Bora ndugu yangu umeliona hilo, maana msukumo wangu kuanzisha mada hii ni kutokana na jinsi jukwaa la wakubwa lilivyopoteza maana kamili ya kinachotazamiwa na kubaki kama maonyesho ya ushoga na usagaji. Picha zinazowekwa hapo kwa wastaarabu wanakimbia haraka kwani tunachotazamia pale ni kubadilishana mawazo juu ya maisha ya ndoa au mahusiano ya ngono kwa kufuata mila na desturi za utamaduni wetu. Lakini kinachoendelea ni kuelimisha jamii ibadilike na kufanya yafanywayo na lesbians/gays.
Pamoja na kwamba kuna special ID ya kuingia huko, hii isiwe ndio kigezo cha kuwa na uhuru unaopitiliza. Huku tunasema ushoga mbaya na papo hapa huko jukwaa jingine tunawafunda watu namna ya kufanya ushoga kwa maneno na picha. Hii haija kaa sawa. Haya haya ndiyo tuliyoyalalamikia Ze-utamu yamerudi kwa mlango wa nyuma kwenye JF yetu.
Jukwaa la Wakubwa JF is too much! nasema hivyo kwasababu hata ulaya ambapo kuna haki zao hao gays and lesbians, bado huwezi kukuta kwenye public forum kama JF inawapa watu access ya kupost huu uchafu. Mimi mwenyewe nilitegemea Jukwaa la Wakubwa lingesaidia watu namna gani ndoa zao na namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za kufanya kuhusiana na maisha ya ngono lkn si katika hali iliyopo sasa kwenye hilo jukwaa.
Kwa ufupi jukwaa la wakubwa inanipa shida sana kuitembelea, hadi nalazimika kutafuta thread ambayo haionyeshi kwamba ina attachment, nikidhania kwamba huko kutakuwa namaelezo bora ya namna ya kufanya mambo ya wakubwa. Lkn cha ajabu, thread zingine hazionyeshi kwamba zina attachments lkn ukifungua tu unakutano na huo uchafu. Na jili jambo siyo zuri kabisa, kwani ukiona kitu cha ajabu hukaa kichwani muda mrefu kuliko kitu cha kawaida.
Ndugu yangu,
Mimi mpaka sasa kuna thread za watu sifungui hata kwa dawa, kwani ukifanya kosa na kufungua hakika utajuta. Kuna dada mmoja anaitwa Z...... na kaka mmoja anaitwa B........, ukifungua thread zao huko hakika hutakaa usahau uchafu wanaopost hapa JF hasa kwenye hili jukwaa la wakubwa.
Mimi kuna swali linanipa taabu,kwamba moderators hata wanapofanya evalutaion ya posts kwenye majukwaa tofauti, hivi hawaoni aina ya posts na aina fulani ya watu wakipost zenye huu mchezo kwa wingi, na hawajiulizi ni kwanini watu makini hawataki kuweka au kuchangia chochote kwenye hili jukwaa la wakubwa? Inauma kidogo na hasa mmoja wa moderator namfahamu vizuri sana na tumewahi kufanya naye kazi ofisi moja huyu mtani wangu, na ni mtu makini sana lkn nashangaa katika hili yeye na mods wengine wako kimya.
Niliwahi kusikia siku moja wakitetea kwamba watu makini wanapotembelea jukwaa hili wanakuwa na ID nyingine. Sasa swali la kuwauliza mods, je nini motives ya watu hawa kuingia hili jukwaa kwa ID ya siri? Je kuna mchango wowote wa maana kwenye jukwaa hili unaloweza kusema ni la watu makini kama ilivyo kwenye majukwaa mengine? Jibu ni moja tu, HAKUNA CHA MAANA ZAIDI YA UCHAFU unaopatikana kwenye hili jukwaa la wakubwa.
Hivyo basi mimi napendekeza jina jipya la hili jukwaa liwe
JUKWAA LA KUCHANGIA KUHARIBU MAADILI YA JAMII badala ya jukwaa la wakubwa. Nasema hivyo kwasababu,watafiti walio wengi duniani wanakubaliana katika jambo moja nalo ni kwamba hakuna kitu kisichokuwa na faida na hasara. Vitu vyote au jambo lolote lina faida na hasara zake. Na kitu kinaonekana ni mbaya pale HASARA zinapokuwa nyingi kuliko FAIDA , na kinyume chake ni sahihi. Sasa hili
Jukwaa la Wakubwa ukiangalia based on this theory, then utakubaliana na mimi kwamba HASARA NI NYINGI KULIKO FAIDA. Hii inamaanisha kwamba, Jukwaa la Wakubwa badala ya kujenga jamii sasa inabomoa jamii kwa kutaka kutahaminisha kwamba chochote kinachofanyika Ulaya au Marekani au Uarabuni ni sahihi sisi kuiga. Watu wanashindwa kujua kwamba mazingira na tamaduni za watu ni tofauti? na sisi waafrika na hasa watanzania kwa kushindwa kuliona hili ndiyo maana hatufanyi maendeleo, kwani tunaingiza tamaduni ambayzo kwayo hatuna msingi na si zetu, hivyo matokeo yake tunaishia kushindwa.
TELO.