Tuna kasumba hizi
1. Uvivu wa kusoma na kufutilia mambo mfano kwenye mitandao kuna fursa nyingi za ajira nje na free courses ila umakini na persistence ya kusoma all small details na kuapply hatuna. Kwa mfano uweke link hapo yenye page 7 tu bado mtu atauliza naomba nifanyie mchongo. Angalia hata mashirika ya kimataifa hapo Geneva watanzania ni wachache sana si kwamba hatuna elimu ila sijui elimu yetu imetulemaza hatu compete kivyetu vyetu sielewi.
2. Kuamini kuwa kila kazi ni connection: vijana wengi huamini hivi na kukata tamaa ya kusaka ajira nje
3. Fear of unknown. Yaani hujui unaogopa nini ila tunaogopa tu kwenda kufanya kazi mbali na nyumbani hatutaki mwenda nje ya comfort zone zetu.
4. Kubweteka na degree na masters zetu. Kuna course nyingi za soft skills zinazomuongezea mtu thamani mf presentation skills, team work, language etc ila tunabweteka na masters tunasahau kila mwaka thamani ya ulichosoma jana inapungua. Mfano fani ya Computer science huwezi kuwa umegraduate mwaka juzi ukasema umetosheka na programming languages za enzi zile lazima uwe unajinoa hapa na pale sasa vijana wa leo wanaringia vyeti na picha kubwa za graduation parties. Kumbuka pia interview za mashirika makubwa wana muassess mtu kwenye competencies nyingi haswa soft skills na upembuzi wake katika mambo kadha wa kadha nje ya fani yake.
5. Kutokuelekezana kwa waliofanikiwa. Mkuu nikupongeze kwa thread nzuri ila baadhi ya waliotoka na kufanikiwa hawatoi mrejesho chanya hata kuwapa moyo wadogo wajaribu. Kuna waliojaribu kufungua hadi blogs hao tunawapa sifa za jinsi ya kupata scholarships ila bado wengi wangeweza ku shed light kwa wenzao.
6. Kuogopa macho ya jamii. Katika jitihada hizi kijana anawaza dah sijui ntaonekanaje . Je nikifeli si ntachekwa na classmates wangu.
Sent using
Jamii Forums mobile app