Kwanini wanataka kuzuia Rais Samia Suluhu asiende kinyume na Hayati Magufuli?

Kwanini wanataka kuzuia Rais Samia Suluhu asiende kinyume na Hayati Magufuli?

Huwezi kurithi mambo ya hovyo tena mengine mlikuwa mnapangiwa na mwendazake tu hayo katika ilani. Hata yaliyokuwapo utekelezaji wake ulikuwa wa hovyo.

Kwa maoni yangu ni kuwa Mama samia Amerithi serikali ambayo yeye alikuwa sehemu yake na ilikuwa na malengo kulingana na ilani ya uchaguzi iliyowaweka madarakani pale, kwa hiyo swala ni ukamilishaji wa ilani ile. Ni maoni yangu tu, siyo kuwa kwa vile karithi serikali na yeye ndiyo bosi basi ilani yao haina maana tena ila yeye ataleta ya kwa kwake tofauti; sidhani kama kweli mambo yanatakiwa yawe hivyo. Wenzetu husema elections have consequences, ambazo yeye atatakiwa azisimamie siyo kuwa azifute.
 
Huwezi kurithi mambo ya hovyo tena mengine mlikuwa mnapangiwa na mwendazake tu hayo katika ilani. Hata yaliyokuwapo utekelezaji wake ulikuwa wa hovyo.
Ni kweli, mawazo binafsi ya Magufuri hayawezi kurithiwa, ila sera zote zilizo kwenye ilani ya CCM aliyeokuwa akitekeleza zitarithiwa.
 
Ndio maana tulishauri apangue "MASALIA YOTE YA MEKO" kama anataka kwenda mbele ,aiendelea kuwakumbatia lazima watamuingiza CHAKA maana hawawezi kwenda tofauti na MEKO maana watanekana MANDUMILAKUWILI.
Ikibidi hivyo na yeye ajipangue!
 
Ukubali usikubali Hayati JPM alikuwa visionary leader na akawafundisha Watanzania na wakamuelewa. Akaweka viwango vya kiuongozi wa kuwa mtumishi wa watu na sio bwenyenye la kuwatumikisha watu.

Kwa kiongozi yeyote wa sasa Tanzania lazima na hana budi kuzingatia na kuhakikisha kila anachoamua na kufanya angalau kiendane na viwango alivyo visimika Hayati JPM. Usipofanya hivyo viwango hivyo kwa kutumia unao waongoza na kuwatumikia vitakufyekelea mbali. Wale mliogongesha glass za mvinyo mkifikiri JPM kafa na mnarudi kwenye shamba la bibi kuhomola mjitathimini na kufikiria upya.

Hotuba ya PM ilivyo shangiliwa Bungeni lakini Mh Bashiru jina lilipotajwa tu unapata picha gani? Mh Rais hawezi kujitenga na viongozi aliohudumu pamoja nao akiwa Naibu wa Rais wa Hayati JPM. Halafu akaleta majipu taambazi yaliotumbuliwa na JPM akabaki salama, nguvu ya ummati wa Watanzania itawatumbua kwa niaba ya Hayati JPM kwa wakati na majira na kwa namna na jinsi ambayo watao wao inafaa.
 
Ni ukweli usiofichika kuwa kuna mkakati wa ndani ya Bunge na baadhi ya Mawaziri wakiongozwa na PM mwenyewe kum pre empty Rais Mama Samia ili ajikute anafanya kazi bila kwenda kinyume na mtangulizi wake JPM....
Aende kinyume, kwani yeye ni mpinzani? Au kaja na ilani tofauti ya uchaguzi?
 
Ndio maana tulishauri apangue "MASALIA YOTE YA MEKO" kama anataka kwenda mbele ,aiendelea kuwakumbatia lazima watamuingiza CHAKA maana hawawezi kwenda tofauti na MEKO maana watanekana MANDUMILAKUWILI.
Yeye mwenyewe mama ni masalia ya Meko na ndio maana hadi sasa bado havai hata barakoa kumuenzi Meko.
 
Meko ni nani?
Masalia ni kina nani?
Rais SSH amekua akifanya kazi na nani kabla ya kuwa rais?
Haijalishi kufanya nao kazi, je alikuwa anaridhika na utendaji ndani ya system?
Kwa speed ile ya kupata ajali ni traffic polisi gani angepiga mkono kumsimamisha?
APANGUE ILI AANZE UPYA
 
Ni ukweli usiofichika kuwa kuna mkakati wa ndani ya Bunge na baadhi ya Mawaziri wakiongozwa na PM mwenyewe kum pre empty Rais Mama Samia ili ajikute anafanya kazi bila kwenda kinyume na mtangulizi wake JPM....
1. MFUMO uliomweka JPM madarakani ndio uliomweka SSH madarakani. Hawezi kuubadili yeye binafsi.

2. Yeye ni sehemu ya waasisi wa MFUMO kwsbb alishiriki kuipinga 'katiba ya Warioba'. Pamoja na marais waliopita: (Mkapa, Mwinyi, na Kikwete) ndio maana Mwinyi alienda kumpongeza juzi kwa "kuanza vizuri" soon atafuatia Kikwete.
 
Kwa maoni yangu ni kuwa Mama samia Amerithi serikali ambayo yeye alikuwa sehemu yake na ilikuwa na malengo kulingana na ilani ya uchaguzi iliyowaweka madarakani pale, kwa hiyo swala ni ukamilishaji wa ilani ile. Ni maoni yangu tu, siyo kuwa kwa vile karithi serikali na yeye ndiyo bosi basi ilani yao haina maana tena ila yeye ataleta ya kwa kwake tofauti; sidhani kama kweli mambo yanatakiwa yawe hivyo. Wenzetu husema elections have consequences, ambazo yeye atatakiwa azisimamie siyo kuwa azifute.
Ilani ya Sisiem ilikuwa inaeleza wazi kuwa wanafunzi watakaobeba mimba wangali shuleni watarejeshwa shuleni mara baada ya kujifungua.

Pamoja na ukweli kuwa ilani hiyo ndiyo iliyomnaji JPM 2015 lkn baada ya kuingia madarakani aliapa kutomrejesha shuleni mwanafunzi yeyote atakayepata ujauzito. Yapo mengi sana aliyafanya ambayo hayapo kwenye ilani, kama kuhamia dodoma nk.

Hivyo ilani ni tiketi tuu ya kukuingiza madarakani, ukishaingia unaamua uonavyo
 
Ilani ya Sisiem ilikuwa inaeleza wazi kuwa wanafunzi watakaobeba mimba wangali shuleni watarejeshwa shuleni mara baada ya kujifungua.
Pamoja na ukweli kuwa ilani hiyo ndiyo iliyomnaji JPM 2015 lkn baada ya kuingia madarakani aliapa kutomrejesha shuleni mwanafunzi yeyote atakayepata ujauzito. Yapo mengi sana aliyafanya ambayo hayapo kwenye ilani, kama kuhamia dodoma nk
Hivyo ilani ni tiketi tuu ya kukuingiza madarakani, ukishaingia unaamua uonavyo
Hiyo ya watoto wazazi kurudi shule siwezi kuijibu kwa vile sina data nayo, lakini hili kuhamia Dodoma ilikuwa ni unfinished business ya Ilani ya CCM ya miaka mingi iliyopita, na yeye alitaka kumalizia. Siyo kuwa kila ahadi iliyomo kwenya ilani hupata nafasi ya kukamilishwa ila siyo vizuri kukana ahadi iliomo kwenye ilani hiyo.
 
As long as amewaacha mamuluki akia Kasim, basi ameliwa . she has to take note of that!
kumuacha Kasimu lilikuwa kosa kubwa sana , sasa wameanza kupanga kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye , atavuna alichopanda
 
Kwa maoni yangu ni kuwa Mama samia Amerithi serikali ambayo yeye alikuwa sehemu yake na ilikuwa na malengo kulingana na ilani ya uchaguzi iliyowaweka madarakani pale, kwa hiyo swala ni ukamilishaji wa ilani ile. Ni maoni yangu tu, siyo kuwa kwa vile karithi serikali na yeye ndiyo bosi basi ilani yao haina maana tena ila yeye ataleta ya kwa kwake tofauti; sidhani kama kweli mambo yanatakiwa yawe hivyo. Wenzetu husema elections have consequences, ambazo yeye atatakiwa azisimamie siyo kuwa azifute.
Nyie uchaguzi si huwa mnaiba? Mnahofu ya nn?
 
Pm anahangaika na Mambo ya jiwe hajui kuwa Kuna utawala mpya, ningekuwa Mimi nawatoa na weka watu wangu watakaolewa maono yangu na sio ya mwendazake
 
"Kodi ya dhuluma, hapana"! Hii ni moja kati ya departure nzuri sana. Naamini na ule uozo na unyang'anyi wa DPP kwenye kesi za kubumba za uhujumu uchumi na money laundering hawezi kuendelea nao...
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Pm anahangaika na Mambo ya jiwe hajui kuwa Kuna utawala mpya, ningekuwa Mimi nawatoa na weka watu wangu watakaolewa maono yangu na sio ya mwendazake

Kitendo cha kumuweka Mh Mpango kama Naibu wa Rais itoshe kukufanya uelewe na kukupa ujumbe kwamba mahisabu ya siasa za Tanzania yame kuwa magumu kama Calculus kwa mijizi na mafisadi na wapambe wao.

Kelele na mihemuko ya pangapangua ya safu za kiuongozi sizisikii tena. Mambo si rahisi kama unavyotaka yawe. Ni suala la kuamua uweke nje jeshi kubwa la kupigana/kupingana nawe ama ulikumbatie jeshi kubwa la kukupambania.
 
Back
Top Bottom