Kwanini wapinzani wanapenda kutumia media za nje kuzungumzia mambo yetu ‘ya ndani’?

Hakika
 
Mkuu, vyombo vya ndani ndio vinawakimbia Wapinzani. Hata ilitokea wakafanya mahojiano maswali yao yanakuwa HAYAJASHIBA. Utakuta wanamhoji Mnyika kwa maswali yale yale wanayomhoji BABA LEVO, Au maswali wanayomuuliza SHILOLE watamuuliza Halima Mdee.
 
Labda TWITER ni ya ndani kwa kila nchi...

BTW, kwani media ipo limited kutangaza habari za nchi zilipo ofisi za medio husika..!? NINI MAANA YA BBC KTANGAZA KWA LUGHA YA KISWAHILI..!? Kwani media za Tanzania, hazina kipengere cha HABARI ZA NJE YA TANZANIA..!? Kwani watu wa huko nje ya Tanzania, huwa hawatumii media zilizopo Tanzania kusema ya kwao..!?

Binafsi, naona MTOA MADA HAJATUMIA AKILI YAKE KUFIKIRI NJE YA BOX..
 
Mkuu, vyombo vya ndani ndio vinawakimbia Wapinzani. Hata ilitokea wakafanya mahojiano maswali yao yanakuwa HAYAJASHIBA. Utakuta wanamhoji Mnyika kwa maswali yale yale wanayomhoji BABA LEVO, Au maswali wanayomuuliza SHILOLE watamuuliza Halima Mdee.
Na maswali yenyewe tanakaa kikada sana
 
Mexicana, siku hizi kila ndege ikitoka kwa Wazungu na kutua KIA, mh. Waziri wetu wa utalii anatupa taarifa ya idadi ya wazungu!! Wazungu ni wazuri kuliko ‘WAJUMBE’!
Jibu murua kabisa..!!! Watu hawafikirii kwa undani wanapotia hoja zao...
 
Wanadhani huko ndo kuna wapiga kura! Tutakachowafanya 28 October watakuja kusimulia!
 
Wananguvu sana govt ya ccm wakawafingie KTN
 
Bongo kuna media gani kama sio utopolo tu yani Very unprofessional kama ITV
 
Usi
Kama mnatumia fedha na silaha kuwalazimisha wanahabari wa Kibongo kurusha maneno ya jiwe huku mkiwakataza kurusha habari za kumwambia ukweli huyo jiwe unadhani tufanye nini kama si kutumia vuombo vya nje!
Usikwepeshe maneno waambie ukweli serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania haipendi kukosolewa na chombo chochote Cha Cha habari kitakachofanya hivyo kesi za kishamba au kubambikiziwa Kodi zitamhusu wao wanataka kusikia magufuli apokewa na mabilioni ya wananchi chato au CCM yavuna wanachadema milioni 700 katavi.
 
Media za ndani zinawaminya wapinzani...kila wakizungumza live matangazo yanakatwa ,
 
Hivi vya ndani haviwezi kutangaza vitapingwa fine na TCRA kwa kukiuka maadili ya uandishi.
 
Chombo chetu cha umma ni tbc, wanaopelekea kutumiwa kwa vyombo vya nje ni hawa ccm kukihodhi
Vyombo gani vimebana.....Lisu na Zitto jana walikuwa mubashara ITV au unazungumzia vyombo gani bwashee?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…