Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Ukitaka kupima ubora wa kitu ni lazima utumie namba. Hiyo namba inaweza kuwa ya kufikilika au makadirio ya kweli.

Tanzania ni nchi masikini, end of story, period, finito, konec. Hakuna discussion ya kusema kuwa sisi ni tajiri kwa sababu namba zote zinazotumika kuelezea utajiri zinaonyesha kuwa sisi ni masikini.

Pamoja na umasikini wetu, Tanzania ina potential ya kuwa nchi tajiri. Na hii potential yetu ndio inayowafanya watu kufikiri sisi kuwa tajiri.
 
Na Afrika kwa ujumla je? Maana hali ya Tanzania haiko tofauti sana na nchi zingine barani Afrika. Karibu Afrika nzima iko ulimwengu wa tatu. Afrika Kusini imeendelea zaidi kushinda nchi nyingine, je ina maana yenyewe ni nchi tajiri (kirasilimali) na ina uongozi mzuri kushinda nchi zingine za Afrika?

Swali jingine la kujiuliza, je ni kipi muhimu kuwa nacho, utajiri wa rasilimali pamoja na uongozi mzuri au kinachohitajika ni uongozi mzuri tu na mengine yatajipa yenyewe?

Nauliza hivyo kwa sababu wakati mwingine nashindwa kabisa kuelewa ninapoangalia nchi kama Japan (the second largest economy) na maendeleo waliyonayo ukizingatia historia (II WW) na rasilimali walizonazo. Juzi nilikuwa naangalia documentary fulani hivi iliyokuwa inaelezea maendeleo ya Japan ktk miaka 30-40 iliyopita. It's remarkable what they have done given their meager (meagre) natural resources.
 
mnakumbuka tulipokuwa darasa la kwanza au la pili tulikuwa tukiimba hivi:

Tanzania, Tanzania
nchi yenye mali nyingi
watu wengi wa ulaya wanaililia sana

niliona ndege wengi
chini wanatia fora
wanapendeza mlio kama mtoto wa nyumbani

my take:
jamani hivi ni kweli watu wengi wa ulaya wanaililia sana Tanzania , au watu wengi wa Tanzania wanaililia Ulaya.

pengine mafunzo haya ya toka elimu ya msingi ndo yamepelekea watu kuwa na mitizamo inayokinzana kuhusu mali zenyewe , je hizo mali ni wealth au ni natural resources?
 
Hilo la wazungu kuililia Tanzania ni kweli kabisa. Nimeshawahi kufanya kazi na wazungu toka Denmark na Sweden ambao walikuwa wanakuja Tanzania kwa mikataba ya miaka miwili na kuruhusiwa kuongeza mara moja mkataba wa miaka miwili mingine.

Wote waliokuwa wanakuja walikuwa wanaongeza mkataba kwa miaka miwili mingine na wote walikuwa wanataka waruhusiwe kuendelea kuishi Tanzania pamoja na sheria za mikataba yao ilikuwa hairuhusu hivyo. Wengine walikuwa wanaangusha mchozi kwa kuwa walikuwa wanaondoka Tanzania. Kilichokuwa kinatushangaza wengi tuliofanya kazi na wazungu wao ni kwamba nchi zote hizo ni matajiri na kiwango cha maisha ni cha juu mno kuliko hata cha Marekani, lakini bado walikuwa wanapenda kuendelea kuishi Tanzania.

Miaka ya karibuni nimekutana na wamarekani, waingereza, wacanada wanaoishi Tanzania ambao wanadai wao ndio wameshafika katika nchi ambayo wanataka kuishi for the rest of their lives, hawataki kabisa kurudi makwao, wanaenda makwao kutembea tu. Hivyo basi hilo la wazungu kuililia Tanzania ni la kweli kabisa
 
Bubu:

Uliyosema ni kweli kabisa. Lakini ukweli ni kuwa wao wanalipwa kwa pesa za kwao na maisha ya Tanzania ni cheap sana hivyo wakija kufanya kazi Tanzania kwa kiwango kikubwa wa-save matumizi mengi.
 
mnakumbuka tulipokuwa darasa la kwanza au la pili tulikuwa tukiimba hivi:

Tanzania, Tanzania
nchi yenye mali nyingi
watu wengi wa ulaya wanaililia sana

niliona ndege wengi
chini wanatia fora
wanapendeza mlio kama mtoto wa nyumbani

my take:
jamani hivi ni kweli watu wengi wa ulaya wanaililia sana Tanzania , au watu wengi wa Tanzania wanaililia Ulaya.

pengine mafunzo haya ya toka elimu ya msingi ndo yamepelekea watu kuwa na mitizamo inayokinzana kuhusu mali zenyewe , je hizo mali ni wealth au ni natural resources?
Na suggest the answer is both kwenye highlighted!

Swali ni why?

Je nia za both wanaolilia ulaya vs wale wanaolilia Tanzania ni sawa?

What about the benefits?

Kwenye second paragraph umenichanganya kidogo kwasababu unauliza "je mali ni wealth au ni natural resources?"

Jibu ni BOTH..Wealth as well as Natural resources.

Hapo kwenye "mali ni wealth", Jibu ni mali=wealth..just different languages!
 
Nadhani tofauti kubwa ya misemo yote hii miwili ilikuwa ni ktk tofauti za ARDHI na WATU..
Mheshimiwa rasi alikuwa akizungumzia WATU hali Mengi na Dr. Slaa walikuwa wakizungumzia ARDHI... sasa swala la kujiuliza kinachounda Tanzania ni ARDHI ama WATU!...
Kwenye highlighted..

My take;

Tanzania inaundwa na BOTH ARDHI(with all its geographical features and lawful boundaries) na WATU!

Swali ni je Mh Rais,Dk Slaa pamoja na Mengi wametofautiana ki meaning ama ni kimawazo na kimtizamo?

Are you sure wanazungumzia vitu viwili tofauti?

Kumbuka hizi kauli zimetolewa kimtiririko wa kujibizana!

Na ndio maana tunazijadili hapa jf.
 
Hakuna haja ya kuimba umaskini bila kuchukua hatua. Mengi aliona hiyo nafasi na kapambana kadri inavyowezekana kujiletea maendeleo yeye mwenyewe na jamii ya Tanzania.

Sasa ni wajibu wa Watanzania wengine pia kuiga mifano ya akina Mengi.
Sio tu kuiga mfano..Bali pia kuchagua viongozi wenye fikra kama hizo!
 
Topiki tamu kweli kweli!

Baada ya Mwalimu, Watanzania tumekuwa masikini wa fikra. Tumeshindwa kutumia mali iliyotuzunguka kujitajirisha. Mfano: Mtanzania anakubali hongo ya Tshs. 500,000/= kuruhusu mgeni kuiba Tshs. 5,000,000,000/= ambayo ni mali ya Mtanzania kwa namna moja ama nyingine. Nasema baada ya Mwalimu kwa kuwa yeye aliamua kutoigusa!

Dr. Slaa na Mengi wako right, lakini wageni hawapori bali tunawapa kwa upumbavu wetu!
 
Tanzani ni nchi tajiri yenye watu masikini. Inajumuisha kauli zote za watu watatu Kikwete, Slaa na Mengi?
Mh Zitto..Did you mean kuwa kauli zote za Kikwete,Slaa na Mengi zinamaanisha "Tanzania ni nchi tajiri yenye watu masikini" ama ulikuwa unauliza if kauli zote kutoka kwao zina maana sawa?
 
Jmushi1,

Statements zote ni sahihi, Tanzania na Afrika kwa ujumla ni tajiri kwa maana ya resources kama ardhi, madini, mafuta nk. Lakini watu wake ni maskini kwasababu tumeshindwa kutumia akili zetu kutengeneza added values kutoka kwenye hizo resources zetu.

Umaskini uko kwenye vichwa vyetu, akili zetu, fikra zetu nk. Hata tukipata uongozi bora sana bado itachukua miaka mingi kwa Watanzania kuwa matajiri. Ni rahisi kubadili uongozi lakini ni ngumu sana kubadili culture ya uvivu
na kutokuwajibika ambayo imejengeka Tanzania na Afrika. Sisemi Waafrika ni wavivu, maana wakija huku nje wanajituma kweli kweli.

Culture yetu ndio ya kimaskini, culture ya kukimbilia majibu rahisi na common sense. Culture ambayo haitufanyi tukae chini na kuwaza nje ya our comfort zone. Kuibadili hii itatuchukua muda mrefu sana na juhudi kubwa mno kuanzia level ya individuals mpaka kwenye viongozi wa nchi.

Ndio viongozi wa Afrika wameiba mabilioni ya resources zetu lakini mimi siamini kama ndio chanzo cha umaskini wetu. Matatizo yetu yanaenda ndani zaidi. Mwalimu Nyerere alijaribu kushughulikia kiini cha matatizo ya Watanzania lakini bahati mbaya akachagua siasa mbaya na chama kushika hatamu mpaka ikafikia mahali ambapo hakuwa challenged na hivyo kudumaa kama viongozi wetu wengine.

Nimekubaliana na mengi hapo juu, upanuzi mzuri walakini...

nabaki kujiuliza -Tunaweza kujikwamua vipi na hii culture
 
Nimekubaliana na mengi hapo juu, upanuzi mzuri walakini...

nabaki kujiuliza -Tunaweza kujikwamua vipi na hii culture
Tujikwamue?
Kivipi ilhali Mh Rais mwenyewe anatuimbisha kuwa sisi ni masikini?
Naomba ufafanuzi tafadhali!
 
Mimi nafikiri huu mjadala wapelekewe wananchi pia ili waulizwe na wao wanafikiri vipi:

1)Rais yuko right kuwa "Tanzania ni masikini" Na ndio maana hatuna pesa za kujenga miundo mbinu.

2)Rais yuko wrong

3)Mh Dk Slaa na R.Mengi wako right.(Slaa anayedai kama Tz ni masikini kwanini wanakuja kuwekeza na R.Mengi anayeamini kabisa kuwa sisi ni matajiri)

4)Wote hapo juu wako wrong

5)Wote hapo juu wako right

Na mwisho sababu za jibu lolote hapo juu!(1-5)

Ama kama wanatofautiana tu kimtizamo
 
``
Hakuna sababu wizara, TANROADS kumchagua mtu mwenye hesabu ndogo, mnapotangaza tenda lazima kuangalia kama kazi ataiweza, ingawa wale watakaokosa watasema mnajali mafisadi,... hayo msiyajali?,`` alishauri.
Kauli ya mh Rais the same day akisema kuwa sisi ni masikini huku akishauri gharama zisipewe kipaumbele bila kujali kama upandishaji gharama huo utamnufaisha mkandarasi ama utainufaisha kazi/tenda na kuona kama gharama zinaendana na quality ya kazi pamoja na mazingira ya utoaji wa tenda hizo!

Ufujaji ufujaji ufujaji...then he turns around and say it loud!

Tanzania ni masikini?!
 
Je Mh Rais alijisahau na kufikiri kuwa anaongea na wafadhili na wala si watanzania?

Kipi ni kipi jamani?

Ama mh Rais firmly wants us to believe that we're poor!?

Maswali ni Mengi kweli kweli!

Nakumbuka hili suala alisha lisema balozi wa Sweden Tanzania, kuwa jamani akilinganisha mali walizonazo Tanzania na Sweden Tanzania ina laslimali za kutosha.

Lakini vile vile Sweden yenye mali kidogo bado inaendelea kuisupport Tanzania.

Kwa hiyo unaweza kuona jinsi hata na watu walioko kwenye diplomasia wanavyoona jinsi tulivyo matajiri.

Tatizo kubwa la Taifa letu ni uongozi mbovu, sheria mbovu zilizokaa kinadhalia kuliko vitendo, Rushwa(ambayo inachochewa na uongozi tulionao).

Haya yote ndiyo yanarudisha maendeleo ya mtanzania nyuma hivyo kuitwa masikini.

Suala la Jk kusema hivyo nafikiri tuna kiongozi aliyekuwa anajua fika matatizo ya wananchi mara tu alipopata madaraka akasahau.

JK alisha ulizwa kwa nini nchi yako ni masikini? Angeulizwa swali hili kabla ya kuwa mkuu wa kaya angemwaga data za kutosha lakini tangia awe president hata suala dogo kama hili linamshinda.

Sishangai maana yeye sasa ni mdau katika kuwafanya watanzania masikini.
 
Sasa kama Rais wetu anasema sisi ni masikini..ina maana akikutana na hao wawekezaji anawaomba msaada/anawataka waje kuwekeza kwenye utajiri ama anawaambia kuwa sisi ni masikini hivyo msije?

Tunajua anatakiwa awaambie kuwa sisi ni matajiri hivyo tunataka namna ya kutuwezesha kunufaika na utajiri wetu!

Sasa huyu ni Mh Rais anayeweza kubargain kwa niaba ya Watanzania kweli?

No wonder nchi imeshauzwa kwasababu wale wanaoiuza wanaamini ni masikini na haifai!

Hao ndio viongozi wetu?

We need change and we need it very soon!
 
Hilo la wazungu kuililia Tanzania ni kweli kabisa. Nimeshawahi kufanya kazi na wazungu toka Denmark na Sweden ambao walikuwa wanakuja Tanzania kwa mikataba ya miaka miwili na kuruhusiwa kuongeza mara moja mkataba wa miaka miwili mingine.

Wote waliokuwa wanakuja walikuwa wanaongeza mkataba kwa miaka miwili mingine na wote walikuwa wanataka waruhusiwe kuendelea kuishi Tanzania pamoja na sheria za mikataba yao ilikuwa hairuhusu hivyo. Wengine walikuwa wanaangusha mchozi kwa kuwa walikuwa wanaondoka Tanzania. Kilichokuwa kinatushangaza wengi tuliofanya kazi na wazungu wao ni kwamba nchi zote hizo ni matajiri na kiwango cha maisha ni cha juu mno kuliko hata cha Marekani, lakini bado walikuwa wanapenda kuendelea kuishi Tanzania.

Miaka ya karibuni nimekutana na wamarekani, waingereza, wacanada wanaoishi Tanzania ambao wanadai wao ndio wameshafika katika nchi ambayo wanataka kuishi for the rest of their lives, hawataki kabisa kurudi makwao, wanaenda makwao kutembea tu. Hivyo basi hilo la wazungu kuililia Tanzania ni la kweli kabisa

Wanakimbia stress pamoja na ugumu wa maisha. Inawezekana hawana kazi za uhakika kwao.

Pia wakiwa bongo wana social status kubwa maana ni white, lakini wakiwa kwao ni tofauti.
 
Swali jingine la kujiuliza, je ni kipi muhimu kuwa nacho, utajiri wa rasilimali pamoja na uongozi mzuri au kinachohitajika ni uongozi mzuri tu na mengine yatajipa yenyewe?

Nauliza hivyo kwa sababu wakati mwingine nashindwa kabisa kuelewa ninapoangalia nchi kama Japan (the second largest economy) na maendeleo waliyonayo ukizingatia historia (II WW) na rasilimali walizonazo. Juzi nilikuwa naangalia documentary fulani hivi iliyokuwa inaelezea maendeleo ya Japan ktk miaka 30-40 iliyopita. It's remarkable what they have done given their meager (meagre) natural resources.

Hawa jamaa wana mindset tofauti kabisa na sisi. Ni sawa na north ilivyo tofauti na south, au east na west.

Ndiyo sababu Mengi amekuwa akiimba siku zote kwamba tunatakiwa kuchange mindset zetu.

How ndipo kikwazo kilipo kwani mifano tunayopokea toka kwa watangulizi wetu yote ni ya kifisadi. Very unfortunate in deed.

Kwa maana hiyo tunaandaa taifa la mafisadi!!!

I am sorry to say this, but that is the reality.

May be inclusion of "ufisadi" as a subject in our curriculum may reverse the situation, but I dont know how serious and prepared is Maghembe and his team.
 
Very Unfortunate In Deed.
Yani Mtu Anadiriki Kumsifia Mwenzake Akipata Kazi Yenye Mianya Ya Kuiba!!!
Mtu Akipata Kazi Anaanza Kuangalia Kama Kuna Chochote Nje Ya Mshahara!!!
Mtu Anajindekeza Apate Kazi Yenye Ulaji!!!
Kwa Kweli Tiba Yetu Bado Haijaanza Kutayarishwa, Nadhani Wajukuu Wetu Wataanza Kuipeleleza Ni Wapi Inapatikana.
Yani Tuna Mindsets Za Ajabu Kabisa, Sijawahi Kuona Hata Mahali Pengine,
Inasikitisha Sana.
Tanzania Ni Masikini Sana Wa Elimu Jamii.
Masikini Wa Kutupwa,
Wazazi Hawajui Cha Kuwafunza Watoto, Watoto Wanakuwa Nunda, Wanafundishwa Na Dunia, Umasikini Huu Utaendelea Hadi Wazazi Watakapojipatia Nguvu Ya Kushape Taifa La Kesho Kwa Upendo Na Misimamo Halali Sustainable Ya Kijamii.
 
Back
Top Bottom