Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kutokana na mfano huo naona picha kamili ya sisi kuitwa NDIVYO TULIVYO...ni pamoja na maajabu kama haya ndio yameijenga community hii.. Je, unafikiri vitu kama hivi ndio sababu kubwa ya umaskini wetu?..Kwa maana kwamba kama wewe ungekuwa nafasi ya mh. rais wetu Kikwete siku ile ya mahojiano ungesema nini sababu ya Tanzania kuwa nchi maskini?..
RAIS Jakaya Kikwete amesema haelewi ni kwa nini Tanzania bado ni fukara ingawa imejaliwa rasilimali nyingi za asili kuliko nchi nyingi za bara la Afrika.
...Nafikiri tunaongoza barani Afrika katika kuvutia uwekezaji katika sekta ya madini..."
...Alipoulizwa juu ya utata wa vivutio vinavyotolewa katika sekta ya madini katika miaka ya nyuma, Rais Kikwete alisema hajui kama kuna utata wowote katika sekta hiyo....
"Matumizi ya kawaida ya mbolea katika kilimo chetu kwa sasa ni ya chini mno ukilinganisha na nchi nyingine. Kwa mfano, sisi tunatumia kilo nane za mbolea kwa ekari moja ukilinganisha na kilo 577 kwa ekari zinzotumiwa nchini Uholanzi," alisisitiza Rais Kikwete.
Alisema katika mpango wa miaka saba wa kuboresha kilimo, mkazo pia unatiliwa katika kuwatumia wataalam wa kilimo kuwafundisha wakulima mbinu za kisasa za ukulima.
Alisisitiza kuwa sekta ya utalii bado inaweza kuliingizia taifa fedha zaidi za kigeni kwa kuendeleza ujenzi wa hoteli zaidi katika fukwe na mbuga za wanyama ili kuwavutia watalii zaidi.
Unashinda kutwa nzima JF unamalumu kikwete kisha unataka nchi ipige hatua; tubadilike wazee umasikini hauondoki kwa porojo!
Swali la msingi la hoja nzima (ya Mtanzania na ya Mkandara) limepressupose kuwa we all agree and recognize this poverty. Kwamba wote tunatambua kuwa "Tanzania ni maskini" na hivyo tujadiliane ni "kwanini sisi ni maskini.
Hivyo tunapozungumzia "umaskini" ni lazima tusema tunazungumzia nini? Je tunazungumzia "kutopiga hatua haraka ya maendeleo" au tunazungumzia "ukosefu wa kipato cha mfukoni kumudu tunachotaka au tunachohitaji"? Je tunapozungumzia umaskini huu tunazungumzia ukosefu wa mahitaji ya msingi ya binadamu (chakula, mavazi, na makazi" bora? Tunapozungumzia umaskini huu ni kuwa si wote tuna magari ya kifahari, nyumba za kisasa, televisheni, internet majumbani kwetu, vyoo vya kuflush n.k?
Hivyo, kabla hatujafika mbali kujadiliana kama wengi walivyofanya hadi hivi sasa tukubaliane kwanza umaskini tunaojaribu kuuchanganua na kukumeng'enyua ni "nini" hasa? ni umaskini wa ukosefu wa vitu, watu, nafasi, hali, mazingira, kujimudu, kujikimu, elimu, uwezo, akili, vipaji au kitu gani hasi? na tukishaumaanisha (define) umaskini huo basi swali la pili tujikulize wa kwetu hasa ni "umaskini upi".. tukishautambua umaskini huu na kukubaliana kuwa ndiyo huo basi tufuatie kutoka hapo na kujiuliza ni kwanini tunao umaskini huo (kama kweli huo ni umaskini).
NAwashangaa sana Viongozi wetu. SUmaye alisema hilohilo na JK anasema hilohilo. NAdhania kama mtu akitoa sentensi kama hiyo cha kwanza inabidi ajiuzuru, kama hujui tatizo ni nini hakika huwezi kujua namna ya kutatua.
May be Mr President had the answer(Corruption within the party and Govermnent na uroho wa ELs na wenzao) but he was shy to speak it out.