Hivi kweli unaamini miaka 120 ndio itakayotuwezesha sisi kuondokana na umaskini?.. Hujafikira kwamba ifikapo miaka hiyo 120 ndio sisi tutakuwa kama Malaysia ya leo wakati wao wamefika dunia nyingine kabisa na bado tukaonekana maskini? Kama unakumbuka tulipopata Uhuru tulikuwa maskini leo miaka 50 bado maskini lakini zipo nchi zimefikia hatua ya kuendelea (developing) yaani wameisha jikwamua ktk Umaskini.Mkandara, kwanza nisamehe kwa kuwa nilipfunguwa nyuzi yako nikaanza kucheka, nimechaka kwa kuwa ni ndefu sana, sikipitia kwa kina yote nime "peruse" tu, lakini nn uhakika nimekuelewa.
Kwanza napenda ufahamu kuwa viongozi wanatokana na wananchi wanawatumikia. Ikiwa wananchi wajinga, wazembe, wavivu, waongo, wazandik, wachawi, mafataani, wapenda vya bure, omba omba, roho mbaya, husda, chuki, hawana uaminifu, wazikaji, matapeli, hawapendi wenzao wafanikiwe, wala rushwa na watowa rushwa, wazinzi, waficha maovu, wanaogopana, wanalindana uovu, na kila sifa mbaya uijuwayo.
Sasa fikiri. Hiyo ndio jamii ya Watanzania walivyo na hiyo ndivyo uongozi wa mwanzo ulivyoiacha ikawa hivyo kwa kuweka misingi mibovu na kutokujuwa walifanyalo na kuifanya nchi ni "lab" ya kufanyia majaribio. Hivyo ndivyo 90% ya Watanzania walivyo. Kuwabadilisha kwa haraka haraka si rahisi. Kubomoa ni rahisi kuliko kujenga. Nyumba inayojengwa miaka mitano mpaka 10 inabomolewa kwa dakika moja tu. Sisi tumebomolewa kwa miaka 24 mfululizo, chukuwa hiyo halafu kila mwaka mmoja tuliobomolewa uupe miaka mitano tu ya kutengeneza, itatuchukuwa kwa uchache miaka 120 toka tulipoanza kutengeneza, imepita miaka 26 toka matengezo yaanze bado tuna miaka 94 kwa uchache.
Usitegemee neema zote mpaka baadaa ya miaka hiyo kuanzia leo. Tunajitahidi na dalili zinaonekana na "improvements" zipo. Toka tulikuwa tunatowa wahitimu wachache wa vyuo vikuu sasa wamezidi maradufu, toka tuliwa tukitaka hata kwenda Mwanza tupite Kenya, sasa hakuna tena hilo. Toka ilikuwa hatuwezi kumiliki majumba, sasa tunaweza kumiliki majumba na maroshan. Tutafika, lakini hesabu zake ndio hizo.
Siku ntakayoona Tanzania kuna kiwanda cha kutengeza sindano za cherehani ndio siku ntajuwa sasa tunaanza kuendelea, kabla ya hapo ni bado kabisa.
Sasa tutaweza vipi jikwamua ktk umaskini kwa kukaa miaka mingi zaidi hali sisi ni wajinga, wazembe, wavivu, waongo, wazandik, wachawi,
mafataani, wapenda vya bure, omba omba, roho mbaya, husda, chuki, hawana uaminifu, wazikaji, matapeli, hawapendi wenzao wafanikiwe, wala rushwa na watowa rushwa, wazinzi, waficha maovu, wanaogopana, wanalindana uovu, na kila sifa mbaya uijuwayo...
Hapo nilipo bold umenigusa haswaaa! na ndipo napotaka tuzungumzie...