Kwanini watanzania hasa waliosomea Lugha wanashindwa kuchangamkia fursa za kazi za ualimu wa Kiswahili, Kiingereza na utafsiri wa lugha nchini Japan

😀😀😀 utakuwa hauko serious kabisa mkuu, mimi ndalichako nilimuacha akiwa katibu wa NECTA na wala sikuwahi kujua kama ni waziri wa elimu kwa sasa na hata sijawahi kumsikia popote akiongea
 
basi ni changamoto kama ni hivi, na tusikubali tu soko la pamoja la ajira la Africa mashariki maana wenzetu watatawala katika mashirika yote ya EA ni bora tubaki hivohivo kama hali ni hii
 
Huyo mwenye masters ya linguistics and translation, mpe page moja ya kwahili akutafsrie kwa kingereza utacheka ufe

Alafu umuambie akamfundushe lugha ya kiswahili mzungu?

Mzungu wa watu atakaa miaka kumi bila kuelewa anachikisoma

Ulishawahi kuskia kiingerza cha wazir wa elimu professor Joyce Ndalichako?

Na kwa kingereza kile sasa ndio amejionowa kwa kusoma Canada, jiulize je asingeenda kusoma huko angeongea nn na yule mchina?


😀😀😀😀 hahaha wewe mtu sio mzuri kabisa hahaha
 
Mkuu Asante kwa kwa thread nzuri binafsi nimefuatilia sana za China shida ni moja kama sio native speaker kupata kaZi kama sio native speaker ni shida hata visa huwez kupata nishafuatilia sana.Pili ukiwa Ngozi nyeusi hata ukipata inabidi uwambie wanafunzi unatoka either UK,US au Australia nk.Hata hao wakenya na waganda yawezekana wanafundisha bila kua na kibali jamaa wako strict sana hata Japan.Hapo tukomae na Kiswahili chetu tutatoboa.
 
Inawezekana waJp hawakuwataarifu wizara ya mambo ya nje, au wao wakalikalia hiyo fursa ili tukose wote?

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo linaweza kuwa kwa balozi wa Tanzania Japan pia,Anapaswa aangalie fursa kwa vijana wa kitanzania na ahakikishe vijana wengi kadri inavyowezekana wanazitumia.
 
Kwa kutumia kiswahili hutaweza kwenda Fanya kazi nchi yeyote labda kenya ukauze githeli!

Ili kiswahili kiwe na soko kwako lazima uwe competent kwenye lugha ya kiingereeza pia na hapo ndio pagumu

Ukiskia mtu yupo competency kwenye lugha inatakiwa awe na uelewa wa skills nne

Listening skills
Reading skills
Speaking skills and
Writing skills

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umesema ukweli kabisa
 
Tatizo linaweza kuwa kwa balozi wa Tanzania Japan pia,Anapaswa aangalie fursa kwa vijana wa kitanzania na ahakikishe vijana wengi kadri inavyowezekana wanazitumia.
Siyaelewi majukumu yao huwa nini ukiachana na masuala ya kidplomasia
 
Hili ngoja nilifuatilie
 
Tatzo ni mfumo wetu wa elimu, vyuo vinazalisha magalasa badala ya wataalam
 
Hizo skills ni za kawaida kaka inategemea tu msingi uliokua nao.Binafsi hizo skills ninaZimudu.Nina exposure ya kutosha na foreigners haswa kutoka USA.Sikatai kwa wabongo wengine.Mimi nilienda hadi BAKITA waniingize kwenye kanzi data yao nikaambiwa hata kama nilisoma Linguistics kama sikusoma Kiswahili Niko Illegible.So sometimes vikwazo vinaanzia home.
 
😳😳😳Mkuu hii unasema kweli?
 
Mkuu Asante kwa kwa thread nzuri binafsi nimefuatilia sana za China shida ni moja kama sio native speaker kupata kaZi kama sio native speaker ni shida hata visa huwez kupata nishafuatilia sana...
Mbona kuna profesa mmoja anaitwa mbele anafundisha kiswahili chuo kikubwa huko America, tusijidharau kwa rangi nafikiri kama uko vizuri unapata tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…