Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Yu wapi anayesema Tanzania ni maskini?

Salehe Mohamed
Feb 1, 2009
Tanzania Daima~Sauti ya watu

KWA takriban miezi miwili sasa tumeshuhudia mabilioni ya shilingi na mali zikitolewa kama dhamana wa watuhumiwa wa ufisadi katika kesi mbalimbali, zinazowakabili katika mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam.

Walianza watuhumiwa wa EPA, wakaja kina Mramba ambao nao waliweka dhamana ya mali zisizopungua sh bilioni moja na mwisho ni vigogo wa BoT kina Liyumba ambao wote kwa pamoja wameweka dhamana ya mali isiyopungua sh bilioni 110.

Tukitamaza kwa undani mali za watu hao ambao wengine walikuwa watumishi wa serikali tunaweza kupata picha halisi ya nchi masikini ya Tanzania tunayoizungumzia kila siku na kutembeza bakuli kwa wahisani tukiomba tupatiwe misaada.

Kama waziri mmoja anaweza kumiliki nyumba mbili za zaidi ya sh bilioni moja, anamiliki akaunti yenye zaidi ya bilioni moja nje, watendaji wengine nao wanawazidi mawaziri kwa kuwa na mali zenye thamani zaidi, huo umasikini tunaozungumzia uantoka wapi?

Tatizo tulilo nalo si umasikini bali ni uongo wa viongozi wa kutudanganya Watanzania kuwa nchi hii ni masikini, ili tuendelee kuwa na mawazo mgando na tukose ujasiri wa kuchunguza rasilimali tulizonazo zinatunusaisha vipi.

Viongozi wamekuwa wakitumia maneno matamu kuwa keki ya taifa ni ndogo au suungura mwenyewe ni mdogo hivyo si rahisi kwa wananchi wote kunufaika na rasilimali zilizopo. Kwa uongo huo wamefanikiwa, kwani asilimia kubwa ya Watanzania tunaamini nchi hii ni masikini, jambo linalowapa nafasi ya kuendelea kufanya ufisadi uliopindukia usio na chembe ya huruma wala aibu.

Sh bilioni 221 ni fedha nyingi sana kama zingetumika kujenga barabara, zahanati, hospitali, shule na huduma nyingine, lakini kwa bahati mbaya fedha hizo zimeingia katika mikono ya watendaji na viongozi wasio waaminifu ambao masilahi binafsi ndiyo kipaumbele chao cha kwanza.

Waziri anapoweka bilioni moja nje ya nchi, kumiliki shamba lenye ekari 40, magari zaidi ya sita, anasomesha watoto zake nje ya nchi, safari za mara kwa mara, tujiulize mali hizo kazipataje?

Anamiliki shamba ekari 40, kuwa na hisa zaidi ya asilimia 20 katika miradi na kampuni mbalimbali za ndani na nje ya nchi hapa nchini. Haya maswali yakijibiwa nina uhakika tutakuwa na mwelekeo mzuru kuhusu nchi yetu kuwa masikini au tajiri.

Tanzania ni nchi tajiri lakini utajiri huo umehodhiwa na watu wachache ambao wamepata elimu na madaraka kwa jasho la walalahoi na sasa wameamua kuwanyonga waliowapa madaraka na kuwagharamia elimu yao kwa kuwaibia fedha na rasilimali kwa tamaa za kujilimbikizia mali.

Ni aibu kwa nchi kuwa na watu wenye uhakika na milo na mambo ya starehe kwa zaidi ya miaka 100 ijayo, wakati kuna wananchi ambao hawana uhakika na mlo mmoja kwa siku na sehemu ya kuishi.

Uongo wa viongozi sasa unaanza kugundulika kwa kuwa mambo yote waliyoyafanya nyuma ya pazia sasa yanaanza kuwa hadharani ingawa mengine bado yanafichwa fichwa.

Sitanyamaza kukemea viongozi wanaoamini uongo ndiyo utakaowasaidia kuongoza nchi kwani nina imani ipo siku wananchi wataanza kuwapiga viongozi hao maana tayari kuna baadhi ya wananchi wameshaanza kuwaita viongozi waliomaliza muda wao kuwa ni mafisadi.

Nina hakika miaka inayokuja serikali itakuwa na wakati mgumu sana wa kuongoza kwa kuwa wananchi watakuwa wamechoshwa na umasikini unaozidi kushamiri siku hadi siku. Tanzanite, mbuga za wanyama, almasi, dhahabu, misitu ni miongoni mwa rasilimali ambazo zimeshindwa kutumiwa vizuri na Wtanzania na hivi sasa zimekabidhiwa mikononi kwa wageni kwa kigezo cha ‘uwekezaji’

Uwekezaji huu ndani yake una mikono ya viongozi na watendaji walafi ambao hujificha katika kivuli cha wageni, huku wakiendelea kula nchi yao huku wakijidai kuwalalamikia wawekezaji kwa kutafuna rasilimali za taifa bila kuwasaidia wazawa.

Leo hii maeneo mbalimbali yamebaki mashimo baada ya dhahabu au almasi kuchimbwa, lakini maisha ya wananchi yamebaki duni huku wakijisia kwa kujengewa vituo vya afya na vijumba visivyolingana na mali iliyovunwa na wawekezaji.

Baadhi ya viongozi tulionao hivi sasa hawapitishi mradi husika au kumkaribisha mwekezaji bila ya watu kukatiwa fedha (ten pasenti). Cha kusikitisha zaidi hata hiyo miradi wanayopewa wawekezaji hao bado ni mzigo kwa taifa, kwa kuwa baadhi yao husamehewa kodi lakini pia wakati mwingine pia serikali huchukua fedha za walipa kodi kuisaidia miradi inayolegalega.

Kampuni za kufua umeme za Richmond, IPTL na nyinginezo ambazo kila kukicha zilikuwa zikilipwa mamilioni ya fedha ni miongoni mwa uwekezaji wa kinyonyaji ambayo ni matunda ya rushwa waliyapewa watendaji wa serikali.

Sitanyamaza kuwaonya viongozi na watendaji kuacha matendo ya kifisadi kwani huklo tuendako tutakuja kuwapiga kiberiti kama tunavyofanya kwa wezi wanaoiba kuku huku mitaani kwetu. Wananchi watafikia hatua hiyo kwa kuwa tunaona kila mafisadi wanapofikishwa mahakamani ni kama vile mashindano ya nani anamiliki kiasi gani au mali zake zina thamani gani.

Mahakama ya Kisutu hivi sasa imekuwa ni sehemu ya kuwaumbua viongozi kwa mali walizozichuma, lakini pia sehemu ya kuwapa hasira wananchi hasa kwa kutambua uovu wa kujilimbikizia mali kunakofanywa na watu waliopewa dhamana ya kuzisimamia rasilimali za taifa.

Sitanyamaza kwa vile sitapenda kuona machafuko yanayotokana na wananchi baada ya kuchoshwa na vitendo vya kifisadi, ndiyo maana nimeamua kuwaonya mapema watendaji na viongozi wa serikali ili tuendako tusije tukalaumiana kama alivyosema Rais Jkaya Kikwete, alipokuwa akitoa hotuba ya kuuaga mwaka 2008 na kuukaribisha 2009.
 
Gharama za ufisadi

Ufisadi Twin Towers shilingi bilioni 221
Meremeta shilingi bilioni 155
EPA shilingi bilioni 133 (2005/2006)
Richmond shiling bilioni 172
Richmond shilingi bilioni 23
Rada shilingi bilioni 40
Jumla shilingi bilioni 744

http://www.raiamwema.co.tz/news.php?d=1141[/url]

Na hapa hatujaweka ufisadi wa ununuzi wa magari ya kifahari unaofanywa kila baada ya miaka miwili na gari moja linagharimu kati ya shilingi milioni 100 na milioni 150. Hatujaweka ufisadi uliofanywa kwenye ununuzi wa ndege ya Rais, magari na helicopters za jeshi. Hatujaweka ufisadi uliofanywa kuzifanyia matengenezo makubwa nyumba zote za serikali zilizouzwa kwa hasara kubwa kutokana na ufisadi huo.
 
Gharama za ufisadi

Ufisadi Twin Towers shilingi bilioni 221
Meremeta shilingi bilioni 155
EPA shilingi bilioni 133 (2005/2006)
Richmond shiling bilioni 172
Richmond shilingi bilioni 23
Rada shilingi bilioni 40
Jumla shilingi bilioni 744

http://www.raiamwema.co.tz/news.php?d=1141[/url]

Na hapa hatujaweka ufisadi wa ununuzi wa magari ya kifahari unaofanywa kila baada ya miaka miwili na gari moja linagharimu kati ya shilingi milioni 100 na milioni 150. Hatujaweka ufisadi uliofanywa kwenye ununuzi wa ndege ya Rais, magari na helicopters za jeshi. Hatujaweka ufisadi uliofanywa kuzifanyia matengenezo makubwa nyumba zote za serikali zilizouzwa kwa hasara kubwa kutokana na ufisadi huo.

Yaani kwa data hizo, mikoa yote ya Tanzania ingewezwa kuunganisha kwa barabara za lami na ile ndoto ya Magufuli ya kutumia taxi kutoka Mwanza hadi Mtwara ingewezekana kabisa na matumizi ya ununuzi wa mashangingi -GX na VX na mafuta na spea zake yasingekuwepo.

Kwa kweli Tanzania si masikini hata kidogo ila Viongozi wetu wengi ndiyo masikini wa akili (Mungu aturehemu).
 
Kama tungekuwa na rais anayethubutu na serikali inayofanya kazi (responsively), nadhani njia rahisi ingekuwa ni kutaifisha mali zote za mafisadi halafu wao ndio waende mahakamani kutushitaki. Kwa kufanya hivyo serikali ingekuwa imekosea?
 
Tanzania tunahitaji sheria maalumu kuwashughulikia hawa watu katika misingi yenye usawa...kama vile Iraq walivyofanya walipomkamata Saddam na wenzie. Si mahakama, waendesha mashitaka wala takukuru yetu wenye uwezo wa kusimamia hizi kesi kikamilifu. Watu wenye dhamana ya mali zetu BoT ghafla wanakuwa na bilioni 100; sio wenzetu kabisa hawa..!!!

Kuna haja wa kuomba msaada kwa wenzetu wa China.
 
Wiz mtwup ni bora muungano uvunjike .maana joto la Tanganyika inavyoibiwa na wajanja wachache linahisiwa mpaka Zanzibar na wamesema bora tujikate maana wanaona jamaa wameshaanza kuwacha mashimo mikoani sasa wanakodolea macho mafuta ya Zanzibar ili waje kuacha mapango matupu.
 
Kutokana na kufuatiliwa kwa mambo yote haya ndipo napoinua mkono wangu na kumpa support Kikwete...Ni ktk utawala wake mambo yote haya yamekuwa wazi na tunaendelea na libeneke..Hata kama hatamaliza utekelezaji wake lakini mwanzo huu utamwezesha atakayekuja kumalizia ngwe hii!
 
Swala hapa ni je hawa ndugu walipata hizi mali kihalali au walipora toka kwa watu maskini?

Hakuna dhambi kubwa kama kumwibia mtu aliye maskini ndugu zangu!
 
Ukijumlisha zote hizo zilizoibiwa, bado ni kiduchu kwa nchi yenye watu zaidi ya milioni 35! Bado tu masikini. Tupende, tusipende.
 
hawa watu ni na kuwanyang'anya kila kitu na kuwafungulia mashamba ya ujamaa, walime huku nyimbo za propaganda za kikomunisti zinapigwa pembeni.bila kwenda mahakamani ! tuwahukumu kwa kura za maoni, some sort of truth commision, kwa sababu hata huyo Mwankenja sasa atakuwa taabani na mikesi yote hii.
 
Hawa wanatakiwa kufirisiwa mali zao zote pamoja na pesa kwenye account zao,na wangetakiwa wasipewe zamana, na inatakiwa wasimamishwe shughuli zote za serikali tena wafukuzwe kabisa hata kazi za ubunge,ndivyo wanavyofanya wenzetu huku Ethiopia,kwa miaka mitatu sasa wapo mawaziri wanasota kwa tuhuma kama hizi.
 
Tungeiba bila ushirikiano wenu? Ni nani anayetupigia kura kutupeleka kwenye asali?

Lakini umesahau maneno ya baba wa taifa. Ngoja nikukumbushe:-

  1. Someni wakati ni huu
  2. Elimu ni dhamana.
  3. Anayepewa elimu ni sawa na mtu anayetumwa na kijiji chake kutafuta chakula wakati wa njaa.

Mnachofanya sasa ni aibu tupu.
 
Lakini umesahau maneno ya baba wa taifa. Ngoja nikukumbushe:-

  1. Someni wakati ni huu
  2. Elimu ni dhamana.
  3. Anayepewa elimu ni sawa na mtu anayetumwa na kijiji chake kutafuta chakula wakati wa njaa.

Mnachofanya sasa ni aibu tupu.

Wapi aliposema kuwa chakula hicho tukigawe bure au tusianze kuonja wenyewe?
 
Swala hapa ni je hawa ndugu walipata hizi mali kihalali au walipora toka kwa watu maskini?

Hakuna dhambi kubwa kama kumwibia mtu aliye maskini ndugu zangu!

Kama ni halali watuonyeshe jinsi wanavyolipa kodi (Taxi returns). Vingenvyo hizi mali zinatakiwa kuchukuliwa na umma kilaini ili wao waende mahakamani ambako kila kitu kitajulikana kama kweli ni zao.
 
Kama wodi hii ilijengwa kimakosa, nani aliyeidhinisha ujenzi wake miaka 2 iliyopita??? Kwa nini waibomoe badala ya kubadili matumizi?????

Kuna nini hapa??? soma habari hii

Serikali yavunja wodi ya Raza Z'bar

Tuesday, 05 May 2009

Na Said Mwishehe

HATUA ya kuvunjwa jengo la wodi ya wazazi ya Hospitali ya Kivunge iliyoko Mkoa wa Kaskazini 'A' Unguja imezua mtafaruku mkubwa huku baadhi ya wadau wakidai kuwa jambo hilo limefanywa kwa fitna .

Akizungumza na Majira jana, mfadhili aliyejenga wodi hiyo, Bw. Mohamed Raza, alidai kitendo cha kuvunja wodi hiyo si cha kiungwana na kina lengo la kudhoofisha maendeleo ya Zanzibar.


Alisema alijitolea kujenga wodi hiyo kutokana na matatizo makubwa yaliyowakabili wanawake wa Mkoa wa Kaskazini A ambayo yalichangia ongezeko kubwa la vifo vya watoto na wajawazito. Ujenzi huo ulianza Februari 19 , 2007 na kukamilika Julai 18, 2007 mwaka huo.


Alisema kabla ya hapo, wajawazito hospitalini hapo walilazimika kuchangia kitanda kimoja watu wawili hadi watatu, hali iliyoleta mateso makubwa kwa wanawake hao.


Tatizo hilo lilikera Kamati ya Maendeleo Visiwani humo inayoongozwa na Mzee Ali Hassan Mwinyi na kuchukua hatua kadhaa kunusuru jambo hilo ambapo, Bw. Raza alijitolea kujenga wodi hiyo.


"Wodi hiyo iliyokuwa na vitanda 10, chumba cha kujifungua na huduma zingine zote , ujenzi wake uligharimu jumla ya sh. milioni 20 ilisadia kwa kiasi kikubwa wanawake wa Mkoa wa Kaskazini 'A' alisema Bw. Raza.


Alisema Mei mosi mwaka huu alipewa taarifa kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya, imevunja jengo lote la wodi hiyo.


"Nilishtuka sukari na presha vikapanda kutokana na ujumbe nilioambiwa. Siku iliyofuata nilizuru hospitali hiyo na kuhakikisha jambo hilo. Nilikuta jengo nililojenga limebomolewa."


Alisisitiza kuwa hatua hiyo si sahihi kwani imechangia kurudisha nyuma jitihada za kuboresha sekta ya afya visiwani humo.


Alisema kama wizara iliona jengo hilo ni dogo hapakuwa na sababu kulibomoa kwani bado kuna maeneo ya kutosha hospitalini hapo, wangeweza kujenga sehemu nyingine bila kufanya uharibifu huo.


Alidai hatua hiyo imefanywa kibabe na kamwe maamuzi ya namna hiyo hayajengi nchi bali yanarudisha nyuma maendeleo ya watu wa Zanzibar.


Alisema kitendo hicho kamwe hakitamvunja moyo wa kujitolea kuchangia maendeleo na ataendelea kujitolea kwa hali na mali bila kujali jinsia rangi wala itikadi.


" Maana ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuwaletea watu maendeleo, leo tunakwenda kuvunja hospitali bila kuwepo sababu za msingi! Wanawaonea wananchi masikini wa mashambani, kwasababu wao hawategemea kupata huduma hapo" alidai Bw. Raza.


Alisema aliamua kujitolea kujenga wodi hiyo kwa heshima ya Rais mstaafu wa Zanzibar, Dkt Salamin Amour anayetoka eneo hilo na pia njia ya kuonesha kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Kamati ya Maendeleo ya Zanzibar katika kueleta maendeleo.


Majira lilipozungumza kwa njia ya simu na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Bw. Sultan Mugheiry kujua undani wa jambo hilo, alisema wanazo taarifa hizo na wanatarajia kutoa ufafanuzi kamili leo.


Sosi:
Majira
 
Ndugu zangu kumekuwa na maswali mengi sana kwa waumini mbalimbali...makanisa mengi hayawaweki watu wazi jinsi gai ya kubarikiwa badala yake wanaelimisha sana kuhusu matoleo.......
yaaah unaweza kutoa sadaka nyiiingi kupita kiasi na zaka nyingi na kila siku mchungaji akawa anakutembelea nyumbani kwako kwa ajili tya heshima za zako .....lakini tujiulize kwa nini makanisa mengi ya watu wa mungu watu hawabarikiwi.....yaani unakuta idadi ya masikini ni kubwa kliko matajiri...si mapenzi ya mungu kuwa masikini ila leo hii napenda kukuelekeza njia za kubarikiwa hata kabla ya kukimbilia kutoa zaka na dhabihu.

1)))Hakikisha maisha yako yako safi..yaani unafwata yale mwenyezi mungu anayotutaka kuyafanya....yawezekana unatumia njia zisizo sahihi katika kutafuta pesa...hapo ndipo unapopishana na neno la mungu...jaribu kuangalia wapi umekosea...ndio maana unaweza kuta mtumishi anatoa kupita m,chezo lakini kila akirudi nyumbani..ugomvi mtupu na mkewe matokeo baba analala juu gorofani mama anaamua kulala ground floor
haya yote ni kwa ajili ya kumkosea mungu....tujaribu kubadilika na kutenda yanayompendeza ndipo tukatoe sadaka na dhabihu..

2))Lazima uokoke...hilo halina ubishi kwamba wokovu ni lazima ,na napenda kurejea tena leo kwamba BIBLIA inaweka wazi kwamba BAADA YA KIFO HUKUMU.....hakuna sehemu iliyoandikwa ukifa unanafasi nyinge ya kuomba msamaha ama kuomba uokoke..biblia iko wazi wakati wa wokovu ni sasa...
hakuna haja ya kupoteza muda wewe unaesoma leo hii amua kutoka moyoni mwako mrudie bwana yesu....mfwate akuokoe kama bwana na mokozi wa maisha yako kumbuka yule alietoa sadaka sana yesu akamwambia pamoja na kunitolea sadaka umeoksa kitu kimoja nacho ni wokovu..hivyo pasipo kuwa na wokovu utahudhuria kanisani mpaka soli iachie hakuna kubarikiwa\

3))Mwambie mungu akutendee kitu kwenye dhabihu yako/sadka/zaka
ndio maana nilikuwa na sisitiza katika mada moja kwamba watumishi wa mungu wanaitaji ufahamu wa mungu zaidi ili waweze kuwaombea washarika wapate ufahamu wa mungu ili wakombolewe.....ukombozi ukishatoke\a then hata umuhimu wa sadaka zaka nk utaujua tu...again ukiwa unatoa dhabihu mlilie mungu mwambie mungu kwa dhabihu hii mungu nakutolea leo hiinakuomba

1))NIPATIE MUME/MKE ANAETOKA KWAKO

2))NAITAJI AFYA NJEMA KWANGU NA WAZAZI WANGU/FAMILIA NK

3))NAITAJI HALI NZURI YA KIUCHUMI,KIFEDHA NIACHE KUAIBIKA...ANGALIA MUNGU NIKICHOKA MBAYA NAAIIBIKA JE UNAKUBALI KUAIBIKA...SEMA NA MUNGU WAKO USIMWOGOPE ANASEMA NJOONI TUSEMEZANE ASEMA BWANA WA MAJESHI...

4)IN GENERAL TAJA MAHITAJI YAKO YOTE UNAYOITAJI MUNGU AKUSAIDIE...SWALA SI KUTOA TU SADAKA/ZAKA/DHABIHU MWAMBIE MUNGU HITAJI LAKO NDIPO UTAKAPOBARIKIWA...KUMBUKA ZAKA NI KWA YALE MUNGU ALIOKUPA..SASA KAMA HUTOMWAMBIA MUNGU KWA ZAKA HII NAOMBA NIONGEZEE WATEJA KWENYE BIASHARA YANGU..NK...UTASHANGAA UNABAKI HAPO HAPO MWISHO WA MWEZI UNAKOSA CHA KUTOA NA KUISHIA KUSEMA MUNGU AMENIACHA...WAPIIIIII WEWE MUNGU AJAKUACHA WEWE MWENYEWE UMEJIACHIA.......RUDI KWENYE MISINGI YA UTOAJI...

baada ya hapo na hayo yote na mengineyo ambayo ama kwa ufahamu wangu sijayatambua naomba wenye ufahamu zaidi tuongezee ekuelimishana zaidi ili tupate baraka za bwana

SI MAPENZI YA MUNGU WANA JF KUISHI NA MAISHA YA KIMASKINI
NI HAKI YETU KUMUULIZA MUNGU NITOKE VIPI.....

MUNGU AWABARIKI

WENU

SHALLOM
 
Sasa hiyo namba mbili si utakuwa unapimga kile kifo cha msalabani au sijakufahamu vizuri?
 
Sasa hiyo namba mbili si utakuwa unapimga kile kifo cha msalabani au sijakufahamu vizuri?

Mkuu sidhani kama vinapingana. Lengo la kifo pale msalabani ni ukombozi wa mwanadamu. Hatahivyo kifo kile hakitupi ruksa ya kutenda dhambi au kutufanya tuendelee kutenda dhambi kwa kuwa tumekombolewa la hasha. Ni kwamba, ukombozi upo kwa yule atakaye mpokea Kristo katika maisha yake kwani kabla ya kile kifo tulikuwa tumetengwa na uso wa Bwana.
 
Back
Top Bottom