Kwanini wanawake wawe na siku yao (Women's Day) na si wanaume?

Kwanini wanawake wawe na siku yao (Women's Day) na si wanaume?

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
15,266
Reaction score
25,555
Mdau amani kwako.

Napenda tujifunze na kupeana elimu kwa undani juu ya hili jambo la 'siku ya mwanamke duniani'.

Mwanzoni wakati dunia ikiwa na amani na upendo Adamu na Hawa walijiona kuwa wenye kufanana na wakiwa na majukumu tofauti kulingana na maelekezo waliyopewa na Allah.

Baadaye kidogo kuna vita ya kimamlaka ambayo leo ndiyo inasumbua dunia kupelekea umoja wa mataifa kutumika kuiweka siku maalum ya mwanamke, hebu tuone kwa ufupi hapa chini.

Tunaambiwa Hawa alikuwa ni mwenye furaha akiwa upande wa mumewe katika nyumba yake pale Edeni; Lakini kama mwanamke wa kisasa alianza kujikweza ili kuchukua nafasi ya juu kuliko ile ambayo Mungu alimpa.

Wanawake wote ambao hawataki kuyabeba kwa furaha majukumu yao ya maisha kwa mujibu wa mpango wa Mungu, katika jitihada zao za kufikia nafasi ambazo hazijawekwa kwa ajili yao wataangukia pua na wengi wanaacha mahali ambapo wanaweza kuwa baraka na kwa tamaa yao ya kutaka kuwa juu, wengi wamepoteza dhabihu ya kweli ya 'kike' na utukufu wa tabia, na wameacha kufanya kazi ambayo mbinguni iliwachagulia.

Kutokana na hilo nagundua kuwa maandiko hasa Mwanzo 2:23 "Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume"

Hapo ilionyesha uwezo unaanzia kwa Adam sababu ndiye alipewa mamlaka ukianzia Genesis verse 21 unaona adam anaandaliwa ili kupewa msaidizi na siyo kiongozi.

Kuna maadili ya siri yaliyo'undwa' ili kutengeza njia rahisi ya kuja kuitawala dunia ambayo ilionekana kupitia mwanamme inakuwa ngumu sana, sababu nature ingali inafanya kazi, hivyo wazee wa secret agenda wakaona watumie ushawishi wa mwanamke, ambaye leo ndiye huyu MODERN EVE anaye andaliwa kuja kurahisisha kazi.

Nawasilisha.
 
Hata sisi wanaume tuna siku yetu! Ni tarehe gani sijui ile!! Sema tu sisi ni wapuuziaji tofauti na hao wenzetu.
 
Hata ya wanaume ipo. Tatizo sisi mambo ni mengi hadi tarehe yenyewe ikifika hujui kama ndio yenyewe
 
Achana nao.

Wanaume kila siku ni yetu.

Tukutane Viti virefu.
 
Upuuzi tu.
Sasa kwenye hii siku ya mwanamke ni nini kilicho tofauti?...
Inaweza kuwa upuuzi kama ulivyosema ila mkuu hii issue ilianza kitambo sana na inapigiwa upatu ili kufikia lengo.
 
Mdau amani kwako.

Napenda tujifunze na kupeana elimu kwa undani juu ya hili jambo la 'siku ya mwanamke duniani'...
Wanawake wanapenda sana kudanganywa ili watumike.

Siku ya wanawake, lakini controller wa siku yenyewe, organizers na waandajai wa matamasha na makongamano ni wanaume.

Tena wengine ndio wadhalilishaji wakubwa wa wanawake. Wanaheshimu mama zao tu.
 
Mdau amani kwako.

Napenda tujifunze na kupeana elimu kwa undani juu ya hili jambo la 'siku ya mwanamke duniani'....
Mbona siku ya Wanaume ipo? Ni Nyinyi wenyewe kuadhimisha hamtaki.
 
TODAYS Naomba ubadili rangi nyeusi katika andiko lako watumiaji wa Dark Mode/Theme waweze kusoma.

Asante.
 
Maana yake hizi siku zingine zote 364 zilizobaki ni za wanaume.
 
Ni muda sasa wanawake waachane na kujihisi inferior, sioni hata sababu ya wao kuwa inferior. Kama ni fursa sasa inaweza kuwa 60-40, wanawake wakiwa na 60% ya fursa.
 
Hapo ilionyesha uwezo unaanzia kwa Adam sababu ndiye alipewa mamlaka ukianzia Genesis verse 21 unaona adam anaandaliwa ili kupewa msaidizi na siyo kiongozi.
Hili somo analiweza Polepole

 
Back
Top Bottom