Sokoro waito
JF-Expert Member
- Nov 21, 2014
- 2,201
- 2,599
Usijali nitakutagAkikujibu nitag
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Usijali nitakutagAkikujibu nitag
Najua ulishamsamehe...Aliishia kulia machozi na kusema nimsamehe!
Nimekupenda bureHonestly, nisingeweza kuwa nae tena kwasababu amevunja IMANI yangu juu yake tena ile imani ya mwanzo ambayo haikuwa na mawaa wala unafiki ndani yake...ili niyafurahie maisha yangu sina budi kumkwepa kama ukoma[emoji16]
sawa best nafikiri pia amekuelewa #ThadHonestly, nisingeweza kuwa nae tena kwasababu amevunja IMANI yangu juu yake tena ile imani ya mwanzo ambayo haikuwa na mawaa wala unafiki ndani yake...ili niyafurahie maisha yangu sina budi kumkwepa kama ukoma[emoji16]
One love mamii[emoji6]Nimekupenda bure
Nasemaje kama uko single msamehe mrudiane, upendo unamanisha kusimama namtu hata katika wakati ambao anajiona hafai na dunia imemtenga yaan kumpenda mtu nakumuamin hata katika wakat ambao anafanya jitihada za kuifanya dunia imuamin na impende.Nilishatimiza amri ya mapendo kwa kumsamehe, inatosha. Nilimpenda sana hilo siwezi kukataa ila machozi yangu yalifuta mapenzi yote niliyokuwa nayo kwake.
Zamani, kwahilo tu sina shida maana nisiposamehe nami sitasamehewa na Muumba wangu. Ilavkurudiana ndio mwikoNajua ulishamsamehe...
Kama huna mme olewa naye tu, maake ulivyokubali toba tu Mungu kamhesabia haki, maisha ndivyo yalivyo.Tulipendana sana, tukapanga mipango kedekede ya maisha yetu ya baadae na kuahidiana kila aina ya ahadi tamu tamu lakini yote hayo hakuyajali na kwa kuwa moyo wa mtu ni kichaka sikuweza kung'amua lolote mpaka siku ile ambayo sitakaa niisahau maishani mwangu!
Kama ilivyoada aliniaga kwa mabusu moto moto, nilijua ni moja kati ya safari zake za kibiashara, nilimwombea kila la heri huko aendako. Na safari ikaanza na kuniacha mwenye majonzi kwani nilijua nitamkosa kwa muda usiopungua wiki moja, kilichoniumiza zaidi ni kujua fika kuwa baada ya masaa yapatayo 12 nisingeweza kuwasiliana naye hata kwa simu maana aliniambia kuwa huko aendako ni maporini kusiko na network. Nilimwamini pasipo shaka. Naam baada ya masaa 12 sikuweza tena kumpata kwenye simu zake zote ila haikunipa shida kwani nililijua hilo.
Siku tatu baada ya kuondoka kwake, mida ya jioni nilishtushwa sana baada ya kupigiwa simu na rafiki yangu mmoja na kunipa pole kabla ya kuniuliza imekuwaje? Badala ya kumjibu nilimwuliza kwa wasiwasi mwingi, ananipa pole ya nini? Na imekuwaje nini? Jibu lake ndilo lilinifanya mpaka leo nisiisahau hiyo siku! Alicheka kwa kejeli kisha akanijibu ina maana hujui kama fulani(alitajajina la mpenzi wangu aliyesafiri siku 3 zilizopita) kanilipia mahali leo na kesho tunaenda kuandikisha ndoa kanisani? Sikusikia kingine alichokiongea bali nakumbuka mwangwi wa maneno yale yaliendelea kujirudia masikioni mwangu kwa masaa kadhaa kabla ya kulala (sina uhakika kama nililala au nilizimia)
Nilipoamka nilikuta simu ikiwa chini huku kioo cha simu kikiwa kimevunjika na betri ya simu imedondokea upande wake, nikajua kuwa baada ya taarifa zile nilidondosha simu pasipo kujijua.
Baada ya wiki moja mpenzi wangu alirudi kama alivyoniahidi akiwa na zawadi lukuki, nilizipokea na nilijaribu kuficha hali niliyokuwa nayo lakini aligundua kuwa sikuwa sawa akaniuliza nina tatizo gani nikamwambia ninaumwa na nimeshauriwa na daktari kupumzika muda mwingi. Alinionea huruma akataka alale kwangu ila nikamkatalia, nikamwambia nahitaji kuwa mwenyewe ili niweze kutumia muda mwingi kwa kulala. Alinielewa na akaondoka.
Sikuonana naye tena kwani kesho yake asubuhi na mapema nilisafiri kwenda mkoa mwingine na nilibadilisha namba ya simu. Tulionana tena siku ya harusi yake na rafiki yangu kipenzi, ilinibidi kwenda kanisani kushuhudia ndoa yao kama nilivyoshauriwa na mwanasaikolojia wangu. Aliniambia hiyo itanisaidia kuamini kuwa yule jamaa si wangu tena. Wakati wanatoka kanisani baada ya ndoa, nilihakikisha maharusi hao tunaonana ana kwa ana, kisha nikatokomea.
Haikuwa rahisi hata kidogo kuendelea na maisha ila kwa msaada wa ushauri wa mwanasaikolojia niliweza kuendelea na maisha japo ilinibidi kubadilisha mtindo wangu wa maisha.
Miezi 6 baada ya ndoa nilipata taarifa kuwa wanandoa wale walipata mtoto wa kiume, ila mtoto mwenyewe ni mwarabu wakati wazazi wake ni Wandengereko wenzangu. Hahahahaaaaa....nacheka kama mazuri mie. Wambea ikawa kutwa kucha wananilitea habari, ile ndoa si ndoa tena bali imegeuka ndoano baada ya kuzaliwa mtoto wa kiarabu. Nikasema pole yao, wavumilie tu maana kitanda hakizai haramu.
Juzi jamaa kanifuata anasema nimsamehe, yalopita si ndwele tugange yajayo. Ameachana na mkewe (rafiki yangu) kama niko tayari tukafunge ndoa ya bomani, niwe mkewe. Ametambua kuwa alifanya kosa kubwa sana kuniacha. Nimemwambia nilishamsamehe kitambo sina kinyongo nae hata kidogo ila "PEMA NI PEMA USIPOPEMA, UKIPEMA SIO PEMA TENA"!
Tafuta na wewe mnyonge.Sana, yasikie kwa mwenzio usiombe yakukute!
Dunia haijamtenga yeye tu ndo anajishtukia. Naamini mkewe bado ana mpenda kama kweli aliolewa naye kwa mapenzi.Nasemaje kama uko single msamehe mrudiane, upendo unamanisha kusimama namtu hata katika wakati ambao anajiona hafai na dunia imemtenga yaan kumpenda mtu nakumuamin hata katika wakat ambao anafanya jitihada za kuifanya dunia imuamin na impende.
Mbona unamshauri vibaya?? Mwenzio amelileta hapa ili kusudi atokee mtu amwambie arudi fasta.
Hilo haliwezekani, abaki na maisha yake mimi na yanguKama huna mme olewa naye tu, maake ulivyokubali toba tu Mungu kamhesabia haki, maisha ndivyo yalivyo.
Wa kumfanyaje?Tafuta na wewe mnyonge.
Mmhh sawaDunia haijamtenga yeye tu ndo anajishtukia. Naamini mkewe bado ana mpenda kama kweli aliolewa naye kwa mapenzi.
Nakuunga mkono kwa asilimia zote!Kuweka nadhir au kula yamini kwa mtu mweusi ni kujipotezea muda...sisi watu weusi sometime huwa nafikiria huenda Mungu alituumba kwa majaribio kabla hajaumba wanadamu kamili (wazungu)
Mambo tunayoyafanya si mambo ya kawaida!
Sent using Jamii Forums mobile app
Tafadhali usifanye hivyo, utamuumiza mwenzio. Yale maumivu hayamithiliki hata kidogo!Najiona nikifanya alichofanya huyo mshkaji soon