na mtangulizi wake JPM.

Mkakati huo unaoendeshwa kimahesabu sina hakika kama Rais ameshaushtukia au kwa vile timu ya wasaidizi wake ni ileile anaweza kuwa anafunikwa na blanketi na halioni hilo?

Je, ni kwa nini mbinu hizo chafu zinafanywa? Je, mama haoni kuwa kuendelea na wasaidizi wasio kubaliana kifikra kuwa yeye ni Rais kwa sasa itakwamisha mipango yake?
Acha ramli, we ulikutana nao wapi wakakwambia hivo?
 
Back
Top Bottom