Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 7,672
- 9,039
Wanangu, huwa sipendi kuchangia wala kujadili mambo ya ngono na mambo binafsi. Ila baada ya kusoma nyuzi nyingi za wanaume wanaobemendwa na wake zao wakijifanya vijogoo, nimeamua lau leo niulize. Kuna nyuzi nyingi za kuwakandia na kuwaonyesha wanawake kama viumbe wa ajabu na dhaifu. Nahisi wengi wanaoleta nyuzi kama hizi ni wahanga wanaolipiza kisasi bila kutaka kujulikana kuwa ni wahanga. Nashauri waache. Imetosha. Tushaona na kujua mateso yao na tunawapa pole.