Kwanini wanaume waliooa huacha kuwashirikisha wenza wao kwenye vyanzo vyao vya mapato?

Kwanini wanaume waliooa huacha kuwashirikisha wenza wao kwenye vyanzo vyao vya mapato?

NAOMBA NITOE YANGU YA MOYONI NA HII IMENIFIKA MIMI ,NATAKA IWASAIDIE WANAUME AMBAO WANATAKA KUOA.


nina mwaka wa 3 kwenye ndoa na maisha yangu ya ndoa ni ya furaha mke hana tatizo na ana akili ya maisha vzri tu.

Mke wako kujua mshahara wako haina shida kama ana akili ya maisha na akiba.
mimi mke wangu ni mchumi na mbahili kwenye hela kuliko hata mimi,yani naweza nkabaki na laki 2 ya mwisho mfukoni ,wife akijua hilo tunaingia katika state ya POWER MODE/BATTERY SAVER matumizi yanabanwa ili yafike mwisho wa mwezi.


SHIDA IPO HIVII.........

Kwa kuwa mshahara mke wangua anaujua ,kila expenditure ya hela lzma atake kujua yani [emoji23][emoji23][emoji23] wakuu nacheka kama mazuri ,

nikitoa 50k nihonge ka manzi ka pembeni ,atahoji ""ile 50k mbona siioni umenunua nini?""
nkienda pata maji matamu/bia nkaspend kama 80k kwa usiku mmoja ,ni ugomvi nyumbani kwamba nafuja hela

CHA KUSHANGAZA WAKUU.

mimi huwa natoa 75% ya mshahara naleta home ili ukae na 25% unabaki benki na mke anajua mgawanyo wa hela ,ila ataenda kuhesabu upya hela nilizoleta tena anaweka na MATE kwenye kidole azihesabu vzri kwa kifupi nisiwachoshe wakuu ni kama CAG / mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za nyumbani.
hata nkisema nilete ukali sa hv tyr kashaujua mshahara nirahisi kunifatilia sana.

NILICHOPANGA KUFANYA

nkipata post na promotion kazini ya nyongeza ya hela hatokuja kuijuaaa kwamweeee ,kamweeeee

kidume hata hela ya kuchepuka sina ,hili kosa la kujifanya HUSBAND MATERIAL SIYO ZURI JMN. MWANAUME NI MWENDO WA JICHO NYANYA TU

Mke ajue 75% ya salary ,Ndugu zako wajue 25% ya mshahar jiroge waambie ndugu unapokea milioni utajua haujui , mchepuko hapaswi kujua mshahara kbsaaa...

ova
Haahaaahaaa haha..husband material [emoji38]
 
Mkuu mimi na hustle mzee ila kwenye developments za familia lazma mwanamke nae mchango wake uonekane! One of my Qualities za mwanamke sitaki mwanamke mchoyo wala tegemezi!

Mimi sitaoa matako wala sura nzuri focus ni brain na attitude ya mwanamke mwenyewe na ambitions! Nyie mnaooa wanawake wa kufuga ili muwapelekeshe oeni tu! Ishu ni mwanamke mwenye uchungu na family na kuhakikisha tunashirikiana kujenga familia bora!

salute chief [emoji1478]
 
Nikitazama mtiririko wa michango naona vijana wanazidi kuwatambua wanawake na namna ya kuishi nao......hali hii itapelekea kupunguza vifo vya wanaume wengi na magonjwa ya msongo wa mawazo........

Sifa kuu ya mwanaume ni kuhakikisha kuwa familia yake inapata mahitaji yote ya msingi kwa wakati muafaka........
 
Wanaume wasiojielewa ndio huficha mambo Matokeo Yao hufa ghafla na kuacha familia ikiteseka, Sasa unaishije na mtu usiye mwamini na hamshirikishani mambo yenu, wanaume oeni wanawake mnaoendana nao vision
Ukikua utaelewa kwani maoni mengi ni tofauti na unavyodhani wewe
 
Haahaaahaaa[emoji38][emoji38][emoji23][emoji23]

Hivi wanawake wana nini na hela? Shetani alimwambia nini Eva baada ya tunda kuhusu hela?[emoji38][emoji38][emoji38]

[emoji23][emoji23] kwa kweli najiiliza kila siku hili swali maana hata Sheitani anakuna kichwa

Kuna mara naona niwasaidie baadhi na kuwapa hata mtaji ila kibri nayo inawasumbua
Kutwa kuomba ila ukimwambia shika mtaji anza biashara ndogo hataki hilo ndio tatizo
Wengi ni ombaomba (sorry) [emoji23][emoji23]
 
Tunaficha mambo mengi sababu nyie sio wavumilivu kabisa! Kidume unajipinda unaweka akiba inafika hata 10M kwa ajiri ya long run projects,kama kujenga au kuanzisha biashara, mwanamke wako akishajua tu,anaanza kupanga mipango yake,mara hii tv,tuibadilishe,mara sijui hizi sofa zimepitwa na wakati,mara sijui tufanye sherehe ya miaka 2 ya ndoa yetu!

Pia wanawake hua na viherehere,anaweza chukua kile kikaratasi cha Salio,anaenda mringishia rafiki yake huko,yeye hajui kama anakutafutia kifo,maana wanaweza kuipata wazee wa ngwasuma,wakatimba usiku wa manane kuomba salio,bahati mbaya usiwe nalo home liwe bank,wanakuuwa!
Pamoja na kwamba sisi kama binadamu- wake kwa waume hata tunapokuwa watu wazima kuna nyakati huwa tunafanya mambo ya kitoto na kijinga.

Lakini kwa upande wa wanawake mambo yao ya kitoto na kijinga ni mengi zaidi ya wanaume.
 
Tunaficha mambo mengi sababu nyie sio wavumilivu kabisa! Kidume unajipinda unaweka akiba inafika hata 10M kwa ajiri ya long run projects,kama kujenga au kuanzisha biashara, mwanamke wako akishajua tu,anaanza kupanga mipango yake,mara hii tv,tuibadilishe,mara sijui hizi sofa zimepitwa na wakati,mara sijui tufanye sherehe ya miaka 2 ya ndoa yetu!

Pia wanawake hua na viherehere,anaweza chukua kile kikaratasi cha Salio,anaenda mringishia rafiki yake huko,yeye hajui kama anakutafutia kifo,maana wanaweza kuipata wazee wa ngwasuma,wakatimba usiku wa manane kuomba salio,bahati mbaya usiwe nalo home liwe bank,wanakuuwa!

[emoji16][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Shida kama anakuhudumia ipasavyo wewe hayo hayakuhusu mwache na hela zake

Kikubwa malengo au mipango mikakati ya maisha yenu lazima uyajue haya kama huyajui mume anaamka anaamua tu anafanya nn anaenda site mwenyewe hakushirikishi hili ndio tatizo na sio kipato chake.
Wewe inatakiwa ujengewe Sanamu pale round about DODOMA.
 
Wanaume wasiojielewa ndio huficha mambo Matokeo Yao hufa ghafla na kuacha familia ikiteseka, Sasa unaishije na mtu usiye mwamini na hamshirikishani mambo yenu, wanaume oeni wanawake mnaoendana nao vision
Mimi nipo upande huu wa Wanaume wasiojielewa,na ninataka nibaki huku huku.
 
Wanaume wote wana fikra sawa na wewe ila shida moja ni kuwa hawa viumbe wote wanafanana tabia sasa utaacha wangapi
Ndugu yangu kama mlivyo nyie hamfanani bac nasisi wanawake hatufanani sabab huwezi kuniweka kundi moja na kahaba au Malaya wa mitaani
 
mwanamke unaepaswa kuwa nae karibu sana na kumshirikisha kwa kila jambo ni Mama yako tu.
Acheni ubinafsi kama mama yako asingeaminiwa na baba yako Leo mngefika hapo ebu waangalie wanao ni yupi atakae Walea na kuwajali zaid nimama yao ila mama yako hawezi kuonyesha upendo mkubwa kama alionao mama yao hivyo kama umeamua hivyo bac jua wanao wataish maisha magumu na watakukumbuka kwa mabaya yako na kukulaani kila Leo na ikiwa bahat mbaya wakakosa support ya elimu labda ukifarik hapo ndio chuki itaongezeka Mara dufu.
Kama unamuona mama wa thaman sana kuliko mkeo ni bora usioe wala usiwe na watt
 
Mjomba tu ndio alikuwa anajua?[emoji28] safi ni ndugu yake haina ubaya hio aliojengewa mke inatosha
Sidhan kama inatosha sabb kaacha watoto hao watoto wataishije watakuwa vipi naukute mama yao alikatazwa asifanye kazi hao watt nani atakae wasaidia kutimiza ndoto zao? Tukijiuliza maswali hayo inapaswa wanaume kama umuamin mkeo ila assets zako andika majina ya wanao kwani hakuna atakae wadhurum wala Mali zake hazito teketea
 
Hahahahah umeongea kweli kabisa maana tukumbuke mapenzi huwa yanaisha na urafiki unakufa ila undugu haufagi!

Mke unayempenda na kumkabidhi michongo yako yote ni rahisi sana kuja kukumaliza yani maana akilianzisha huko dawati lazma atakuminya kende tu[emoji28] yani atahakikisha amekomba kila ulichonacho una lodge zako mgawane, una hoteli napo ale share, una malori sijui coaster yani vyanzo vyote lazma ahakikishe kakukomesha.

Wanawake ni kuishi nao kwa akili na miongoni mwa vitu ambavyo ni vya kuwa navyo makini ni jasho lako na vyanzo vya pesa. Usije ukaishia kufa kwa stress! Limit michongo yako hata siku akianza vurugu mnaachana kiroho safi!

Kuna yale mapumbavu yanafunguaga joint account kabisa na wake zao[emoji28] yani ushee pool ya pesa na mkeo? Upuuzi wa kiwango cha lami! Kujitaftia mabalaa tu.
[emoji1] [emoji1] [emoji1] ni mahaba tu yamemkolea
 
Kuna kitu umekigusa hapo, Mimi mara nyingi huwaga napishana kauli na mke wangu kwa suala kama Hilo... Siku hizi ananiuliza eti pesa hazioni naficha kwenye gari... Sasa na Mimi namuuliza swali niambie ni siku gani umelala na njaa, na siku gani ndani sijakupa akiba na Hela yako ya matumizi binafsi? Anakosa jibu maana hakuna hata siku moja ambayo kakosa anachikitaka kwa matumizi ya mwezi mzima. Ila ndo hivo hamridhiki mpaka muoneshwe pesa mkononi.
Mmmmhhhh sio wote maana kama kunakuwa na bajeti ya familia kila mwezi huwezi kutumia pesa hovyo na ili ujue unatoa kias gani. Kwanza unapaswa kukaa na mkeo kupanga bajeti iwe katika sehem Tatu
1. Chakula, kama wote ni wafanyakaz inabid kila mtu achangie kiasi chapesa ila mume uwe zaid ya mke namjue vitu gani ndani vinahitaj kwa suala la chakula na inagharm bei gan kwa manunuz
2. Elimu, kama mnawatoto mnapaswa kufungua account ya familia kulingana na idad ya watoto mlionao inapaswa kila mtu achangie kwa asilimia kadhaa kweny hiyo account
3. Afya. Sasa hapa mnaweka pesa ya akiba ikitokea jambo lolote la dharula itawasaidia kama matatiz ya wazaz au ndugu mnachukua kweny pesa hii ambayo mnaitunza kila mwezi
MKIFANYA HIVI KILA MTU ATAKUWA NA UHURU WA KUPAMBANA NA FAMILIA NA KUONDOA HALI YA UTEGEMEZI PANDE ZOTE MBILI NA PESA YENU MTAJUA MATUMIZ YAKE MTAPUNGUZA GHARAMA ZINGINE AMBAZO HAZINA MSINGI
 
Kuna mwanamke asiyedanga?! Ukiamini basi siku ya kujuwa lazima ufe kwa pressure tu
Sio wote wanaodanga ndugu kulingana na tabia ya mume mchapukaji ndio wanahofia na wake zao watachepuka
 
Back
Top Bottom