ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Jamii gani hiyo?Kwa nini wanawake Waislamu hawaruhusiwi kushiriki shughuli muhimu za maziko kama hata kwenda makaburini kuzika wapendwa wao?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jamii gani hiyo?Kwa nini wanawake Waislamu hawaruhusiwi kushiriki shughuli muhimu za maziko kama hata kwenda makaburini kuzika wapendwa wao?
Uislamu ni QURAN na SUNAH kwanza unaelewa hili jambo?halafu mimi nilikuwa namjibu kwa ujumla kuwa dini haina kwanini ukipewa amri ni kutiiLeta kifungu cha Quran kinacholataza hilo.
Kuna nchi moja huko Asia inaitwa Afghanistan nayo imekataza wanawake wasiende shule. Nao wanadai Quran imekataza.
Kila Waislam wakitaka kumfanya mwanamke ni bidhaa husinguzia Quran. Acheni uwongo. Leta hilo katazo hapa kwa kunukuu Quran
Hakuna tatizo hadith zenye mashaka zina fahamika na mashaka yake yameelezwa , ndio maana pamoja na mashaka lakini wote Suni kwa shia bado wanatumia hadith, ndio maana waprotestant waliacha vile vitabu 6 ambavyo Waroma wanavitumia mpaka leo, huwezi kuzuia watu kutafsiri au kutokukubaliana ipo hiyo siku zoteKuna Mashaka kwenye hadithi ndio sababu hata Mashia kuna hadithi wanazipinga ila kwenye Qur'an hakuna utata.
Kitu kikishakuwa na shaka kinapoteza credibility, ndio maana unakuta watu wanabase kwenye Qur'an ambayo haina shaka.Hakuna tatizo hadith zenye mashaka zina fahamika na mashaka yake yameelezwa , ndio maana pamoja na mashaka lakini wote Suni kwa shia bado wanatumia hadith, ndio maana waprotestant waliacha vile vitabu 6 ambavyo Waroma wanavitumia mpaka leo, huwezi kuzuia watu kutafsiri au kutokukubaliana ipo hiyo siku zote
Kwenye mwendokasi, kwenye daladala, shuleni, vyuoni mbona mnachangamana?Sio utamaduni wa Dini ya Kiislam kuchangamana wanaume na wanawake. Full stop
Saudia Arabia sio utawala wa kiislamu? Mpogolo wa ifakara unaujua uislamu na kuishi uislamu kuliko wasaudia Arabia ambapo kibra ipo huko, ambapo Quran ilishushwa huko kwa ajili yao.sasa magari yana husika vip na Uislamu?muwe mnaelewa kuwa Saudi Arabia sio utawala wa kiislamu ule, ni tawala za watu tu walizo jiamulia
udhaifu wa hadithi na usahihi upo wazi, wala hakuna cha kushangaza ndio maana watu wanakubaliana kwenye vingi, hivyo vichache tunavyotofautiana Mungu anajua nani sahihiKitu kikishakuwa na shaka kinapoteza credibility, ndio maana unakuta watu wanabase kwenye Qur'an ambayo haina shaka.
Hapo hapo.Ili Wanaume msije kuwatamani
Mtume kazaliwa pale na kapambana na makafiri wa pale, utawala ule sio wa kiislamu ni wakifalme tu usiwe mvivu kufatilia basi, kule Israel serikali inaruhusu mpaka paredi za mashoga kwa akili zako utasema ni utawala wa kibiblia uleSaudia Arabia sio utawala wa kiislamu? Mpogolo wa ifakara unaujua uislamu na kuishi uislamu kuliko wasaudia Arabia ambapo kibra ipo huko, ambapo Quran ilishushwa huko kwa ajili yao.
Huwa mnachekeshaga sana
Kwasababu sio nchi inayofata sheria ya kiislamu, ila mkipata nafasi ya kufata sheria mnafata bila tabuu, kuzoeleka kwa haramu haifanyi kuwa ni halaliKwenye mwendokasi, kwenye daladala, shuleni, vyuoni mbona mnachangamana?
Ni Kwa sababu hakuna Mabasi ya Kiislam, Kwa shule zinazofuata utaratibu wa Kiislam wanawake hutenganishwa na wanaume madarasaniKwenye mwendokasi, kwenye daladala, shuleni, vyuoni mbona mnachangamana?
Saudi Arabia ni nchi ya kiislamu, inafuata sharia.Mtume kazaliwa pale na kapambana na makafiri wa pale, utawala ule sio wa kiislamu ni wakifalme tu usiwe mvivu kufatilia basi, kule Israel serikali inaruhusu mpaka paredi za mashoga kwa akili zako utasema ni utawala wa kibiblia ule
Hapo sasa hakuna utofauti. Ni sawa na kenge anakimbia mvua alafu anaenda kuingia bwawaniNi Kwa sababu hakuna Mabasi ya Kiislam, Kwa shule zinazofuata utaratibu wa Kiislam wanawake hutenganishwa na wanaume madarasani
Lengo langu ni kuonyesha kuwa hayo mnayosema hayana maana kwa sasa kwa maisha yaliyopo. Huwezi kukwepa kuchangama na wanawakeKwasababu sio nchi inayofata sheria ya kiislamu, ila mkipata nafasi ya kufata sheria mnafata bila tabuu, kuzoeleka kwa haramu haifanyi kuwa ni halali
Ni kwanini Wakristo mnalazimisha Waislam wafanya mfanyavyo? Waislam na Qur An Yao imewaambia kwamba '...hawatokuwa radhi nanyi mayahudi na manaswara(Wakristo) mpaka mfuate Mila zao....'Hapo sasa hakuna utofauti. Ni sawa na kenge anakimbia mvua alafu anaenda kuingia bwawani
Ukweli wa mambo kwa maisha ya sasa hayo mambo yenu yamepitwa na wakati. Hamtaki kuchangama na wanawake lakini kwenye mwendokasi mnabambiana, kwenye daladala mnapumuliana, Sasa mnakua mmefanya nini?
1.Saudia Arabia ni nchi yenye waislamu wengi kwa maana ya wakazi sio nchi ya kiislamu kwa maana ya kuongozwa na Quran na Sunan, ile ni nchi ya kifalme tu ilio amua kufanya uislamu kuwa dini rasmi na kiarabu kuwa lugha rasmi hakuna la ziada pale , ndio maana wanarithishana tu babu, baba na watoto ile nchiSaudi Arabia ni nchi ya kiislamu, inafuata sharia.
Israel mara nyingi hapa nimesoma na nasoma kuwa hawaupendi ukristo, wanaupiga marufuku ukristo, hairuhusiwi kumtaja kristo. Pia mara nyingi tumekubaliana Israel wakristo ni wachache kuliko hata waislamu na ipo hivyo.
Tufahamu kwanza kabla hatujaslimWatu waheshimu imani za wengine. Mnaotaka kujua kwanini wanawake hawaruhusiwi makaburini kwenye uislamu jiungeni na uislamu ili mjifunze.
Jibu likipatikana uniite, naenda kusonga ugali kwanzaNasema sibanduki hapa mpaka kielewe, toeni sababu watu tujifunze.
Nimekwambia haramu haiwezi kuwa halali kisa imezoeleka, lazima watu wakumbushwe kuwa jambo fulani sio sawa hata kama linafanyikaLengo langu ni kuonyesha kuwa hayo mnayosema hayana maana kwa sasa kwa maisha yaliyopo. Huwezi kukwepa kuchangama na wanawake