Let me get this right are you saying if we get our contracts right buy fuel and it would be the end of our woes, if so enlight me how please?

And what approach are you taking in terms means tested?
 

Mimi nawaheshimu sana wachagga,ni watu wanafanana na wa Asia katika kujitambua,ku enzi utamaduni wao,hardworking, determination,focused.Huwa nawatania kwa kuwaita wachina wa Tanzania.Pia huwa nasema kama wangepata busti kwenye viwanda vyao vidogovidgo tusingekuwa tuna import vitu kama vile viatu kwa sababu tungekuwa na " viatu vya mchagga'
of good quality.

Wachagga ni mfano wa kuigwa ili kuleta maendeleo hapa Tanzania ,honestly speaking.Kujitambua na kujua nini cha kufanya in our own perspective ndo msingi wa maendeleo.Nipo huku ughaibuni,huwa tunatoa vitu China na kuleta huko home for business,mimi na rafiki zangu wote ninaowafahamu wamelizwa na ndugu zao huko Bongo,isipokuwa mchagga,huwa anashangaa inakuwaje ndugu yako anaweza kukuibia na kukumaliza kabisa,yeye anapeta na business zake safi,sisi wengine tumeamua tuanze kuwekeza huku tuliko.

Kuhusu external factors kama WB,IMF etc,kwa mtizamo wangu,naona ni woga tu,lakini sio kitu cha kutufanya tusithubutu.Watu wa success in life wanasema: 90% of all fears normally never happen,>>>>>,kwa hiyo tuthubutu,wenyewe watakuja in other ways.

"KWANI WAO WAWEZE WANA NINI, NA SISI TUSHINDWE TUNA NINI"...Juma Nature
 

Mdau Mchambuzi thanks for your thorough analysis maybe the solution would be to adopt the mining policies of Botswana to eliminate donor aid and set us free?..
 
Tanzania, budget yetu haiweki kipaumbele kwenye DEVELOPMENT ( Ni aibu hata kuweka % ya budget inayokwenda kwenye Dev).

Na kwa kuongezea tu, bajeti ya serikali imegawanyika katika makundi mawili -
1. Matumizi ya kawaida [Posho, mishahara, kutibu viongozi nje, safari za wakubwa nje, repairs za nyumba za viongozi, repairs za magari ya wakubwa, petroli na diesel za magari ya wakubwa, n.k);

2. Matumizi ya Maendeleo [Elimu, Afya, Miundo Mbinu, Maji, Kilimo n.k].

Kwa miaka zaidi ya 25 sasa, ukitazama kila bajeti Tanzania, 65%-70% huwa inaenda kwenye matumizi ya kawaida, na 30%-35% kwenye matumizi ya maendeleo. Kibaya zaidi ni kwamba, hata hizi zinazoenda kwenye matumizi ya maendeleo, mfano sekta ya afya, fedha zinaishia kwenye matumizi ya kutibu viongozi nje, na pia kuendesha hospitali za rufaa, na zile special kwa magonjwa kama kansa, mifupa n.k. Asilimia 75 ya bajeti za wizara kama ya afya inaishia huko juu, only 25% ndio inaenda kwenye ngazi za wilaya na zahanati. Ndio maana wilayani, na kwenye kata, zahanati, na hospitali za serikali hazina madawa, hazina vifaa, na hazina wataalam wa kutosha kwani hakuna hela huko, so wataalam wengi wanakimbilia ngazi za mikoa na kwenye hizo taasisi za kitaifa kama vile hospitali za rufaa, n.k. Mwisho wa siku unakuta too much manpower chasing very few resources huko, kitu ambacho kinachangia sana mambo kama haya ya migomio ya madaktari.
 
Mdau Mchambuzi thanks for your thorough analysis maybe the solution would be to adopt the mining policies of Botswana to eliminate donor aid and set us free?..

Upo sahihi. That's one of the best options for us. Nasikia serikali imekuja na sera mpya ambapo makampuni yote ya madini ya sasa na ya baadae yanatakiwa yatoe free shares kwa serikali 10%. Huu ni mwanzo mzuri lakini ni ndogo sana. Ilitakiwa iwe like 25%, ili kuwe na more impact in terms of revenues, kwani migodi kwa kweli inatengeneza hela nyingi sana. Kilo moja ya gold ni zaidi ya shillingi milioni 30; na hawa watu wanachimba gold tani 10, 15 kwa mwaka - kwa maana ya kilo zaidi ya 15,000 (kampuni moja tu). Sasa elf 15 maar millioni 30 ni ngapi? karibia 300 Billion shillings; Na gharama za kuendesha mgodi sio kubwa sana, especially kwenye ukanda kama wetu ambao una content nyingi sana per ton of mchanga, na yenye high quality; Kwa wastani, kufanya exploration ya leseni mpya ili kubaini kama kuna madini ya kutosha ni kama 2 billion shillings; baada ya hapo, kununua vifaa, mafuta n.k ili kuanza uzalishaji, ni kama 9 billion shillings; na kama tunavyojua, migodi ni more capital intensive, so labour charges ni zile za maskini wachache tu kuendesha malori n.k, na kuwalipa peanuts, na kuwa na management ya watu wachache, shughuli zinaendelea. Sasa kama jumla ya gharama za uendeshaji kwa mwaka ni wastani wa billioni kumi, na huku unatengeneza hadi billioni 300, kwanini usilipe kodi? Hivi inaingia akilini kweli kwamba kwa miaka kumi mgodi una declare loss, ili kukwepa ushuru? Ni ujinga wetu tu sisi wenyewe watanzania.

Kuhusu Botswana, nilipata bahati ya kwenda kutembea kule, licha ya serikali kuwa na karibia 50% ya hisa katika kila mgodi, pia hauwezi kukuta eti mtu ana dhahabu mtaani, yani hata ukiiona kwa bahati mbaya kwenye barabara, unaikimbia maana ukikamatwa nayo unapotezwa na serikali.
 
Sisi ni maskini kwa sababu hatuna vision wala discipline ya matumizi, kuanzia serikali kuu hadi kwa mtu mmoja mmoja

Serikali inasema haina pesa wakati kuna israfu kwenye matumizi yake ya kawaida

Muuza madafu analalama kazi ngumu na hapati faida ya kumtosha lakini ana wake wawili na watoto wanne
 

Dhana yako ya kujitambua na uchambuzi wako juu ywa wachagga umeshikana vizuri sana. Kuhusu WorldBank, ambao wapo kwa niaba ya interests za G8 za kuendeleza ukoloni mamboleo, ni kweli, sio wa kuogopwa, kitu muhimu ni self determination kama taifa kuondokana na uchumi tegemezi. Wakubwa wengi wanapenda kutegemea misaada kwani hii pesa ni rahisi sana kwa maana nyingi. Vinginevyo ni aibu, na ndio maana Nyerere alikuwa anauliza viongozi- Mnasubiri misaada kutoka kwa WorldBank na IMF, kwani ni wajomba zenu hawa?? Akiwa na maana kwamba misaada hii ina madhara makubwa sana;
 
Hizo nchi wana export manpower sisi tunatafuta manpower hatuna. Hawa Watanzania wanaokwenda nje ni kwa njia zao wenyewe tu lakini sio kwa kuwa tuna Industry ya ku Export Manpower. Hatuna.

Ingawa sijaelewa sana una maana gani kuhusu industry ya ku export man power, pengine kwasababu ninaichanganya na tatizo la brain drain, point yangu ilikuwa tu kwamba watanzania walio nje wengi wana mapato tu ya kuweza saidia ndugu zao nyumbani. Kutuma Dollar 50 kwa mwezi kwa shangazi kijijini Mara itafanya mambo mengi sana.
 

Hapo sio sahihi, Mjerumani aliwekeza reli inayopita sehemu zote muhimu, kulikuwa kuna central, south na north Routes. Mwingereza aliirithi reli na akahakikisha inafanya kazi vizuri kabisa, na wakati tunachukuwa Uhuru, kulikuwa kuna reli kila siku ya kwenda Mwanza, ya kwenda Tanga, Ya kwenda Arusha na ya kwenda mpaka Kenya. Ambapo hakuna reli kulikuwa kuna mabasi ya Railway na magari ya mizigo ya railway. Barabara ingawa zilikuwa si za lami lakini wakati tunachukuwa Uhuru barabara zote kubwa zilikuwa zikipitika misimu yote, si mvua si jua. Kulikuwa kuna PWD (Public Works Department) ikifanya kazi inavyotakiwa na mabarabara yote makuu yalikuwa na vituo vya TRM (Tanganyika Road Maintenance) hawa walikuwa wanahakikisha barabara zinapitika wakati wote.

Tanganyika haikuwa maskini wa mwisho, huo si ukweli kabisa, vipi uwe maskini wa mwisho wakati wa uhuru ambapo ulikuwa ndio exporter wa kwanza wa mazao ya shambani katika Afrika. Kumbuka katika Afrika nzima.

Ukweli ubaki kuwa ukweli, wakati anaondoka Nyerere kila kitu kilikuwa taabani. Nakumbuka sisi utotoni tukipanda treni kusafiri hadi unaona raha, vitanda vizuri, mashuka myeupe safi kabisa, chakula kizuri, hakuna kubanana, hakuna kuchelewa na ukienda Iringa hakuna reli unapanda basi la Railway. Aaaah, yule mzee katumaliza vibaya sana. Kila kitu kakiuwa, hakuna hata palipobaki na afadhali. Kubomowa ni rahisi kujenga ni tabu.

Ni miaka 120 tena hapo tusijidai ujanja, sisi wenyewe hatuwezi. Inabidi tupate wataalam wa uhakika kutoka huko walikoweza. La tunajidai kufanya wenyewe basi miaka 500 mingine, hata tusome tupindukie. Maawee! Kusoma pekee hakusaidii sana kunafuta baadhi ya ujinga lakini kuelimika ndio muhimu. Na kuelimika hakuji kwa kusoma tu. Kuelimika kunakuja na "expirience".

Utashindana na mtu ambae ana Universities kwa miaka 800 iliyopita, wasomi wangapi wametoka huko na wameacha "expience" ya kiasi gani? wewe ndio kwanza vyuo vyako vyote havijatowa mpaka leo hata wahitimu 500,000 kwa miaka yoooote vilivyokuwepo. Halafu unafikiri utaweza tu? Maaaweee! Tazama wenzenu miaka yao vilipoanza vyuo vikuu:

The first universities in Europe with a form of corporate/guild structure were the University of Bologna (1088), the University of Paris (c. 1150, later associated with the Sorbonne), the University of Oxford (1167), the University of Palencia (1208), the University of Cambridge (1209), the University of Salamanca (1218), the University of Montpellier (1220), the University of Padua (1222), the University of Naples Federico II (1224), the University of Toulouse (1229),[SUP][10][/SUP][SUP][11][/SUP] the University of Siena (1240).
 

Nilikuwa nakufahamisha kipato cha kutoka nje kule kingi kwa kuwa wana export manpower kwenda kufanya kazi nje ya Kenya (modern slavery), nchi nyingi tu zinafanya hivyo hususan Europe, USA, Mexico, Philippines, India, Pakistan, Banladesh, Srilanka, Sudan na sasa Kenya na kwingine, wanaingiza mapato kutokana na ku export manpower nayo ni industry ya pekee. WaTanzania wanaoishi na kufanya kazi nje wengi wameenda kwa njia zao binafsi na si kwa kuwa kuna Serikali ina sector maalum ya kuhamasisha na kutafuta soko la kupeleka nguvu watu nje kufanya kazi.

Nadhani utanielewa kama bado, unaweza google "manpower export" utaona nchi nyingi zinafanya biashara ya ku export manpower, skilled, semi skilled na unskilled.
 

Sikusema kwamba Tanzania ilikuwa ni nchi maskini wa mwisho Afrika bali nilisema moja ya nchi maskini Afrika. Ukweli upo pale pale. Kwa mfano, takwimu zinaonyesha hali ilikuwa kama ifuatavyo in 1960 kwa Kenya na Tanzania:


GDP: Kenya = 7.6 Billion Kenya Shillings; Tanzania 5 Billion Tanzanian Shillings;
Exports (Ambapo Kilimo kilikuwa zaidi ya 90% ya exports): Kenya 1.8 Billion Kenyan Shillings; Tanzania 1.3 Billion Tanzanian Shillings;

Kumbuka pia kwamba nchi zote zilikuwa chini ya East African Currency Board, so nchi zote mbili zilikuwa na exchange rate to a dollar zilizokuwa sawa:

Exchange Rate 1960: Kenya, 1 USD = 7.142 Kenyan Shillings; Tanzania, also 1 USD = 7.142 T.Shillings.

Ukifanya conversion hapa, Kenya had a bigger GDP in dollars, as well as bigger values ya exports in agriculture than Tanzania;

Source: WorldBank, World Tables, Second Edition (1980).
 
Wakuu umaskini wa Tanzania unatokana na weaknesses zilizopo ndani ya Tanzania, kuwalaumu wa nje ni kukwepa ukweli. External factors zina role yake, lakini bado sisi wenyewe hapa nyumbani hatujafanya kazi ya kutosha na kufikia kiwango cha kusema tatizo liko nje na si ndani. Zamani tulikuwa tunaambiwa tulinyonwa tulipuuzwa na kudharauliwa, lakini sasa hivi tunaona kuwa tumejiweka wenye vulnerable kutokana na kuwa we have one of the worst political systems, weakest institutions on the planet, corruption na uswahili.


Angalia mawaziri wetu, wabunge wetu, madiwani wetu. Tell me kama wao ndio wanafaa kuwa pale walipo kuliko walio nje. System tuliyonayo inaruhusu kumwacha mtu mwenye Merit kuwa kiongozi na kuruhusu wahuni, wezi na mafisadi kuwa mdarakani. Tanzania haiwezi kuwa na system sawa na UK au US, kwa kuwa ina mazingira tofauti sana. Ukiangalia baadhi ya CV za wabunge wetu unaweza kucheka, kuna watu hapa JF wanaweza kuwa wabunge bora na mawaziri bora kuliko waliopo. Siku hizi tunasikia kuwa mtu amepewa uwaziri, amepewa ubunge.....amepewa amepewa amepewa. Jenerali Ulimwengu alisema vyeo ni zawadi za watoto wa marafiki, mahawara, na kitu cha kulipia fadhila.

Angalia taasisi zetu zilivyodhaifu, angalia bunge lilivyo sloppy, angalia executive ilivyodhaifu(imefikia hatua ya kusema inawaogopa mafisadi) licha ya nguvu iliyopewa kisheria. Angalia kama kweli imewahi kuja na plan, suggestion au idea yoyote yenye uwezo wa kubadilisha hali ya nchi na kuifanya iwe better than it is now. Angalia jinsi inavyoshughulikia maswala ya uhalifu, uchumi, ya jamii na ya siasa, unaweza kudhani kama ni kundi la watoto linajadili jambo.

Ufisadi ndio tusiseme, tunakumbuka wikileaks walisema rais wetu alihongwa suti, kama rais(as institution anahongwa) what about rais and individual, waziri as individual, mbunge as individual?? Tunafahamu kuwa kuna mafisadi wameiba mabilioni ya fedha na wanafahamika, lakini serikali ilikuja kumkamata mhasibu mmoja aliyejikopesha shilingi laki 2 za serikali ili kumtibu mtoto wake.

Angalia tumejenga uwanja gani wa ndege toka mwingereza aondoke, tumejenga shule gani ya maana, tumejenga nini cha maana na kusema hiki tumefanya baada ya uhuru. Alivyojaribu kujenga Nyerere viko wapi?

Watu wanazungumzia viwanda, wengine wangependa virudi kama ilivyokuwa enzi ya nyerere, which is good, ambavyotunasikitika kuwa havipo. Lakini tunasahau kuwa tuliviuza kwa kuwa tulishindwa kuvimanage, unamchagua mtu kuwa mkurugenzi wa shirika analivuruga analifilisi kwa kuwa ni "mwenzetu" anahamishiwa sehemu nyingine. Huo uenzetu sasa upo kwenye serikali na kwenye bunge, tunashindwa kuji-manage. Kuna element nyingine ya uswahili ambayo ni kubwa sana na ni kansa katika siasa na utendaji wa Tanzania. hatua ya kwanza ni kuondoa ujinga huu. Uswahili ndio sumu kwenye attitude towards work kwa watanzania wengi. Tunaendesha mambo kishakaji, hata kazi tunafanya kishkajikishkaji tu.

Kwa hiyo kama ni kutoa jibu rahisi, ni kuwa Tanzania ni maskini kutokana na poor management, hatuna uwezo wa ku-organize resources zetu na kuzifanya zituletee maisha mazuri. Tukiendelea na style ya sasa ya uongozi hapa Tanzania, na kama serikali itanedelea kuwa ya design ya sasa hakuna kitakachobadilika hata miaka 1000. Tutakaa kujiliwaza kuwa uchumi wetu unakuwa kwa asilimia 5, na na muaskini pia unakuwa kwa asilima 10.
 

Kuhusu Treni kuwa nzuri, na huduma za mabasi kuwa nzuri, unadhani ni kwanini, si ni kwasababu serikali ilikuwa inatoa ruzuku na pia kuziendesha? Na baada ya 1985 WorldBank na IMF wakasema serikali iachane na hiyo biashara? Vipi tena dada yangu, mbona unachanganya mambo. Funguka.

Kuhusu Nyerere kuiacha nchi taabani, ebu naomba nijazie jedwali hapo chini - takwimu za 1985 wakati anaondoka, maana nikijaza mimi utaniona mwongo. Ukizijaza hizo, tujaribu fananisha Nyerere alizipokea hizo sekta za uchumi katika hali gani, na aliziacha katika hali gani, kwani unachofanya hapa ni kufananisha hali ilivyokuwa wakati wa uhuru na ile wakati anang'atuka:

GDP BY SECTOR OF THE ECONOMY 1960 1985 FOR FAIZA FOXY TO DETERMINE
KILIMO2.6 Billion Tanzanian Shillings X
MINING163 Million Shillings X
MANUFACTURING446 Million Shillings X
ELECTRICITY, GAS AND WATER53 Million Shillings X
TRANSPORT AND COMMUNICATIONS400 Million Shillings X
TRADE AND FINANCE887 Million Shillings X


Mind you:
In 1960: Exchange rate 1 USD = T.Sh 7.142
By 1985 wakati mwalimu anaondoka, Exchange rate: 1 USD = 17.47 Shillings.

Naomba unifafanulie Nyerere alibomoa wapi, bila ya kukwepa kutoa maelezo pia aliku nchi katika hali gani, na alijenga wapi. Tafadahali jaribu kuepuka hoja za ugali wa yanga, mchele wa simba, maharage ya coastal union. Pia ni naomba usiweke picha za magrorofa mapya chini ya awamu ya sasa, majengo ambayo mwanakijiji kutoka Itigi, akiingia tu pale mapokezi, anaweza kuitwa mwizi, kutokana na mavazi yake ya kifukara.

Naomba tujadili hali ya 1960 Nyerere alipokeaje, na wakati anaondoka aliiacha vipi, kwani wewe ndio umelenga hapo. Na key variables ni kuangalia key sectors of the economy zilikuwa vipi, nimekusaidia kuzipanga hapo juu.
 
Mkuu Mkandara,
Nikushukuru kwa mada inayoleta fikra. Mada kama hizi tunazihitaji kama sehemu ya michango yetu kimawazo. Niwaombe wachangiaji tuiangalie mada kama tatizo la Watanzania na si kuanza kulumbana nje ya mada na kupoteza mwelekeo.
Tuheshimu mawazo ya kila mmoja wetu hata kama tunatofautiana. Tofauti ni sehemu muhimu ya majadiliano.

Nipitie hoja chache kama zilivyoletwa na kwa tafsiri mbali mbali za umasikini wetu kutoka kwa Mkandara na MM.

Mkandara: Ni kweli kuna denial miongoni mwetu na kuna uhalali wa hilo. Ukiiangalia nchi yetu, watu wake na majaaliwa ya mola pengine kwa kulinganisha na nchi nyingine, ni ngumu kuamini sisi ni masikini. Sidhani kuwa tumekwama, ninachoelewa ni kuwa kuna kundi dogo limetukwamisha. Kundi hili linaitwa viongozi (nitafafanua) au lack of political will kama alivyosema Mchambuzi.

Mchambuzi: Ni kweli kuwa kuna ncha mbili zinazotudumaza za ndani na za nje, za ndani ni asilimia 60 na za nje ni 40. Za nje ni 40 kwasababu ingekuwa ni kubwa kama unavyosema basi tusingekuwa na tofauti ya umasikini wa Kilimanjaro na Singida au Mbeya na Kigoma. Kwa vile sababu kubwa ni za ndani tofauti ya Kagera na Mtwara inakuwa wazi. Viongozi wetu wanatumia external factor kukwepa ukweli. Huwezi kulaumu mfumo wa dunia wakati wako huuthamini. Mfano, hivi IMF au WB au G7 wametulazamisha tulipe watu posho za kukaa 330,000 halafu twende kuomba msaada wa kujenga vyoo kwasababu wao ni sababu ya tatizo letu!!

Raia Mwema: Ni matusi kusema Watanzania ni wavivu na hujiuliza serikali imewafanyia nini.
Kumbuka kazi za mtu binafsi zinaathiriwa sana na serikali kisera, mipango n.k. Kazi ya serikali ni kujenga mazingira mazuri yatakayozaa mafanikio kwa mtu mmoja mmoja na baadaye taifa kwa ujumla. Hivi mtu amelima nyanya Kipera Morogoro na zinaoza kwasababu hakuna soko uvivu wake upo wapi?
Kwanini kuwe na machungwa ya South Africa kule UK, na vitunguu vya Karatu viuzwe na Wakenya US? Hivi huoni hapa kuna lack of opportunity inayoanzia kwenye kuwezeshwa kielimu kwanza na baadaye mazingira mazuri!
Hapa ndipo naona hoja ya MM kuhusu Use, lack of opportunity na right and justice inapoingia.

Faizafox: Unaposema siku utakapoona kiwanda cha sindano basi utajua tumeanza kuendelea, halafu unasema kuna imrovement!! inanipa shida kuelewa unasimamia wapi. Nikukumbushe tu kuwa tulishaanza kuwa na viwanda vya zana za kilimo, baiskeli, mbolea na nguo ambavyo vimebinafsishwa na sasa ni vyuma chakavu kama kile cha Man'gula.
Labda nikuulize kwanini unataka kiwanda cha sindano na umesahau huko tulishapita?
Nadhani jiulize kwanini tumerudi nyuma na si lini utaona kiwanda cha sindano.

Nimalizie kwa kusema, tatizo letu si rasilimali wala rasilimali watu, na wala si sera. Tatizo letu lipo sehemu mbili.
1. Sisi wananchi tumeamini kuwa viongozi wametuajiri na sio sisi tuliowaajiri.
Kwamba wao wanapaswa kufanya wanachokitaka na si kile tunachokitaka wananchi. Tumesahau kuwa kabla ya ukoloni kuna jamii ziliwakataa warithi wa machifu kwasababu tu hawakuwa na sifa za uchifu na walimpa mrithi wa pili au wa tatu kiti cha enzi. Hawa hawakuwa na elimu bali kujitambua. Sisi tumepoteza hisia za kujitambua.

2. Kwa sababu viongozi wanadhani wametuajiri ndio maana wanaamua kujipangia yale yenye manufaa kwao na familia zao na si taifa.
Ndiyo maana hakuna anayehoji kwanini miaka 50 hatujaweza ku balance bajeti.

Ndiyo maana hakuna anayefikiri kuwa diaspora wanawezaje kuchangia maendeleo na jinsi gani serikali inaweza kufaidika na michango yao kwa jamii. Hivi kwanini western union ikusanye pesa zote na kuzirudisha Ulaya.
Kwanini serikali isijenge mazingira mazuri ili kupata kidogo kinachokuja.

Ndiyo maana hakuna kiongozi anayejiuliza, kwanini mkulima wa Kipera auze tenga la nyanya sh 1500 wakati hakuna nyanya Dar na Dodoma na nini kifanyike ili kumsaidia mkulima huyu anayehitaji ada za shule na ambaye angechangia kodi katika mazingira mazuri ya biashara achilia mbali kuikomboa familia yake kieleimu na afya.

Hatuja kwama, isipokuwa hatuna utashi wa kujikwamua. Kama tungesimama kwa pamoja na kuwaambia hakuna kununua vx , hakuna vikao vya posho za laki mbili na hizo zipelekwe katika elimu na afya, na muhimu kama tungewapa deadline ya mwaka na malengo ya kufikia kinyume chake wapishe wenye uwezo tusingekuwa hapa.

Umasikini wetu ni zao la kukosa nidhamu na wananchi tunadhima ya kusimamia nidhamu kwa njia yoyote ile ili mradi viongozi waelewe sisi ndio waajiri wao na tuna uwezo wa kuwaondoa kwa demokrasia hata kama wana siku 100 ofisini.
Hatuna nidhamu ya kuwatia adabu tuliowaajiri na wao hawana nidhamu ya kutusikiza na hapa ndipo tatizo lilipo.
 
Mada nzuri sana kwanza umasikini wetu una vigezo mbali mbali tafsiri mbali mbali kwa watu mbali mbali.

Kitu cha kwanza kwanda tunatakiwa tuwe na defnition moja ya umasikini na tueelewe. lakini vyovyote vile palipo na tatizo basi wadau wakuu ni VIONGOZI na WAONGOZWAJI. Sasa hawa kila mmoja ana mchango wake chanya au hasi katika tatizo.

NITAAAZA NA VIONGOZI

Kwa taifa kama la Tanzania na africa viongozi ndio wanatkiwa kuwa chachu na hapa ndipo kulipo na tatizo. Bila kuwepo viongozi wenye VISION vita ya umasikini imekuwa ngumu sabbau ni vita inapiganwa kwa style ya moto.

Kuna mtaalam mmoja anaitwa Bwana Walter rodney rafiki yangu aliniambia nisome.kitabu chake . Ni kitabu cha zamani sana lakini madai na hoja za mtaalam huyu zimesimama mpaka leo na zinaweza kuelezea kwa nini sisi ni masikini. Moja ya sababu ni ViONGOZi na siasa. na nyingine ni sisi mtu mmoja mmoja mimi na wewe

Ni mmoja watu wasiofurahishwa kuona SIASA ndio ajira inayolipa zaidi. Kwa haraka haraka unaweza usione uhusiano wa hii na umasikini lakini kwangu ni moja ya sababu......... Kam kwenye wilaya au mkoa mbunge ni Public figure anayepkea mshahara mkubwa na sio Afisa Elimu, Maji, Kilimo, Afya, Mhandisi

Na mbaya zaidi kitu kinaitwa demokrasia kinaweza kutupofusha lakini hivi hakuna anayeshangaa gharama za uchaguzi kwenye majimbo fulani ni mara tano ya pesa za maendeleo zinazopelekwa kwenye jimbo hilo hilo.

KUKOSA au KUTOTAMBUA VIPAUMBELE SAHIHI

Je
  • Ni kweli kilimo ni uti wa mgongo wa Tanzania kivitendo au ni siasa na maneno tu ? UWekezaji kwenye Kilimo ukoje
  • Kati ya waziri na waizara wa utalii au wa madini au kilimo na waziri wa mmbo ya nje wa Tanzania ni ipi inapewa kipaumbele na kuthaminiwa zaidi.?
Wizara ya mambo ya nje na wizara ya Ulinzi ya USA na UK zina mchango katika pato la taifa ndio maana kwao hizo ni wizara nyeti zaidi ya hata wiziara nyingine . Sasa sisi kwetu tunatathimi vipi mchango wa wizara ya mambo ya nje au ya Uliinzi mpaka ionekana ni muhimu sana kuliko nyingine.

Nisieleweke vibaya. Sina maana hizo wizara zidharauiwe lakini tukubaliane tutambue vipaumbele sahihi. Nchi kama Norway Inawezeana Jeshi la Uokozi na majanga lina Priority kubwa kuliko Jeshi la vita sababu Norway yenyewe inajiita na imejitambulisha katika duni kuwa ni Neutral. so haiwezi sana kwenye kununua vifaru inawezeka kwenye kununua vifaa vya uokozi na majanga.

vile vile nimewai kuhoji hivi kwa nini tunasikia Mwambata wa kijeshi wa tanzania ubalozini South afrikca au USA na sio mwambata wa kiuchumi au kiutalii au kibishara.. Ni vitu vidogo laini kwangu naona ina uhusiano na UMASIKINI wetu sababu viongzoi wetu wanaotkaiwa kuwa na VISION wamekariri. Tumeona kwenye cable za wiki leaks balozi wa USA akifanya lobbying kampuni ya USA Boeing ipate tender na kupiga bao Airbus. Je sisi huko mabolozini kuna sera hata ya kufanya lobbying ili chain super market moja inunue asali au bidhaa fulani kutoka Tanzania .

So kimataifa sisi ni masikini sababu tumekalaia kwenye Political diplomacy wakati wenzetu balozi zao wanazitumia kufanya technlogical, economical intelligence na lobbying. Inawezekana ubalozi wa japana tanzania una data toyota ngapi kwa mwezi kutoka japa zinaingia Tz. Sababu wana mtu wa kuchambua takiwmu hizo na kutoa ushauri. Lakini siwezi kushangaa mtanzania ukipiga simu ubalozi wa tanznaia japan au china kuuliza je Wachina au wajapan wanatumia asali ton ngapi kwa mwaka na wananunua kutoka nchi gani na kiasia gani utaaambiwa sio kazi yao..................

to be continued ....
 
........unaonyesha wazi hukuelewa kitu. Umetoka mtupu na pengine hili ndio tatizo jingine kuwa tumesoma lakini hatukuelemika.......

@Mkandara:Maadam umegundua hilo nina imani mara nyingine utafanyajitihada zakuwasaidia wasomaji wa namna hii wasitoke watupu katika mada zako kama unakusudia wazielewe.

Nilitegemea katka post yako ya kwanza ungemalizia na sentensi kama hizi hapa chini.


Wadau, what if the minerals mined here are sold in TZS to strengthen the currency and make petrolium imports cheaper?

Sell Gold, Diamonds & Tanzanite in TZS to strengthen the currency and reduce the price of imported petrol?



Mdau Mchambuzi thanks for your thorough analysis maybe the solution would be to adopt the mining policies of Botswana to eliminate donor aid and set us free?..



Kwa kuzingatia namna Mchambuzi alivyoeleza hapo awali kuwa umasikini wa Tanzania unatokana na mifumo ya ndani na mifumo ya nje, basi hipo haja ya kuweka mfumo mwingine utakaotoa kasoro hizo kwenye mfumo uliopo. Ingawa mifumo ya nje ina nguvu kubwa juu ya mipango yetu ya kukabiliana na changamoto za kiuchumi kutokana na Baadhi ya viongozi wetu kuwa waoga kutetea maslahi ya taifa huku wengine wakijikita katika ubinafsi, bado tunayonafasi ya kurekebisha mambo kwa kukuhakikisha wakati wakuandaa katiba mpya basi miongozo itakayodhibiti mifumo ya ndani na nje iliyotufikisha katika umasiki huu iingizwe katika katba bila vikwazo.

Ilikukabiliana na tatizo hilli kwa hatua za muda mfupi napendekeza mambo mawili kati ya mengi:

1. serkali inatakiwa kufufua upya mifumo ya uzalishaji wa viwanda kwa kuwanyanga wote waliopewa viwanda lakini kwa sasa viwanda hivyo havifanyi kazi na kutafuta muwekezaji ambaye anaweza kuviendesha, na ingekuwa jambo jema kama muwekezaji huyo angekuwa mtanzania au Taasisi imara za hapa nchini kama NSSF nakadhalika. Pia itoe mazingira mazuri kwa wajasiriamali wazalendo kuanzisha viwanda vya kuongeza ubora wa bidhaa hapa nchini, na kuwawezesha pia kupata masoko bora ya bidhaa zao nje ya nchi.

2. Serikali kupitia vyombo vya sheria na taasisi zake za fedha iwezeshe kudhibiti matumizi ya fedha za kigeni ndani ya nchi.
 

Hayo uliyoleza hapo yanawzeana yasie matatio maubw sana kama hiyo mishahara inalipa madaktari 50,000 na si mbrigedia 10,000. au inalipa mbunge wa jimbo lenye wapiga kura 20,000 tu. hapa bwana Rodney anaelezea cancer tuliyonayo ya siasa


Japo hizi ni takimu za zamani lakini naamin ndio ukweli wa hali halisi ulivyo sasa politics being best paying career


Huo mfano wa Gabon wa wastani wa mbunge na idadi ya wapiga kura nadhani kwa zanzibar upo wazi . Na baadhi ya majimbo ya tanzania nayo upo.
Kwa kweli binafsi sioni sababu ya kuwa na majimbo mengi wakati nchi yetu bado tunashare matatiza common. kama Maji. miundombinu afya, elimu, Mawasiliano. Kwangu kila mkoa unatakiwa usiwe na zaidi ya wabunge watano au sita. Hizo pesa nyingine za majimbo zingepelekwa kutatua matatizo ya umasikini

Huko ulaya sababu matatizo ya msingi ya binadamu walishayatatua basi unakuta wana matatizo na kero tofuti so wanahitaji wawakilishi wengi. sisi NEC yetu inamuongezea mzigo mwananchi.....
 
Tanzania, resources zinaibwa na wajanja, hiyo nakubali.........

kuna mambo mengine inabidi tujilaumu. Na sio tunaibiwa sisi wenyewe ndio tunawezesha na kuratibu kuibiwa kwetu.........

Mfano ile bei ya kuuza swala na twiga wanaoepelekwa nje tutasema tunaibiwa na nani kama si kujiibia na na kujihujumu sisi wenyewe waafrika.

MImi naona kitenda chaa kuuza wanyama hai nje ni sawa na Kitendo cha Toyota ya japan kuhamisha baadhi ya Ofisi zake kuu Tanzania na mapato na faida yake yote.

Wachina ambao hawategemei sana utalii wao wanyama wa panda kwao ni Teasure na wanawakodisha sio kuwauza. Sababu wachina kuna kitu wametambua zamani ambacho sisi hadi leo bado hatujatambua.......

So kama kweli kuna ushirikiano wa jumuiya ya afrika mashiriki na umoja wa afrika usio wa kisiasa tulitakiwa kukubaliana
  • kuzuia kabisa kuuza wanyama pori hi nje ya nchi maana ni sawa na kuhujumu utalii, uchumi na kuleta umasikini.
  • Kama kuna Ulazima basi kukodisha badala ya kuuza kama wachina walivyofanya Toka mwaka 1984.
Kwa hiyo nakubalina na wanaosoma kwamba tatizo kubwa kwamba mpaka sasa hatujajitambua . Leo hii tukiulizwa national treasurer za tanzania ni zipi . hta viongozi wenyewe hawajui.
 
Nashukuru sana kwamba wewe umetazama hivyo na pengine unazo points za maana. Mimi binafsi naamini TANZANIA ni sisi, tunaposema Tanzania imepata Uhuru ina maana ya watu wake na sio ardhi..vivyo hivyo tunapozungumzia umaskini wa nchi unawagusa moja kwa moja wananci wake..Na maadam tupo ktk kundi la nchi maskini na naamini hatuwezi kufanya mabadiliko yoyote ya kiuchumi kama tutajiondoa ktk kuamini kwamba Tanzania ni nchi maskini na inahitaji mabadiliko ili watu wake wapate kutajirika..Utajiri wa nchi unathaminishwa kutokana na utajiri wa wananchi wake.

Hivi Tanzania (exports) mauzo yake kwa mwaka ni kiasi gani kiasi kwamba tuweke madai ya Utajiri? maana utajiri unakuja pale unapouza na kupata faida.. Huo mgawanyo wa keki ya Taifa unauweka ktk mtazamo gani ikiwa tumekanda kilo moja tu ya unga na kupika keki ndogo haitoshi kuondoa njaa yetu wote na ndiyo sababu kubwa sisi kugombania mezani!.. Hawa viongozi wetu wanachofanya ni kukosa ustaarabu tu wa mezani, ni ulafi wa kuona sahani la keki mezani na wanaiona haitoshi kutushibisha wote, hivyo kwa njaa zao ndio maana unawaona wanajilimbikiza mali kabla hazijaisha. Washibe wao kwanza lakini kama tungeweza kuzalisha zaidi na kuuza zaidi kuifanya keki yetu iwe kubwa huu ulafi wao usingekuwepo leo mezani.

Kama nilivyosema hapo awali ninaamini hakuna mtu anayezaliwa tajiri, Mwenyezi Mungu kaiumba dunia hi ina kila aina ya opportunities ambazo zinaweza mtajirisha binadamu yeyote kama atafuata utaratibu fulani wa kutafuta riziki hizi na zipo kila sehemu hata Jangwani, msituni au baharini. Na dunia nzima kwa ujumla wake ni TAJIRI kila kipande cha ardhi, bahari, maziwa na mito kina thamani kubwa sana kulingana na mahitaji ya kibinadamu. Tena naweza kusema Bahari ambayo haina watu ni tajiri kuliko ardhi tupu...lakini sivyo, ila ni sisi wanadamu tunao thaminisha Utajiri na Umaskini wa nchi kutokana na watu wake. Hivyo hakuna nchi maskini na sidhani kama unaweza kunambia nchi hata moja ambayo mwenyezi Mungu kaifanya maskini kiasi kwamba hata watu wake ni maskini - Hakuna.

Umaskini unatokana na kushindwa kutumia fursa tulopewa na mwenyezi Mungu, maadam sisi tumeshindwa kuzi thaminisha rasilimali tulizojaaliwa basi huu ndio umaskini wenyewe. Na nikatoa mfano wa nchi kama Saudia ama tazama nchi zote za jangwa hizi huwezi kusema wao ni matajiri kwa sababu wana mafuta, ingekuwa hivyo basi hata Nigeria ingekuwa tajiri kuliko hata Bahrain, Qatar au Saudia maana tusikimbie ukweli kwamba ni WATU wanaoutengeza utajiri. Sii Nigeria au Saudia inayouza mafuta, inayoweka mikataba na kadhalika bali ni watu wake. Hata yule maskini ombaomba mtaani ukimtazama historia ya maisha yake utakuta kwamba aidha alinyimwa fursa au alishindwa kuitumia fursa za utajirisho.

Sasa unaposema hatuwezi kusema Nigeria sio maskini hali ni maskini kwa sababu umechukua mafuta kama thaminisho la nchi basi hivyo hivyo hakuna nchi duniani ambayo ni maskini isipokuwa WATU wake ndio maskini..Kwa nini tunaepa ukweli huu kuamini kwamba sisi ni maskini na tunahitaji kufanya mageuzi ktk maamuzi, fikra zetu ili nasi tupate kuitwa matajiri. Botswana nchi ambayo 3/4 ni jangwa hawana utajiri hata wakulinganisha na mkoa wa Arusha tu lakini tazama walivyoweza kuibadilisha nchi hiyo miaka 25 tu iliyopita...

Nadhani mahala napokubaliana nawe sana ni ktk kuonyesha sababu za kukwama kwetu ambazo zimeonyesha wazi kwamba kilicho mbele ya yote ni 1. UFISADI (ulafi wa viongozi ktk mgao wa keki) 2. Uzembe wa wananchi ktk uwekezaji na Uzalishaji 3. Tunaokoteza vya majalala (cheap import products kutoka China na India) - Shukran sana maana haya yanajaza gap iliyopo juu ya hoja ya umaskini wetu na nadhani hii inatupa picha ya mtazamo wa ndani kama alivyoainisha Mchunguzi na ningependa sasa hivi turudi nyuma tukusanye mawazo yote ya umaskini wetu toka sababu na vyanzo vya NDANI na kuviweka ktk orodha ili tupate kuvijadili na jinsi gani tunaweza kupambana navyo bila kusahau sisi WATU ni wananchi wa aina gani kama alivyo tuwekea FaizaFoxy hapo nyuma..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…