Tanzania inaresource nyingi sana ukilinganisha na nchi zingine zilizo endelea, Mfano Mbuga za Wanyama, Madini, Bahari ya Hindi, Maziwa (Tanganyika, Nyasa na Victoria) Watu wastaharabu na wenye ushirikiano, Siasa zetu ni za kistaharabu,
Halafu tunamisitu ya kutosha na mvua pia zinanyesha za kutosha sana, kwaajiri ya kilimo,, tuna mito mikubwa na Mabwawa ya asili kiasi kwamba Hata umeme tunauwezo wa kufua kwatumumia Resources hizo bila kutumia Gharama Kubwa na Kupata Faida Kubwa kwa Maendeleo ya nci,,
Lakini kitu kinacho nichanganya mimi Hivi vitu vyote vinaisha vinakwenda Wapi? Hivi Gesi ya Songas inafanya nini mpaka tunakuwa Na Mgao wa umeme?. Madini yanakwenda wapi sisi tunabaki waomba misaada?