Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Bro usidanganyike Kikwete kachaguliwa na tume ya uchaguzi ya Taifa NEC sio wananchi
 
Mutaendelea na kusota na umasikini mpaka pale mutakapoamua kuiondosha Chama Cha Mafisadi CCM kwenye madaraka.
 

Kutokana na mfano huo naona picha kamili ya sisi kuitwa NDIVYO TULIVYO...ni pamoja na maajabu kama haya ndio yameijenga community hii.. Je, unafikiri vitu kama hivi ndio sababu kubwa ya umaskini wetu?..Kwa maana kwamba kama wewe ungekuwa nafasi ya mh. rais wetu Kikwete siku ile ya mahojiano ungesema nini sababu ya Tanzania kuwa nchi maskini?..

Mkandara,

samahani mapema ni zile siku ambazo nina muda kama utaiona ndefu.

Jk ana tofauti na mtanzania wa kawaida kwa kweli kazi yake ata mimi naona nawedha ifanya ingawa sina political experience alizo nazo yeye.

Lakini kufuata miguu ya Kagame inataka mtu anaelielewa somo la siasa kisawa sawa hivyo mtu kama mimi sidhani kama nafaa kuwa ata junior minister huko. Nchi ambayo imepata kingozi kwa sasa Africa ni Rwanda. ukisema 'Ndivyo Tulivyo' Rwanda itakusuta with the amount of changes they have achieved in a short time.

Kwa hivyo kwetu ni uongozi mmbovu wa wachache kusababisha mateso ya wengi. Kwani nilikupa sababu tatu na zote zinachangia kuua maendeleo kabla ata atujaanza kusema tufanye nini kunyanyua uchumi wetu.

Ukitaka kujua hatuna kiongozi wewe raisi unasema eti hujui kwa nini sisi ni maskini hivi ata huyu mtu kweli anajua hata wajibu wake ni nini? as a human being ni kichwa ambacho akijali umaskini wa taifa lake. Ndio maana aelewi kwa nini, the moment you say that in an industrial society its the end of your political career and a subject of political joke (ridicule) for a long time.

Kuna vitu viwili muhimu lazima uelewe 'nature' na 'nurture'. Nature ni kusema mabadiliko ya hali ya hewa, survival za wanyama, impacts of global warming, mazingira ambayo rain forests zinajitokeza, mwanamke kupata kizazi, sijui kukua, kubalee, kufa etc. etc.

Lakini kamwe tusiseme eti 'Ndivyo Tulivyo' yaani hii ni kusema ni nature yetu kuwa wavurugaji. Kukubali hili ni kusema hawa wazungu, sijui wachina ni wana nature ya maendeleo hivyo indirectly kukubali kuwa sisi ni inferior race to them mentally.

Lakini ukweli wenyewe si hivyo kwa wewe ntatumia mfano wa-mkandara junior na mambo anayoyafanya kwenye darasa lililojaa wazungu kama 'ndivyo tulivyo' sasa iweje tena kijiafrica kiwatese kwenye uwanja wao. Hii ni kuonyesha vipaji tunavyo sasa 'nurture' ndio tatizo kwani hapa ndipo maendeleo ya wenzetu yalipo.

'Nurture' ni ku foster situation to get the desired results. Kwa kifupi ni akili ya binadamu kuleta mabadiliko au matarajio hayatakayo kutumia fikra.

Mfano kujifunza kulima hivyo lazima tukopi sababu ambazo rain forest zina shamiri hivyo maji yana hitajika kwa kuwa atuna mvua lazima tujue tutamwagilia vipi kwani ni lazima, ardhi nayo inahitaji virutubisho fulani fulani kwani si sehemu zote unaweza lima na mwisho mbegu za kuweza kuleta hilo zao ulitakazo. Hivyo kulima ni nurture ya binadamu mwenyewe ni kitu ambacho katengeneza. Sasa hawa wenzetu leo wameeanza ku-nurture mpaka viumbe atu jui tu kama bado hawaja mtengeneza binadamu kwenye laboratories.

Vile vile akili ya binadamu pia ni nurtured almost ninety percent (the ninety percent is based on my psychology school of thinking) inaweza kuwa less or more lakini its a proven fact kwamba akili ya binadamu ni 'nurtured' yaani ni ya kuundwa tu maranyingi ni kutokana na mazingira yake.

Mfano mwarabu kwao kuoa binamu, au kuchukua mke wa kaka akifa ni sawa hizo ni mila zao, kwetu ata ukiwa muislamu kuoa binamu si sawa na kumchukua mke wa kaka akifa duuh we tena sijui jamii itakuonaje. Hii ni mistari ya fikra zilizopo kwenye jamii mbili tofauti nani sawa hapa? Jibu ni unategemea una muuliza mtu alietoka mila gani.

Sasa wenzetu wameshajua umuhimu wa nurture ya mawazo watu uamini kile wanachokijua maranyingi ndio maana propaganda nyingi si kweli mfano mzungu anae ona kwamba yeye ni bora kuliko mtu mweusi.

Lakini inabidi aamini hivi kwa jinsi tunavyo behave kutokana na tabia ambazo tuna nurture na jinsi media inavyo potray bala la Africa, lakini mzungu anaekuja Africa na kuishi atakwambia si kweli bali kuna highly corrupt officials na sheria za ubavu. Yaani anaiona africa kama mimi na wewe kwa sababu kaijua. Hivyo basi ni muhimu ku-nurture right thoughts kwenye jamii ili kufanikisha.

Hawa wazungu wengi especially wa middle class families utakuta watoto zao asubuhi ndio wana gawa magazeti na baskeli zao, kwenda kukata majani kwa jirani au kufanya kazi za weekend wakati wapo shule. Hii ni mfano wa nurture ya kuchukua responsibility ya income lakini hawa watoto wangeweza lala kwani kipato cha baba kinatosha. Lakini ni kumfunza mtu kuwajibika na baba wala aigusi hiyo hela ni responsibility ya mtoto kujifunza kuitumia. Hivyo kesho anapoenda kusema naomba hela ya viatu swali litakua hule mshahara wako uliufanyia nini? sasa usishangae vijana wa kizungu wengi huondoka kwao wakiwa 18 na kuanza kupanga kabla ya kuingia kwenye property ladder kwani wakishaingia teens wanafunzwa responsibilities za kujitegemea na kutoa hile fantasy ya kutegemea mtu ata baba yako mzazi.

This is how they nurture thoughts that translates into behaviours. Kwa watoto by parental guidance, and social environment ndio maana wenye hela huu avoid sehemu zenye drug problems kwa sababu mtoto inabidi um-nurture the right thoughts god knows what the streets will nurture the kid with drugs around and other anti social behaviours all around the neighbourhood.

Sasa angalia sisi watoto wetu tunawafunza nini, au hawa maskini wanao jilindukia watoto wana wafunza nini hao watoto ktk responsibility iwapo wao wenyewe awapo responsible. Si ajabu maisha ya maskini kote duniani hayana tofauti its a fact less responsible and no future goals mladi siku ipite, wiki, mwaka, lakini si wakusema baada ya miaka fulani nataka kuwa nime achieve kitu fulani kwa ajili ya kuboresha maisha yangu kwa kufikiria kwa namna za kweli na kwa kujitegemea si kwa fantasy wala msaada na sikusema mungu atanisaida kamwe utamuona kama ujafanya kitu cha kuleta mabadiliko wewe mwenyewe utashinda siku na mchana kwenye hilo jumba msikiti/kanisa, kamwe atokei ni wewe kuleta hayo mabadiliko.



Na serikali za hawa wenzetu pia zinaendeleza jukumu la ku-nurture thoughts ili asilimia kubwa za watu wake waweze kuwa responsible kwenye kuchangia in their economy kwa faida yao na ya serikali.

Sasa hapa ndio mkandara junior atapo feli akirudi bongo na kichwa chake na kuweza kukufanya wewe useme ni kweli 'ndivyo tulivyo'. Wakati hawa anaowashinda leo kesho wao watakua wanapewa nafasi kwenye institutions kama mahospitali, engineering, law firms etc. Either through full time employment, apprentices au hata volunteering lakini na mabosi vile vile wanaangalia kwani kama washawapa favor watoto wanao wajua wenye talent hawa wezi waache wapotee wachukuliwe na makampuni mengine wanathamini kichwa kama cha mkandara junior kwetu amna hiyo. Kwanza ni akina Pamela, Ridhwani, Salama, Kitova, Kambarage na wengineo wakitoka hao ni wale wanaowajua akina Pamela, wakitoka wao ni wale wazazi wao wapo siku nyingi humo. Hivyo mtoto wa Juma duuh inakua bahati kubwa hivyo kuishia kupoteza kipaji cha mkandara junior ambae yupo bongo kasoma bongo na hana baba wakumpeleka ulaya hili akirudi awatishe na kizungu kwani huko kwetu kizungu ndio msomi au mwenye akili jamani nyie wa tanzania very ignorant people.

Kweli hii 'ndivyo tulivyo' au tabia mbaya za viongozi wetu kunyima chance watu kuleta changamoto, huta staajabu tuna maprofesa wengi sana nje wanao fanya mavitu makubwa kwenye nchi za wengine kwetu siasa ni mbovu atuna viongozi tuna wata wala.

Na uongozi wenyewe nao una nurture ufisadi sasa tazama the way huu ufisadi unavyo operate utagundua hamna Mwanasiasa wa juu atakaenda mahakamani hapa wala mkuu yeyote atakae fungwa. Mtu kama Zombe kesha waulia sana hawa viongozi wetu hivyo kufungwa huyu awezi, Wizi wa madini Kikwete alikua huko kabla ya kuingia uraisi na ni yeye kawa chagua watu wa kuwapeleka huko kwenye nishati, anajua vilivyo kuna nini huko sasa mnshangaa nini Lowassa na Richmond, wala amna chochote kinachotokea ya kusema Kikwete ajui, he knows everything yeye ndie president sasa tunashangaa eti ajui kwanini tanzania ni maskini unataka kusema mimi na wewe tunauelewa ufisadi kushinda Kikwete wakati yeye yupo siasa za juu tanzania karibu miaka ishirini anaelewa tosha nurture inayoendelea huko ndio maana ahadi yake inakua ngumu kwani na yeye anatabia hizoo huyu ni nyani anaeliona k......, sasa ni kutulisha sisi propaganda na kuanza kulumbana hapa wakati the responsible person tunamjua si yeyote bali raisi mwenyewe huo ndio ukweli wenyewe.

Mpaka a sort matatizo matatu kuwapa elimu wananchi weki elimu si shule tu hata ya watu wazima ni elimu, uongozi bora wenye kulenga maendeleo na sheria zisizo mlinda yeyote mpaka hapo ni sisi tutakua maskini. Hivyo sivyo tulivyo, Kwani hata 'Mizungu Ndivyo Ilivyo' ebu waulize waingereza wakwambie parliamentary allowance ilivyokua ina abuse-ziwa, lakini hakuna amna ata mmoja alienda mahakanani ila wamegundua sheria ndio zilikua mbovu mwanadamu anajulikana kwa tamaa mpe nafasi uone tazama bankers wanavyo jipongeza na hizo bonuses. Hivyo wenzetu wanajua umuhimu wa sheria, uongozi wenye kulenga maendeleo ya jamii na kuweka mikakati yenye ku-nurture individual responsibility.

Ukiweza hayo kwanza kwa asilimia ya wananchi million 30 wako watakoa potea lakini maendeleo ya kasi yatakuja kwa wote au uige china huchague middle class families lakini the gap will be to wide just waulize wachina wa kibongo, ila wao wanajua nini maana ya individual responsibility leo wanasukuma mikokoteni kesho hao wana maoteli, kama walivyoona china amna opportunity ya kuwasaidia ila bongo itawapa mlo watch this space.... ndio utagundua si kwamba 'ndivyo tulivyo' bali tunasheria mbovu, uongozi mbovu, na highly ignorant society hiyo ni recipee for a poor society.
 
Watanzania ni masikini kwa sababu they do not know anything else na wameridhika.

Kama mtu anapeperusha bendera ya CCM kwenye kibanda chake cha udogo wakati hana huduma ya maji safi, matibabu, shule ni wazi kwamba ameridhika huyo na anastahili kwa asilimia 100% hali aliyokuwa nayo.
 
Juma Contena,
Mkuu nadhani umeona maelezo yangu kuhusiana na NDIVYO TULIVYO..
Bila shakla kabisa Ndivyo Tulivyo inatokana na NURTURE ambayo kwa bahati mbaya inakwenda sambamba na NATURE..
Utakumbuka msemo wangu wa WATU na MAZINGIRA... na hakika umefafanua vizuri sana hapo juu uliposema kwamba:- Akili ya binadamu pia ni nurtured almost ninety percent (the ninety percent is based on my psychology school of thinking) inaweza kuwa less or more lakini its a proven fact kwamba akili ya binadamu ni 'nurtured' yaani ni ya kuundwa tu maranyingi ni kutokana na mazingira yake.


Hapa mkuu wangu ndipo mimi Mkandara napoliona tatizo la mwafrika..
Ndivyo Tulivyo ni kutokana na sisi kujifunza na kutumia elimu ya mazingira ya Ulaya ili kutuwezesha sisi kupata maendeleo..yaani tunajaribu kubadilisha mazingira yetu ili yafanane na Ulaya..badala ya ku face matatizo yetu kama matatizo sugu na maadui wa maendeleo ktk mazingira yetu...
Maprofessa wetu wote walosoma wamesoma elimu ya mazingira ya Ulaya.. Hawawezi kutafsiri elimu yao na kui apply ktk mazingira yetu, wanashindwa na ukiwauliza sababu watasema resources na tools hatuna... Na binafsi naamini kabisa Tanzania na nchi za Kiafrika tumeshindwa kuendelea kwa sababu tumeshindwa kukubali kupambana na matatizo yetu kutokana na mazingira yetu isipokuwa tunajaribu kuyabadilisha mazingira yenyewe..
Hivyo Ndivyo Tulivyo ni pamoja na kutoamini kwamba Binadamu tumeumbwa na AKILI na ni hiyo akili inatakiwa kuvumbua tiba ya matatizo yetu kulingana na mazingira tuliyopo na sio KUIGA Ulaya wanafanya nini..
Mfano mdogo sana, sisi tumejaliwa na mwenyezi MUngu tumepewa maziwa ya maji baridi na masafi toka ktk lakes (maziwa) tulokuwa nayo, lakini tazama nchi nzima ina tatizo kubwa la maji.. tumeshindwa kujenga misingi ya maji safi kwa wote badala yake tunaagiza ama kuuziwa maji ya chupa ambayo huchanganywa madawa..Leo hii magonjwa kama cancer ni magonjwa ya kawaida kabisa jambo ambalo miaka ya 60 tulikuwa tunauliza Cancer ndio nni?..Na kibaya zaidi tunaagiza maji ya chupa kwa sababu ndio maendeleo tunayoyaona huko Ulaya watu wakinywa maji ya chupa! tumeshindwa kufahamu kwamba wenzetu hawana jinsi - hawana maziwa wala mito ya maji baridi na safi kama sisi.

Hivyo mkuu wangu Profesa wa Kitanzania anawezxa sana kufanya kazi vizuri Ulaya tena atasifiwa sana kwa sababu elimu yake imelengwa ktk kukabiliana na mazingira ya Ulaya, na ndio maana tunazidi kusisitiza watu kupata elimu yao kwa kiingereza..Hatuna sababu zaidi ya Ulimbukeni na kwamba msomi asojua kiingereza ni aibu. Majuzi Chavez kahojiwa na CNN kazungumza lugha gani? Ahmadinajad kazungumza kwa lugha gani, viongozi wote niliowaona UN wote wamezungumza kwa lugha zao za Asili isipokuwa AFRIKA.. JK akienda UN akazungumza kiswahili ili Watanzania asilimia 80 wapate kumsikia na kufahamu alozungumza basi nchi nzima itampiga vita na kusema JK kaabisha nchi, hali asilimia 80 ya wananchi wametoka kapa!..
Hapo ndipo utakapo jua kwamba sisi - NDIVYO TULIVYO!
 
Last edited:
Kwa sababu tunatumia muda mwingi kupika majungu JF badala ya kufanya kazi
 
RAIS Jakaya Kikwete amesema haelewi ni kwa nini Tanzania bado ni fukara ingawa imejaliwa rasilimali nyingi za asili kuliko nchi nyingi za bara la Afrika.

Ukimuuliza JK kwamba alikuwa anakimbilia nini madarakana ilhali hana "ACTION PLAN" wala hajui anakwenda kutekeleza nini, sijui kama atakujibu!
Sasa kama raisi mzima HAELEWI kwa nini nchi ni maskini, wasaidizi wake je wasemeje?




...Nafikiri tunaongoza barani Afrika katika kuvutia uwekezaji katika sekta ya madini..."

Sawa, ila kama uwekezaji wenyewe ndio ule wa KUUA watu kwa sumu zinazotoka katika mgodi basi tutarajie madhara makubwa hata kwa uchumi, achilia watu ambao wanateketea na maji ya mto TIGITHE kule Mara.



...Alipoulizwa juu ya utata wa vivutio vinavyotolewa katika sekta ya madini katika miaka ya nyuma, Rais Kikwete alisema hajui kama kuna utata wowote katika sekta hiyo....

Sasa kama alikuwa hajui, kwa nini aliunda kamati ya akina Zitto, Manyanya na wenzake kuchunguza uozo mikataba ya madini?




"Matumizi ya kawaida ya mbolea katika kilimo chetu kwa sasa ni ya chini mno ukilinganisha na nchi nyingine. Kwa mfano, sisi tunatumia kilo nane za mbolea kwa ekari moja ukilinganisha na kilo
577 kwa ekari zinzotumiwa nchini Uholanzi," alisisitiza Rais Kikwete.

JK must be joking!
Ardhi ya Waholanzi haina rutuba kama ardhi ya kwetu, kwa sababu ardhi yao ni ya "Kutengenezwa" kuna haja gani ya kuwaiga Waholanzi katika kuweka mbolea nyingi? Wao ardhi wameitengeneza kutokana na 'Kuhamisha' bahari, hivyo ardhi ina chumvi nyingi, wanahitaji neutralizers nyingi zaidi ili kuondoa salinity katika udongo! Shida hiyo haipo pale Gairo na Kibaigwa, wala Uyole, sasa kuna haja gani ya kuwaiga Wadachi?




Alisema katika mpango wa miaka saba wa kuboresha kilimo,
mkazo pia unatiliwa katika kuwatumia wataalam wa kilimo kuwafundisha wakulima mbinu za kisasa za ukulima.

Sasa JK, kazi ya mabwana shamba kwa miaka yote hiyo imekuwa ni ipi, kama unatilia mkazo suala hili wakati huu?



Alisisitiza kuwa sekta ya utalii bado inaweza kuliingizia taifa fedha zaidi za kigeni kwa kuendeleza
ujenzi wa hoteli zaidi katika fukwe na mbuga za wanyama ili kuwavutia watalii zaidi.

Ila msijenge pale COCO beach please, bado tunapapenda!
 
Unashinda kutwa nzima JF unamalumu kikwete kisha unataka nchi ipige hatua; tubadilike wazee umasikini hauondoki kwa porojo!
 
Unashinda kutwa nzima JF unamalumu kikwete kisha unataka nchi ipige hatua; tubadilike wazee umasikini hauondoki kwa porojo!


Sema TUNASHDINDA JF!
Kwani ww ulikuwa wapi unapoandika ujumbe huo?
 
sisi wananchi ndio masikini lakini viongozi wetu sio masikini,

na siku za kula mtu akipikiwa pilau ya siku moja tu basi kila yake kwa viongozi wapotofu.

lakini hili swali nafikiria akaulizwe kikwete kwani yeye na jamaa zake wanakula uzuri

lakini sie naona ndio wapumbavu sio masikini
 
Swali la msingi la hoja nzima (ya Mtanzania na ya Mkandara) limepressupose kuwa we all agree and recognize this poverty. Kwamba wote tunatambua kuwa "Tanzania ni maskini" na hivyo tujadiliane ni "kwanini sisi ni maskini.

Hivyo tunapozungumzia "umaskini" ni lazima tusema tunazungumzia nini? Je tunazungumzia "kutopiga hatua haraka ya maendeleo" au tunazungumzia "ukosefu wa kipato cha mfukoni kumudu tunachotaka au tunachohitaji"? Je tunapozungumzia umaskini huu tunazungumzia ukosefu wa mahitaji ya msingi ya binadamu (chakula, mavazi, na makazi" bora? Tunapozungumzia umaskini huu ni kuwa si wote tuna magari ya kifahari, nyumba za kisasa, televisheni, internet majumbani kwetu, vyoo vya kuflush n.k?

Hivyo, kabla hatujafika mbali kujadiliana kama wengi walivyofanya hadi hivi sasa tukubaliane kwanza umaskini tunaojaribu kuuchanganua na kukumeng'enyua ni "nini" hasa? ni umaskini wa ukosefu wa vitu, watu, nafasi, hali, mazingira, kujimudu, kujikimu, elimu, uwezo, akili, vipaji au kitu gani hasi? na tukishaumaanisha (define) umaskini huo basi swali la pili tujikulize wa kwetu hasa ni "umaskini upi".. tukishautambua umaskini huu na kukubaliana kuwa ndiyo huo basi tufuatie kutoka hapo na kujiuliza ni kwanini tunao umaskini huo (kama kweli huo ni umaskini).
 
Mkuu Mwanakijiji,
Hivi Yule maskini omba omba mtaani huwa ana umaskini wakitu gani? hivi kweli unaweza tenganisha kati ya haya kuweza pata haswa umaskini wa omba omba mtaani kuwa maskini kwa sababu hana fedha za chakula, maskini kwa sababu hana nyumba nzuri? au hana gari zuri?

Mimi nadhani kazi hiyo ni kubwa zaidi.. tunakubali sisi ni maskini iwe wa Hali na Mali tosha kabisa... chukulia kama wewe umesimamanafasi ya Kikwete sidhani kama ungerudisha swali na kuuliza sisi tuna umaskini gani?..itaonyesha una kataa umaskini wetu hali upo wazi kabisa kuwa Tanzania ni maskini..

Na isije chukuliwa manao hoji mada hii kwa kejeli ati masikini ni watu lakini nchi yetu ni Tajiri.. kwani ukweli ni kwamba HAKUNA nchi maskini duniani.... hakuna ardhi maskini sehemu yoyote ile iwe Iceland au Greenland. Hata jangwa lina utajiri wake, kinachotakiwa ni wakazi wa jangwa hilo kugundua mazingira yao na rasilimali zinazopatikana jangwani huko.. Hakuna ardhi wala viumbe wengine ambao wanaweza kuwa Maskini ila sisi binadamu..
 
Swali la msingi la hoja nzima (ya Mtanzania na ya Mkandara) limepressupose kuwa we all agree and recognize this poverty. Kwamba wote tunatambua kuwa "Tanzania ni maskini" na hivyo tujadiliane ni "kwanini sisi ni maskini.

Hivyo tunapozungumzia "umaskini" ni lazima tusema tunazungumzia nini? Je tunazungumzia "kutopiga hatua haraka ya maendeleo" au tunazungumzia "ukosefu wa kipato cha mfukoni kumudu tunachotaka au tunachohitaji"? Je tunapozungumzia umaskini huu tunazungumzia ukosefu wa mahitaji ya msingi ya binadamu (chakula, mavazi, na makazi" bora? Tunapozungumzia umaskini huu ni kuwa si wote tuna magari ya kifahari, nyumba za kisasa, televisheni, internet majumbani kwetu, vyoo vya kuflush n.k?

Hivyo, kabla hatujafika mbali kujadiliana kama wengi walivyofanya hadi hivi sasa tukubaliane kwanza umaskini tunaojaribu kuuchanganua na kukumeng'enyua ni "nini" hasa? ni umaskini wa ukosefu wa vitu, watu, nafasi, hali, mazingira, kujimudu, kujikimu, elimu, uwezo, akili, vipaji au kitu gani hasi? na tukishaumaanisha (define) umaskini huo basi swali la pili tujikulize wa kwetu hasa ni "umaskini upi".. tukishautambua umaskini huu na kukubaliana kuwa ndiyo huo basi tufuatie kutoka hapo na kujiuliza ni kwanini tunao umaskini huo (kama kweli huo ni umaskini).

Dear Mzee Mwanakijiji,
Nimefurahi sana namna ulivyoelezea kuhusu huu umaskini wetu. Kwa kweli kama mimi ningelikuwa ndio owner wa hii Forum basi ningeliisimamisha mijadala yote na tukajadili hili suala la umaskini wetu mpaka tukajua kwanini sisi ni maskini na nini tufanye ili huu umaskini ututoke.
Sisi ni maskini na tutaendelea maisha yote kuwa maskini because we lack education (not literacy).
Hivyo tunavyozungumzia "umaskini" ni lazima tufahamu kuwa tunazungumzia kukosa kwetu elimu. Wengi wetu hatukupata nafasi ya kujielimisha na wengi katika vizazi vyetu wanasoma kwenye mazingira ambayo yatawafanya wawe de-motivated katika maisha yao kila siku.
Umaskini wetu sio ukosefu wa kipato cha mfukoni. Tunaweza tukajazwa mapesa kila mtu mfukoni mwake and still umaskini wetu hautoondoka.
Umaskini wetu sio kwasababu ya ukosefu wa mahitaji ya msingi ya binaadamu kama ulivyoyaeleza hapo juu. Serikali inaweza ikaweka vituo katika kila Kata na hapo watu wakawa wanakuenda kituoni kula bure cha asubuhi, cha mchana na cha usiku kama ilivyokuwa China huko nyuma and still tutakuwa maskini.
Pia, serikali inaweza kumjengeea kila mtu nyumba kama zile za NHC za siku zile and still umaskini wetu utabakia pale pale.
Kila mtu nchini kwetu anaweza kuwa na gari, TV, internet na vyoo vya kuflush and still tutabakia maskini, na hivyo vyoo vya kuflush vitafanyakazi siku 2-3 tu na baadae vitajazwa mchanga na kufunikwa na watu watafanya shughuli zao mwituni walikozowea!
Karume kule kwa wenzetu aliwajengea wananchi nyumba za ghorofa pale Michenzani na siku moja alfajiri alipokuwa Karume akipita akasikia jogoo anawika ghorofani. Karume akasimamisha gari na mwenyewe akaenda juu. Huko juu akamkuta mswahili anafuga kuku ghorofa ya 4. Kwanini? Jaza mwenyewe. Mswahili alihamishwa ghorofani hapo hapo.
Umaskini tunaouzungumzia na ambao unaotubana kweli sio ukosefu wa material things. Ukosefu wa material things ni ishara tu za ukosefu wa elimu. Umaskini wetu ambao serikali yetu na Sh JK haujui ni kutambua kuwa tunakosa elimu. Elimu sio kusoma na kuandika tu bali in addition to other things is information about or training in a particular subject. Bila ya elimu hayo yote tunayoyafanya - yaani kujenga mabarabara mapana, majumba marefu, etc ni kazi bure. Hizo nyumba ndefu zitamalizikia kufugiwa kuku na mbuzi ndani. Hizo barabara zitakujakuwa vidimbwi vya vyura.
Elimu ndio iwe NAMBARI ONE kwenye nchi yetu na sio CCM!!!
Sifahamu kwanini JK hafahamu kuwa elimu ndio kila kitu. Ukosefu wa elimu ndio unaoleta ishara hizo zote za umaskini – yaani ukosefu wa chakula, ukosefu wa nyumba bora, ukosefu wa mavazi, etc etc. Hata tukapewa leo chakula cha bure, nyumba bora za bure na kila mtu akapewa suti 3 au 4 (japokuwa Pinda hataki tuvae suti) still tutakuwa maskini. Tupe elimu na utaona kuwa tutajua wenyewe nini chakukila, tutajua wenyewe wapi pazuri pakulala na pia tutajua wenyewe tuvae nini.
Sekta ya elimu ndio sekta ya kutiliwa mkazo, lakini leo sekta hii ndio sekta ya mwisho kabisa katika nchi yetu. Shuleni watoto wanakaa chini kwenye mchanga bila ya viti wala meza. Shule tele hazina walimu wa kutosha. Safari moja nilikuwa kule ZNZ na nikaitembelea ile Karume Technical College na nikakuta department nzima inayo mwalimu mmoja tu. Nilisikitika sana sana. Nilijiuliza hii serikali ya Mapinduzi inayoringiwa sana na CCM ipo wapi? Wizara zetu za elimu hazijali kabisa juu ya yale yanayotokea mashuleni. Walimu wakiwepo wasiwepo kwao ni sawa tu. Watoto wanapelekwa kukata kuni, kuteka maji, etc hakuna mmoja anaejali au kuuliza.
Yule Mwana_Forum anaesema kuwa Miafrika Hivi Ndivyo Tulivyo naona kapatia kabisa na wala hajakosea.
 
NAwashangaa sana Viongozi wetu. SUmaye alisema hilohilo na JK anasema hilohilo. NAdhania kama mtu akitoa sentensi kama hiyo cha kwanza inabidi ajiuzuru, kama hujui tatizo ni nini hakika huwezi kujua namna ya kutatua.
May be Mr President had the answer(Corruption within the party and Govermnent na uroho wa ELs na wenzao) but he was shy to speak it out.

I CONCUR WITH YOU.....
Kama kiongozi hajui basi hata kupanga mikakati ya kupambana na umaskini itakuwa kazi kubwa.Lakini na wananchi siye tumejiweka wapi kwenye hili? Viongozi wetu hawajui, na sisi hatujui pia? Kama tunajua, ni njia gani zinatumika/zinaweza kutumika kuwasaidia hawa viongozi kujua na hatimaye kutafuta ufumbuzi? Haya ni maswali ya kifilosofia na nadharia zaidi.Kila mtu mwenye uelewa wa kawaida anajua fika kuwa umasikini wetu kwa kiasi kikubwa ni wa kujitakia, kujisababibishia na unaletwa na uroho wa hao hao tunaowategemea kufanya yafuatayo:
1.Kushika dhamana ya rasilimali zetu na kuhakikisha zinatumika kwa manufaa yetu sote
2. Kutuongoza kwa uaminifu
3. Kutumia maarifa, ujuzi, uelewa na nafasi/dhima na dhamana tulizowapa kuwakilisha maslahi yetu kama wananchi

Kwa vile viongozi wetu wengi wanaenda kinyume na matarajio yetu hayo kwa kuacha nyufa na mianya ya kuwezesha uvujaji wa rasilimali zetu, basi ubinafsi, ulafi, ubadhirifu, ufisadi, uzembe na vitendo na hulka zinazofanana na hayo yote huendelea kutudidimiza zaidi na zaidi katika umaskini.Kwa mtaji huu, viongozxi wetu waelewe kuwa hatuwezi kamwe kujiondoa kwenye rindi zito la umaskini.
SIAMINI KAMA KIONGOZI WETU KATIKA ILE OFISI YA JUU KULIKO ZOTE HAYAJUI HAYA.

CHA KUFANYA:
katika kipindi kifupi -hao viongozi wetu wazibe nyufa za UVUJISHAJI WA RASILIMAlI za nchi yetu; sisi wananchi tuwe makini zaidi katika kufuatilia na kuhoji bila kuchoka ( persistently).TUWABANE MBAVU TU HADI KIELEWEKE.
 
Hivi karibuni Balozi wa Marekani alisema kwamba tutafakari kwa nini sisi ni masikini licha ya kuwa tuna maliasili nyingi? Naomba wana JF tutafakari swala hili
 
Sisi ni maskini ki uchumi kwa sababu ya viongozi waliopo wasio kuwa na vision.. Asilimia ndogo sana ya viongozi ambao wana nia ya dhati ya kuiendeleza Tanzania.. Wengi wanawaza jinsi ya kushinda chaguzi na kuendelea kujinufaisha wao na familia zao! But I promise them, kuna siku moto utawaka, na hawatakuwa na nafasi ya kuuzima.. Haiwezekani nchi kama North Korea iliyokuwa na uchumi sawa na Tanzania mwaka 1961, juzi hapa inamtishia Marekani kwa kuzalisha Uranium.. Sisi hatuna chochote..

So sad! I hate most of Tanzanian politicians especially Jk na group lake.. It sucks! Na inakera zaidi unapomsikia Makamba anasema yupo pale kuilinda katiba ya CCM na Ilani yake, na si kuilinda NCHI.. What is the hell?
 
Tuna generation inayotaka ulaji tu.Viongozi wa sasa ,ni kusafiri tu nje ya nchi.Chama tawala kipo tu kulinda maslahi ya elites na kuwadanganya wananchi poor huko vijijini.

Angalia Waziri Mkuu Pinda.Tangu mwaka uanze amecover maili ngapi hewani kwenda majuu.

Kwa sasa London ndio play ground zao kwa kuona diaspora na matawi ya CCM.Naona wanaenjoy matunda ya Wazungu,kupanda ndege,kulala hotel safi,kununua suit ,na kukwepa traffic na joto Dar Es Salaam.
 
Wengi viongozi tunaokuwa nao ni wizi na ubinafsi mtupu. Hii imeondoa uzalendo na kuwafanya hata WaTz wanaoanza kazi kuwa na fikra za kujiju tu na si kwa maslahi ya nchi!
 
Sisi ni maskini kwa sababu watanzania tumeamua kuwa na kubaki maskini milele. Siku akili zetu zikipevuka tutakuwa kati ya matajiri wa dunia hii.

Lini? itategemea na sisi wenyewe na ohhhhhhhh Mungu wangu kama utajiri wenyewe utakuwa bado upo!
 
Mbona vidole vyote tunelekeza kwa wengine yaani sisi mmoja mmoja tumefanya nini kupambana na umasikini na kuwasaidia wengine kupambana na umasikini?
 
Back
Top Bottom