Kwanini watanzania hasa waliosomea Lugha wanashindwa kuchangamkia fursa za kazi za ualimu wa Kiswahili, Kiingereza na utafsiri wa lugha nchini Japan

wewe ndio unatakiwa uwe co-ordinator wa kuwaunganisha watanzania huko, tafuta sehemu huko wanaohitaji walimu wa kiswahili, njoo utupe details tu apply...

Haya mambo ya kugoogle mwenyewe bila ya kuwa na mtu wa uhakika wa kukuunganisha mwisho unaangukia kwa matapeli wa kinigeria
 
Hivi vijamaa vyenye macho madogo ni vichumia tumbo ...... havikupi dili kabisa badala yake vinakuja kukusanya coins zetu milioni 200
mkuu kuna fani ambazo kama umesoma mbogo huwezi kuzifanyia kazi huku ila sio kwenye lugha mkuu, wakenya na waganda nakuhakikishia wengi tulikuwa nao japan wanafundisha kiswahili na ngeli na watafsiri
 
Tafuta NGO ya KIjep au Kichina kama utaipata .....angalau Korea Kusini wana tabia za kusaidia watu wadogo......hawa wengine ni miradimikubwa iliyokaa kirushwa rushwa tu......nafikiri nao ni masikini kama sisi
 
😀😀😀We jamaa, wewe ni mmoja wa fani hizi?
 
Tafuta NGO ya KIjep au Kichina kama utaipata .....angalau Korea Kusini wana tabia za kusaidia watu wadogo......hawa wengine ni miradimikubwa iliyokaa kirushwa rushwa tu......nafikiri nao ni masikini kama sisi
mkuu mimi nazungumzia kwa huku kwao, achana na huko nyumbani
 
Mbona watanzania kibao wapo huko wanafundisha kiswahili?
 
Shida sio lugha ya kiswahili,shida in lugha ya kiingereza huwezi amini hapa bongo hata MTU mwenye PhD kizungu kinamsumbua just imagine

MTU first degree stela maris university
Masters:mzumbe university
PhD:udsm
Hiyo mtu hajapata exposure yeyote kwenye lugha ya kingereza(kuishi na native speakers) hivi unazan MTU kama huyo abakubalika kimataifa au kuweza kushawishika kufundisha hicho kiswahili huko Japan amezrzika na salary yake ya 1.2ml
Kusoma hizoo course za kiingerza sio mchezo ada sio chini ya 500000 za kibongo

Wakenya na waganda kiingerza kibawabeba sana kwwnye soko la ajira,kuna mwaka Fulani nlikuwa hong Kong wakenya na waganda wamejaa mbaya na wanapata kazi za ndani n house boy sababu tu anajua kiingereza so atatoa msaada mkubw kwa mtot wake

Kuliko umuajiri mbongo mwenye degree ya kubabaisha asiyejua kingerza vizur bora umuajir mkenya au mganda aliyeishia shule ya msingi akulelee mtoto wako

Changamoto nyingine hatujui wapi pa kuanzia,yan hutujui hata hiyo passport mtu hajui anaipataje yan?

Cha mwisho kabisa ni mtaji ,ujue ukiwaza kwenda hata hapo Malaysia bila dollar 1000 unakuwa deported, hebu waza.

Passport 200000/=
Visa dollor120
Flight ticket 670
Accommodation per day50$
Health insurance 154$/3 month

Kibongo bongo sio rahisi kuyamudu hayo yote ukitarajua kuwa ndii umemaliza chuo



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida sio lugha ya kiswahili,shida in lugha ya kiingereza huwezi amini hapa bongo hata MTU mwenye PhD kizungu kinamsumbua just imagine

MTU first degree stela maris university
Masters:mzumbe university
PhD:udsm...
mkuu nashukuru kwa kulithibitisha hili la uhitajiwa wa hawa watu kwenye hizi nchi na umekiri kabisa na wewe ushawahi kuzitembelea na umeona lakini umenishangaza kidogo, mtu unawezaje kuhitimu fani ya lugha na usijue kiingereza?
 
Tatizo wanasoma lugha halafu hawaijui lugha, huku bongo tunasubiri ajira za ndani tu. Ajira za nje wanaenda watoto waliosoma Internation au waliosoma nje ya nchi
 
Tatizo wanasoma lugha halafu hawaijui lugha, huku bongo tunasubiri ajira za ndani tu. Ajira za nje wanaenda watoto waliosoma Internation au waliosoma nje ya nchi
duuuh
 
Tuna kasumba hizi

1. Uvivu wa kusoma na kufutilia mambo mfano kwenye mitandao kuna fursa nyingi za ajira nje na free courses ila umakini na persistence ya kusoma all small details na kuapply hatuna. Kwa mfano uweke link hapo yenye page 7 tu bado mtu atauliza naomba nifanyie mchongo. Angalia hata mashirika ya kimataifa hapo Geneva watanzania ni wachache sana si kwamba hatuna elimu ila sijui elimu yetu imetulemaza hatu compete kivyetu vyetu sielewi.

2. Kuamini kuwa kila kazi ni connection: vijana wengi huamini hivi na kukata tamaa ya kusaka ajira nje

3. Fear of unknown. Yaani hujui unaogopa nini ila tunaogopa tu kwenda kufanya kazi mbali na nyumbani hatutaki mwenda nje ya comfort zone zetu.

4. Kubweteka na degree na masters zetu. Kuna course nyingi za soft skills zinazomuongezea mtu thamani mf presentation skills, team work, language etc ila tunabweteka na masters tunasahau kila mwaka thamani ya ulichosoma jana inapungua. Mfano fani ya Computer science huwezi kuwa umegraduate mwaka juzi ukasema umetosheka na programming languages za enzi zile lazima uwe unajinoa hapa na pale sasa vijana wa leo wanaringia vyeti na picha kubwa za graduation parties. Kumbuka pia interview za mashirika makubwa wana muassess mtu kwenye competencies nyingi haswa soft skills na upembuzi wake katika mambo kadha wa kadha nje ya fani yake.

5. Kutokuelekezana kwa waliofanikiwa. Mkuu nikupongeze kwa thread nzuri ila baadhi ya waliotoka na kufanikiwa hawatoi mrejesho chanya hata kuwapa moyo wadogo wajaribu. Kuna waliojaribu kufungua hadi blogs hao tunawapa sifa za jinsi ya kupata scholarships ila bado wengi wangeweza ku shed light kwa wenzao.

6. Kuogopa macho ya jamii. Katika jitihada hizi kijana anawaza dah sijui ntaonekanaje . Je nikifeli si ntachekwa na classmates wangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu nashukuru kwa kulithibitisha hili la uhitajiwa wa hawa watu kwenye hizi nchi na umekiri kabisa na wewe ushawahi kuzitembelea na umeona lakini umenishangaza kidogo, mtu unawezaje kuhitimu fani ya lugha na usijue kiingereza?
Parabola, mtu huku bongo anaisoma lugha ili afaulu apate cheti ili a graduate na kula mpunga na ndugu zake lakini muulize alichokisomea kama anaweza kukifanyia kazi

Huyo mwenye masters ya linguistics and translation, mpe page moja ya kwahili akutafsrie kwa kingereza utacheka ufe

Alafu umuambie akamfundushe lugha ya kiswahili mzungu?

Mzungu wa watu atakaa miaka kumi bila kuelewa anachikisoma

Ulishawahi kuskia kiingerza cha wazir wa elimu professor Joyce Ndalichako?

Na kwa kingereza kile sasa ndio amejionowa kwa kusoma Canada, jiulize je asingeenda kusoma huko angeongea nn na yule mchina?



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…