Kwanini wanawake wenye mafanikio wanaogopwa?

Kwanini wanawake wenye mafanikio wanaogopwa?

Kilenzi _Jr

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2021
Posts
301
Reaction score
1,110
UPO ukweli kuwa wanaume wengi wanawaogopa wanawake wenye mafanikio. Hawa ni wanawake wenye kiwango kikubwa cha elimu, fedha, umaarufu au hata madaraka katika jamii. Hoja ya wanaume wenye mawazo haya ni ugumu wa kuwaongoza wanawake wanaowazidi kama alivyonieleza Godfrey, mwalimu wa sekondari jijini Arusha:

“Mwanawake akipata kitu anakuwa jeuri sana. Hawezi kukusikiliza tena na atataka awe huru kufanya mambo yake bila kuingiliwa.” Kwa mujibu wa Godfrey, uwezo wa kifedha na mafanikio kwenye maeneo mengine ya maisha mara nyingi humfanya mwanamke asiwe na utayari wa kuwa chini ya utawala wa mwanaume. “Huwezi kuishi na mwanamke anayejiona yuko juu yako na ukabaki salama. Hatokuwa tayari kukupa nafasi ya kuwa na sauti kwenye nyumba.”
 
Mwanaume hutafuta pesa ili kumridhisha Mke wake na familia ila Mwanamke hutafuta pesa Kama kujikomboa ili ajitenge na mwanaume na unajua sababu za kutaka kujitenga?

Ili awe na maamuzi ya kujitawala (independent) ambacho huwezi kukiona katika mahusiano yenye amani Kama mwanamke anajitawala hivyo tunaogopa hayo

Britanicca
 
Nawakumbusha tu..
Mama Maria Nyerere yuko hai.
Mama Karume yuko hai.
Mama sokoine yupo hai
Mama Salmin Amour yuko hai
Mama Omary juma yuko hai.
Mama abdul jumbe yuko hai tena WOTE 2
Mama samwel sitta yuko hai
Mama Mkapa yuko hai
Mama Maiga yuko hai.
Mama Maalim Seif yuko hai
Mama Kijaz yuko hai
Mama Janet Magufuli yuko hai.

Tafakari,chukua hatua...WABABA TUNAFELI WAPI?
 
Wanaume wengi Ni dhaifu na wana inferiority complex, wanapenda wanawake wanyonge wawatese Ili waonekane wao ni vidume wa shoka, wanaamini hivyo, sasa mwanamke anayejitegemea mwenye shule wanaume wakitanzania Wana mwogopa ka kituo Cha police na kumwita jeuri
 
Nawakumbusha tu..
Mama Maria Nyerere yuko hai.
Mama Karume yuko hai.
Mama sokoine yupo hai
Mama Salmin Amour yuko hai
Mama Omary juma yuko hai.
Mama abdul jumbe yuko hai tena WOTE 2
Mama samwel sitta yuko hai
Mama Mkapa yuko hai
Mama Maiga yuko hai.
Mama Maalim Seif yuko hai
Mama Kijaz yuko hai
Mama Janet Magufuli yuko hai.

Tafakari,chukua hatua...WABABA TUNAFELI WAPI?
Daaah🤔
 
Mwanaume utafta pesa ili kumridhisha Mke wake na familia ila Mwanamke utafta pesa Kama kujikomboa ili ajitenge na mwanaume na unajua sababu za kutaka kujitenga? Ili awe na maamuzi ya kujitawala (independent) ambacho huwezi kukiona katika mahusiano yenye amani Kama mwanamke anajitawala hivo tunaogopa hayo

Britanicca
So kwetu sisi wanaume tunafanyaje Sasa Ili mwanamke Huyu tumuweke chini yetu?
 
Duh! Mkuu umepotea sana humu jamvini. Nimefurahi kukuona.
Nawakumbusha tu..
Mama Maria Nyerere yuko hai.
Mama Karume yuko hai.
Mama sokoine yupo hai
Mama Salmin Amour yuko hai
Mama Omary juma yuko hai.
Mama abdul jumbe yuko hai tena WOTE 2
Mama samwel sitta yuko hai
Mama Mkapa yuko hai
Mama Maiga yuko hai.
Mama Maalim Seif yuko hai
Mama Kijaz yuko hai
Mama Janet Magufuli yuko hai.

Tafakari,chukua hatua...WABABA TUNAFELI WAPI?
 
Mwanamke mwenye mafanikio binafsi sio wa kawaida. mwanamke akiwa bright anakuwa strong very powerful na kama portalist dunia nayo humlinda
 
Kiasili anaeolewa ni mwanamke, hivyo Mwanaume ndiye anayestahiki kuwa juu ya mke wake.

Hivyo mwanamke mwenye mafanikio hayuko tayari kuwa chini ya mwanaume anaemzidi elimu au mafanikio. Hapo lazima mahusiano yawe na mgongano.

Ndio maana wanawake wengi wenye mafanikio wanaishi wenyewe tu na watoto wao, ndoa huwa zinawashinda
 
Back
Top Bottom