jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,329
- 25,263
Gamba,
Ukiangalia staili ya wasomi kujipatia mali (rich, wealth0 ni kupitia kalamu na njia nyepesi. hakuna watu wenye kutaka kupitia njia ngumu kujenga mali kwa kutumia natural resourceskama kina Ford, Rockefeller na koo tajiri nyingine zilizofanya duniani.
Sisi tunataka ule utajiri wa ma CEO, wa mishahara mikubwa na marupurupu, lakini hata kufanya kazi kwa juhudi na maarifa kutumia rasilimali tulizonazo ili kuongeza mapato ya kampuni au shirika ili kuhakikisha mishahara yetuinaongezeka marudufu hatutaki.
Tanzania tuna neema ya kuwa na rasilimali nyingi. Ni juhudi na maarifa yetu wenyewe ndizo zitakazotupa uwezo wa kuwa Taifa linalojitegemea na lenye utajiri wa kutosha kutoa huduma.
Sisi tunakimbilia kutafuta wageni wafanye hiyo kazi ya kuzalisha hizo mali asili na rasilimali tukisubiri kupata utajiri kwa kukata kodi na kupokea mishahara!
Reverand umemsahau na Carnegie kwenye listi! Ambaye kwa asili alikuwa masikini na akaanzisha ile "Carnegie Foundation"
Kihistoria hawa watu walipata u zillionea wao kwa ufisadi hapa marekani wakati ule wa "The gilded Age"
Age ambayo ni similar na hii tunayoipitia sasa hivi ya Ubinafsishaji nk!
Mafisadi wa kimarekani enzi hizo walitake advantage kama mafisadi wetu wanavyofanya nchini mwetu!
Lakini wananchi wa Marekani walipowajia juu wakageuka kuwa "Philanthropists"
Kwa maana nyingine wakaamua kutumia utajiri wao kwa kujitolea kuijenga marekani!
Hiyo ni kwenye "progressive era".....Ndani ya US history wakati wa kina Woodrow Wilson na Roosevelt. Wilson tunamkumbuka pia kwa zile "14 points"
Era ambayo wamarekani walichoshwa na ufisadi na kuamua kufanya mabadiliko makubwa!
Mafisadi wali igeuza mioyo yao na kuamua kuwatumikia wananchi kwa mali waliyowaibia!
Carnegie alijitolea pesa zake zote zilizokuwa ni nyingi kupindukia!
Akasema zitumike kwenye kila kitu mpaka utoaji wa scholarships!
Wakaijenga marekani...Kuanzia barabara, Hospitali, mashirika kama vile YMCA ndiyo mafisadi waliyaanzisha kuwasaidia masikini!
Haki za wafanyakazi, mazingira bora ya kazi, haki za wanawake kupiga kura, sheria za vyakula, sheria za kuwabana viongozi mafisadi!
Listi ni kubwa!
Kwa kifupi watu hao waliokuwa mafisadi na wanyonyaji ndio waliogeuka na walioijenga marekani tunayoiona kwa kiasi kikubwa mno!
Wakaugeuza ufisadi kuwa something positive!
Hapa ndio tumekwama kwasababu viongozi wetu hawakubali kuwa kuna ufisadi!
Haya ni matatizo ambayo waafrika tumeshindwa kujifunza kutokana na historia ya dunia na hivyo mara nyingi ku resort kwenye mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kama wanavyoelekea kutaka kufanya watuhumiwa wa ufisadi!
Na ndio maana pia nika suggest wakamatwe kabla ya kufanya hivyo!
Waigeuze mioyo yao na watubu ili tulijenge taifa jipya badala ya kuanza umwagaji damu!