Swali la msingi la hoja nzima (ya Mtanzania na ya Mkandara) limepressupose kuwa we all agree and recognize this poverty. Kwamba wote tunatambua kuwa "Tanzania ni maskini" na hivyo tujadiliane ni "kwanini sisi ni maskini.
Hivyo tunapozungumzia "umaskini" ni lazima tusema tunazungumzia nini? Je tunazungumzia "kutopiga hatua haraka ya maendeleo" au tunazungumzia "ukosefu wa kipato cha mfukoni kumudu tunachotaka au tunachohitaji"? Je tunapozungumzia umaskini huu tunazungumzia ukosefu wa mahitaji ya msingi ya binadamu (chakula, mavazi, na makazi" bora? Tunapozungumzia umaskini huu ni kuwa si wote tuna magari ya kifahari, nyumba za kisasa, televisheni, internet majumbani kwetu, vyoo vya kuflush n.k?
Hivyo, kabla hatujafika mbali kujadiliana kama wengi walivyofanya hadi hivi sasa tukubaliane kwanza umaskini tunaojaribu kuuchanganua na kukumeng'enyua ni "nini" hasa? ni umaskini wa ukosefu wa vitu, watu, nafasi, hali, mazingira, kujimudu, kujikimu, elimu, uwezo, akili, vipaji au kitu gani hasi? na tukishaumaanisha (define) umaskini huo basi swali la pili tujikulize wa kwetu hasa ni "umaskini upi".. tukishautambua umaskini huu na kukubaliana kuwa ndiyo huo basi tufuatie kutoka hapo na kujiuliza ni kwanini tunao umaskini huo (kama kweli huo ni umaskini).
Dear Mzee Mwanakijiji,
Nimefurahi sana namna ulivyoelezea kuhusu huu umaskini wetu. Kwa kweli kama mimi ningelikuwa ndio owner wa hii Forum basi ningeliisimamisha mijadala yote na tukajadili hili suala la umaskini wetu mpaka tukajua kwanini sisi ni maskini na nini tufanye ili huu umaskini ututoke.
Sisi ni maskini na tutaendelea maisha yote kuwa maskini because we lack education (not literacy).
Hivyo tunavyozungumzia "umaskini" ni lazima tufahamu kuwa tunazungumzia kukosa kwetu elimu. Wengi wetu hatukupata nafasi ya kujielimisha na wengi katika vizazi vyetu wanasoma kwenye mazingira ambayo yatawafanya wawe de-motivated katika maisha yao kila siku.
Umaskini wetu sio ukosefu wa kipato cha mfukoni. Tunaweza tukajazwa mapesa kila mtu mfukoni mwake and still umaskini wetu hautoondoka.
Umaskini wetu sio kwasababu ya ukosefu wa mahitaji ya msingi ya binaadamu kama ulivyoyaeleza hapo juu. Serikali inaweza ikaweka vituo katika kila Kata na hapo watu wakawa wanakuenda kituoni kula bure cha asubuhi, cha mchana na cha usiku kama ilivyokuwa China huko nyuma and still tutakuwa maskini.
Pia, serikali inaweza kumjengeea kila mtu nyumba kama zile za NHC za siku zile and still umaskini wetu utabakia pale pale.
Kila mtu nchini kwetu anaweza kuwa na gari, TV, internet na vyoo vya kuflush and still tutabakia maskini, na hivyo vyoo vya kuflush vitafanyakazi siku 2-3 tu na baadae vitajazwa mchanga na kufunikwa na watu watafanya shughuli zao mwituni walikozowea!
Karume kule kwa wenzetu aliwajengea wananchi nyumba za ghorofa pale Michenzani na siku moja alfajiri alipokuwa Karume akipita akasikia jogoo anawika ghorofani. Karume akasimamisha gari na mwenyewe akaenda juu. Huko juu akamkuta mswahili anafuga kuku ghorofa ya 4. Kwanini? Jaza mwenyewe. Mswahili alihamishwa ghorofani hapo hapo.
Umaskini tunaouzungumzia na ambao unaotubana kweli sio ukosefu wa material things. Ukosefu wa material things ni ishara tu za ukosefu wa elimu. Umaskini wetu ambao serikali yetu na Sh JK haujui ni kutambua kuwa tunakosa elimu. Elimu sio kusoma na kuandika tu bali in addition to other things is information about or training in a particular subject. Bila ya elimu hayo yote tunayoyafanya - yaani kujenga mabarabara mapana, majumba marefu, etc ni kazi bure. Hizo nyumba ndefu zitamalizikia kufugiwa kuku na mbuzi ndani. Hizo barabara zitakujakuwa vidimbwi vya vyura.
Elimu ndio iwe NAMBARI ONE kwenye nchi yetu na sio CCM!!!
Sifahamu kwanini JK hafahamu kuwa elimu ndio kila kitu. Ukosefu wa elimu ndio unaoleta ishara hizo zote za umaskini yaani ukosefu wa chakula, ukosefu wa nyumba bora, ukosefu wa mavazi, etc etc. Hata tukapewa leo chakula cha bure, nyumba bora za bure na kila mtu akapewa suti 3 au 4 (japokuwa Pinda hataki tuvae suti) still tutakuwa maskini.
Tupe elimu na utaona kuwa tutajua wenyewe nini chakukila, tutajua wenyewe wapi pazuri pakulala na pia tutajua wenyewe tuvae nini.
Sekta ya elimu ndio sekta ya kutiliwa mkazo, lakini leo sekta hii ndio sekta ya mwisho kabisa katika nchi yetu. Shuleni watoto wanakaa chini kwenye mchanga bila ya viti wala meza. Shule tele hazina walimu wa kutosha. Safari moja nilikuwa kule ZNZ na nikaitembelea ile Karume Technical College na nikakuta department nzima inayo mwalimu mmoja tu. Nilisikitika sana sana. Nilijiuliza hii serikali ya Mapinduzi inayoringiwa sana na CCM ipo wapi? Wizara zetu za elimu hazijali kabisa juu ya yale yanayotokea mashuleni. Walimu wakiwepo wasiwepo kwao ni sawa tu. Watoto wanapelekwa kukata kuni, kuteka maji, etc hakuna mmoja anaejali au kuuliza.
Yule Mwana_Forum anaesema kuwa
Miafrika Hivi Ndivyo Tulivyo naona kapatia kabisa na wala hajakosea.