Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Mkandara, kwanza nisamehe kwa kuwa nilipfunguwa nyuzi yako nikaanza kucheka, nimechaka kwa kuwa ni ndefu sana, sikipitia kwa kina yote nime "peruse" tu, lakini nn uhakika nimekuelewa.

Kwanza napenda ufahamu kuwa viongozi wanatokana na wananchi wanawatumikia. Ikiwa wananchi wajinga, wazembe, wavivu, waongo, wazandik, wachawi, mafataani, wapenda vya bure, omba omba, roho mbaya, husda, chuki, hawana uaminifu, wazikaji, matapeli, hawapendi wenzao wafanikiwe, wala rushwa na watowa rushwa, wazinzi, waficha maovu, wanaogopana, wanalindana uovu, na kila sifa mbaya uijuwayo.

Sasa fikiri. Hiyo ndio jamii ya Watanzania walivyo na hiyo ndivyo uongozi wa mwanzo ulivyoiacha ikawa hivyo kwa kuweka misingi mibovu na kutokujuwa walifanyalo na kuifanya nchi ni "lab" ya kufanyia majaribio. Hivyo ndivyo 90% ya Watanzania walivyo. Kuwabadilisha kwa haraka haraka si rahisi. Kubomoa ni rahisi kuliko kujenga. Nyumba inayojengwa miaka mitano mpaka 10 inabomolewa kwa dakika moja tu. Sisi tumebomolewa kwa miaka 24 mfululizo, chukuwa hiyo halafu kila mwaka mmoja tuliobomolewa uupe miaka mitano tu ya kutengeneza, itatuchukuwa kwa uchache miaka 120 toka tulipoanza kutengeneza, imepita miaka 26 toka matengezo yaanze bado tuna miaka 94 kwa uchache.

Usitegemee neema zote mpaka baadaa ya miaka hiyo kuanzia leo. Tunajitahidi na dalili zinaonekana na "improvements" zipo. Toka tulikuwa tunatowa wahitimu wachache wa vyuo vikuu sasa wamezidi maradufu, toka tuliwa tukitaka hata kwenda Mwanza tupite Kenya, sasa hakuna tena hilo. Toka ilikuwa hatuwezi kumiliki majumba, sasa tunaweza kumiliki majumba na maroshan. Tutafika, lakini hesabu zake ndio hizo.

Siku ntakayoona Tanzania kuna kiwanda cha kutengeza sindano za cherehani ndio siku ntajuwa sasa tunaanza kuendelea, kabla ya hapo ni bado kabisa.
Hivi kweli unaamini miaka 120 ndio itakayotuwezesha sisi kuondokana na umaskini?.. Hujafikira kwamba ifikapo miaka hiyo 120 ndio sisi tutakuwa kama Malaysia ya leo wakati wao wamefika dunia nyingine kabisa na bado tukaonekana maskini? Kama unakumbuka tulipopata Uhuru tulikuwa maskini leo miaka 50 bado maskini lakini zipo nchi zimefikia hatua ya kuendelea (developing) yaani wameisha jikwamua ktk Umaskini.

Sasa tutaweza vipi jikwamua ktk umaskini kwa kukaa miaka mingi zaidi hali sisi ni wajinga, wazembe, wavivu, waongo, wazandik, wachawi,
mafataani, wapenda vya bure, omba omba, roho mbaya, husda, chuki, hawana uaminifu, wazikaji, matapeli, hawapendi wenzao wafanikiwe, wala rushwa na watowa rushwa, wazinzi, waficha maovu, wanaogopana, wanalindana uovu, na kila sifa mbaya uijuwayo...
Hapo nilipo bold umenigusa haswaaa! na ndipo napotaka tuzungumzie...
 
Siku ntakayoona Tanzania kuna kiwanda cha kutengeza sindano za cherehani ndio siku ntajuwa sasa tunaanza kuendelea, kabla ya hapo ni bado kabisa.

Hapa unaji contradict, kwani ni awamu moja tu ndiyo tunaifahamu ilijenga viwanda sio vya kiwango cha sindano tu, bali pia vifaa vikubwa zaidi vya uzalishaji. Pengine ungesema hivi: Siku ntakayoona Tanzania inarudisha viwanda kama enzi za Nyerere ndio siku ntajua sasa tunaanza 'tena' kuendelea, vinginevyo, kwa sasa, hakuna lolote la maana zaidi ya kilimo cha mvua na chota chota ya dhahabu.
 
Hivi kweli unaamini miaka 120 ndio itakayotuwezesha sisi kuondokana na umaskini?.. Hujafikira kwamba ifikapo miaka hiyo 120 ndio sisi tutakuwa kama Malaysia ya leo wakati wao wamefika dunia nyingine kabisa na bado tukaonekana maskini? Kama unakumbuka tulipopata Uhuru tulikuwa maskini leo miaka 50 bado maskini lakini zipo nchi zimefikia hatua ya kuendelea (developing) yaani wameisha jikwamua ktk Umaskini.

Sasa tutaweza vipi jikwamua ktk umaskini kwa kukaa miaka mingi zaidi hali sisi ni wajinga, wazembe, wavivu, waongo, wazandik, wachawi,
mafataani, wapenda vya bure, omba omba, roho mbaya, husda, chuki, hawana uaminifu, wazikaji, matapeli, hawapendi wenzao wafanikiwe, wala rushwa na watowa rushwa, wazinzi, waficha maovu, wanaogopana, wanalindana uovu, na kila sifa mbaya uijuwayo...

Hapo nilipo bold umenigusa haswaaa! na ndipo napotaka tuzungumzie...

Your point stimulates kitu kingine. Sote tunajua umuhimu wa diaspora remittance - fedha ambazo kwa mfano, watanzania walio nje wanatumia ndugu zao. Kwanini sisi tupo nyuma ya nchi nyingi sana Za Afrika? Kenya, Uganda, wametupita sana katika hili. Wakenya, Waganda, waliopo Canada huko kwako Mkandara, waliopo UK, USA, etc, kila mwaka wanatuma jumla ya dollar zaidi ya billioni moja; Sisi Tanzania hata nusu ya hizo hatutumi nyumbani. Na takwimu za WorldBank zinaonyesha kwamba, idadi ya fedha hizi kuja bara la afrika ni kubwa kuliko idadi ya Foreign Aid. Fedha hizi za waafrika waliopo nje wanaotumia ndugu zao, wingi wake umepitwa na Foreign Direct Investment Pekee, then second ndio hizi fedha, na third ni Foreign Aid. Na hizi ni jumla ya fedha watu wanazotuma western union n.k.

Kwanini sisi watanzania tupo nyuma katika hili? hatupendi ndugu zetu nyumbani wafanikiwe? tuna roho mbaya? Kwanini waganda, wakenya wanatupita katika hili? Wataalam wanasema kwamba impact ya fedha hizi ni kubwa kuliko ile ya Foreign Aid kwani unlike foreign aid ambayo ina matatizo mengi kama masharti ya WorldBank jinsi gani ya kuzitumia, ubadhirifu na ufisadi wa viongzi wetu n.k, diaspora remittances - fedha zinazotumwa na watanzania waliopo mfano wa Ulaya, Marekani kuja Tanzania zinaenda moja kwa moja kwa mlengwa na nyingi husaidia familia zao in terms of ada za shule, matibabu, lakini pia zinanunua viwanja, baiskeli, zinajenga nyumba n.k.

Hata hapa kwetu Tanzania, ni kabila moja tu ndio lenye tabia ya kujali kwao - nao ni wachaga. Hawa kwao kuna maendeleo kutokana na utamaduni wao wa kutuma fedha makwao, kuanzisha miradi makwao, kujenga n.k. Lakini wanyakyusa, wahehe, wanyamwezi, wahaya, wabondei, wasukuma, wakurya, wangoni, n.k, wengi wao hawafanyi hivyo. Ina maana makabila mengine hawana uwezo wa fedha kama wachaga? Au wana roho mbaya au ni hawana moyo wa kizalendo kwa ndugu zao huko mikoani? Makabila mengi, kipimo cha mafanikio yao ni matumizi Dar-es-salaam.
 
Je, unaweza kutenganisha internal factors na external factos kama source za mafanikio hayo unayoyataja?

Na je, haya anayoyataja Mwanakijiji kama njia sahihi ya kutafsiri maana ya umaskini:
a. Kukosa Nafasi (opportunity)
b. Kukosa Haki (right and justice)
c. Kukosa Usawa (equality of dignity as well as that of opportunity)
d. Kukosa Kutumia (USE)

Je, una maoni gani juu ya haya in the context ya hiyo miaka 24 ambayo nadhani unamzungumzia BABA WA TAIFA na pia miaka baada ya BABA WA TAIFA kung'atuka?

Hayo yote ni pumba za Mwanakijiji za kawaida, kama humjui utaona unasoma cha maana kumbe hakina lolote.

Nani aliosema hayo hakuna Tanzania? Opportunities zilizopo hapa hakuna nchi yoyote duniani nilizozikuta kama hizo. Na nimetembea sana tu duniani. Leo aniambie yeye ni haki ipi aliyoikosa hapa Tanzania ambayo kwingine kaipata. Usawa? unaongelea usawa zaidi ya wapi? au chini ya wapi? nini comparison basis zake?

Watanzania ni wepesi sana wa kutupia mpira kwingine na wa kutunga sababu za kushindwa, yote ni uvivu.

Mimi nakwambia kama kuna land of opportunity kwa sasa duniani, basi Tanzania inaongoza. Labda mtu uwe mvivu wa kutupa na hauna muono hata wa kutazama hatua kumi mbele na hayo ndio Watanzania wengi hawana.
 
Hapa unaji contradict, kwani ni awamu moja tu ndiyo tunaifahamu ilijenga viwanda sio vya kiwango cha sindano tu, bali pia vifaa vikubwa zaidi vya uzalishaji. Pengine ungesema hivi: Siku ntakayoona Tanzania inarudisha viwanda kama enzi za Nyerere ndio siku ntajua sasa tunaanza 'tena' kuendelea, vinginevyo, kwa sasa, hakuna lolote la maana zaidi ya kilimo cha mvua na chota chota ya dhahabu.

Hujanielewa. Nimesema kiwanda cha sindano za charahani. Na siongelei viwanda vya Nyerere vilivyokufa toka mwenyewe yuko hai. Ambavyo havikutusaidia chochote zaidi ya kutuongezea umaskini.

Nnapotaja hicho kiwanda cha sindano nna maana kubwa sana. Nichambulie kidogo kabla ya kuweka kiwanda inatakiwa ufanye nini, ukifanya hivyo unaweza kunielewa nna maanisha nini.
 
Mkuu Kuongezea tu, Hiyo $1.5 B USD might be 10% of the true value of the Gold mined due to transfer pricing. that is the companies sell the products to subsidiary entities at the fraction of the price to pay low taxes in the country of origin...
...Kwa sababu ya kuwa na Viongozi wabovu ambao wanagawa rasilimali (Dhahabu, Almasi, Uranium, Tanzanite, misitu, Wanyama, ardhi n.k) za nchi kwa wachukuaji katika bei ya kutupa mwaka nenda mwaka rudi.

Haingii akilini kabisa nchi yenye utajiri mkubwa kama ya kwetu ishindwe kulipa hata mishahara ya Wafanyakazi wake. Mwaka 2010 mapato ya dhahabu yetu yalikuwa $1.5 billion lakini tulichoambulia hapo ni kidogo sana lakini hao wanaojiita Viongozi hawaoni kabisa tatizo la kugawa utajiri wetu wa nchi huku aslimia kubwa ya wananchi wakiwa wanaishi katika maisha yaliojaa ufukara wa kutisha!!! Shamba la bibi hilo wacha wavunaji wajichukulie.
 
Hivi kweli unaamini miaka 120 ndio itakayotuwezesha sisi kuondokana na umaskini?.. Hujafikira kwamba ifikapo miaka hiyo 120 ndio sisi tutakuwa kama Malaysia ya leo wakati wao wamefika dunia nyingine kabisa na bado tukaonekana maskini? Kama unakumbuka tulipopata Uhuru tulikuwa maskini leo miaka 50 bado maskini lakini zipo nchi zimefikia hatua ya kuendelea (developing) yaani wameisha jikwamua ktk Umaskini.

Sasa tutaweza vipi jikwamua ktk umaskini kwa kukaa miaka mingi zaidi hali sisi ni wajinga, wazembe, wavivu, waongo, wazandik, wachawi,
mafataani, wapenda vya bure, omba omba, roho mbaya, husda, chuki, hawana uaminifu, wazikaji, matapeli, hawapendi wenzao wafanikiwe, wala rushwa na watowa rushwa, wazinzi, waficha maovu, wanaogopana, wanalindana uovu, na kila sifa mbaya uijuwayo...
Hapo nilipo bold umenigusa haswaaa! na ndipo napotaka tuzungumzie...

Tulipopata Uhuru hatukuwa maskini, nani aliokudanganya? tulipopata uhuru tulikuwa the largest exporters of agriculture products in Africa. Tukabomolewa. Na nani? unamjuwa sana.

Miaka 24 baada ya Uhuru tukawa the largest importer wa misaada katika Afrika.

Kuhusu miaka 94 na Malaysia hapana, tutakuwa sawa au kupita wao kwa siku hizo. Kabla ya hapo no way, hiyo ni kwa uchache.
 
Your point stimulates kitu kingine. Sote tunajua umuhimu wa diaspora remittance - fedha ambazo kwa mfano, watanzania walio nje wanatumia ndugu zao. Kwanini sisi tupo nyuma ya nchi nyingi sana Za Afrika? Kenya, Uganda, wametupita sana katika hili. Wakenya, Waganda, waliopo Canada huko kwako Mkandara, waliopo UK, USA, etc, kila mwaka wanatuma jumla ya dollar zaidi ya billioni moja; Sisi Tanzania hata nusu ya hizo hatutumi nyumbani. Na takwimu za WorldBank zinaonyesha kwamba, idadi ya fedha hizi kuja bara la afrika ni kubwa kuliko idadi ya Foreign Aid. Fedha hizi za waafrika waliopo nje wanaotumia ndugu zao, wingi wake umepitwa na Foreign Direct Investment Pekee, then second ndio hizi fedha, na third ni Foreign Aid. Na hizi ni jumla ya fedha watu wanazotuma western union n.k.

Kwanini sisi watanzania tupo nyuma katika hili? hatupendi ndugu zetu nyumbani wafanikiwe? tuna roho mbaya? Kwanini waganda, wakenya wanatupita katika hili? Wataalam wanasema kwamba impact ya fedha hizi ni kubwa kuliko ile ya Foreign Aid kwani unlike foreign aid ambayo ina matatizo mengi kama masharti ya WorldBank jinsi gani ya kuzitumia, ubadhirifu na ufisadi wa viongzi wetu n.k, diaspora remittances - fedha zinazotumwa na watanzania waliopo mfano wa Ulaya, Marekani kuja Tanzania zinaenda moja kwa moja kwa mlengwa na nyingi husaidia familia zao in terms of ada za shule, matibabu, lakini pia zinanunua viwanja, baiskeli, zinajenga nyumba n.k.

Hata hapa kwetu Tanzania, ni kabila moja tu ndio lenye tabia ya kujali kwao - nao ni wachaga. Hawa kwao kuna maendeleo kutokana na utamaduni wao wa kutuma fedha makwao, kuanzisha miradi makwao, kujenga n.k. Lakini wanyakyusa, wahehe, wanyamwezi, wahaya, wabondei, wasukuma, wakurya, wangoni, n.k, wengi wao hawafanyi hivyo. Ina maana makabila mengine hawana uwezo wa fedha kama wachaga? Au wana roho mbaya au ni hawana moyo wa kizalendo kwa ndugu zao huko mikoani? Makabila mengi, kipimo cha mafanikio yao ni matumizi Dar-es-salaam.

Hizo nchi wana export manpower sisi tunatafuta manpower hatuna. Hawa Watanzania wanaokwenda nje ni kwa njia zao wenyewe tu lakini sio kwa kuwa tuna Industry ya ku Export Manpower. Hatuna.
 
Hizo nchi wana export manpower sisi tunatafuta manpower hatuna. Hawa Watanzania wanaokwenda nje ni kwa njia zao wenyewe tu lakini sio kwa kuwa tuna Industry ya ku Export Manpower. Hatuna.

Kwa nini hatuna industry ya kuexport manpower?
 
Your point stimulates kitu kingine. Sote tunajua umuhimu wa diaspora remittance - fedha ambazo kwa mfano, watanzania walio nje wanatumia ndugu zao. Kwanini sisi tupo nyuma ya nchi nyingi sana Za Afrika? Kenya, Uganda, wametupita sana katika hili. Wakenya, Waganda, waliopo Canada huko kwako Mkandara, waliopo UK, USA, etc, kila mwaka wanatuma jumla ya dollar zaidi ya billioni moja; Sisi Tanzania hata nusu ya hizo hatutumi nyumbani. Na takwimu za WorldBank zinaonyesha kwamba, idadi ya fedha hizi kuja bara la afrika ni kubwa kuliko idadi ya Foreign Aid. Fedha hizi za waafrika waliopo nje wanaotumia ndugu zao, wingi wake umepitwa na Foreign Direct Investment Pekee, then second ndio hizi fedha, na third ni Foreign Aid. Na hizi ni jumla ya fedha watu wanazotuma western union n.k.

Kwanini sisi watanzania tupo nyuma katika hili? hatupendi ndugu zetu nyumbani wafanikiwe? tuna roho mbaya? Kwanini waganda, wakenya wanatupita katika hili? Wataalam wanasema kwamba impact ya fedha hizi ni kubwa kuliko ile ya Foreign Aid kwani unlike foreign aid ambayo ina matatizo mengi kama masharti ya WorldBank jinsi gani ya kuzitumia, ubadhirifu na ufisadi wa viongzi wetu n.k, diaspora remittances - fedha zinazotumwa na watanzania waliopo mfano wa Ulaya, Marekani kuja Tanzania zinaenda moja kwa moja kwa mlengwa na nyingi husaidia familia zao in terms of ada za shule, matibabu, lakini pia zinanunua viwanja, baiskeli, zinajenga nyumba n.k.

Hata hapa kwetu Tanzania, ni kabila moja tu ndio lenye tabia ya kujali kwao - nao ni wachaga. Hawa kwao kuna maendeleo kutokana na utamaduni wao wa kutuma fedha makwao, kuanzisha miradi makwao, kujenga n.k. Lakini wanyakyusa, wahehe, wanyamwezi, wahaya, wabondei, wasukuma, wakurya, wangoni, n.k, wengi wao hawafanyi hivyo. Ina maana makabila mengine hawana uwezo wa fedha kama wachaga? Au wana roho mbaya au ni hawana moyo wa kizalendo kwa ndugu zao huko mikoani? Makabila mengi, kipimo cha mafanikio yao ni matumizi Dar-es-salaam.

Wadau, what if the minerals mined here are sold in TZS to strengthen the currency and make petrolium imports cheaper?
 
Naomba niseme machache kuhusiana na Mtazamo wa Nje na Umaskini Wetu. Ni muhimu tutakumbuka kwamba Maendeleo katika dunia ya leo ni matokeo ya vitu viwili: Moja ni Vita; na Pili ni Uporaji wa rasilimali kupitia ukoloni na ukoloni mamboleo. Hata Marekani imefanikiwa kuwa taifa kubwa kijeshi na kiuchumi kutokana na vita vya dunia vilivyopita kwani, kwa vile yeye hakupigana sana/moja kwa moja, vita vya dunia vilimfungulia biashara kubwa vyakula, silaha, nguo, n.k katika nchi zilizokuwa vitani (nchi za ulaya), kwani nchi zilizokuwa vitani wakati ule, hazikuweza kuzalisha viwandani mwao. Vinginevyo kabla ya vita vya kwanza vya dunia, Marekani haikuwa hata katika kumi bora ya nchi tajiri duniani – in terms of GDP. Lakini since then, marekani imekuwa inatawala dunia. Sasa, ili utawala wake uendelee, "Foreign Policy" inayolinda maslahi ya Marekani ikawa (na bado ni hivyo leo hii) ni muhimu sana. Na hivi ndivyo nchi kama Japan, South Korea, Malaysia n.k, zilikuja kupaa kiuchumi, tofauti na wengi kufikiria kwamba mafanikio ya hizi nchi ni matokeo ya juhudi zao pekee. Nchi hizi zimeendelea chini ya "Guided Capitalism", sio soko huria kama tunaloambiwa Tanzania tulifuate leo.

Kilichoinua South Korea, Malaysia, Singapore, n.k, ni Cold War. Kwa mfano, baada ya vita vikuu vya pili kuisha, marekani ilitambua umuhimu wa Japan, hivyo kumtengenezea masingira mazuri ya kufanya biashara na marekani ili asivutike na Soviet Union. Ndio maana Japan akainuka sana, akanogewa sana na ubepari, na akawa hataki kabisa kusikia kitu kinaitwa Soviet Union. Lakini marekani akaona hiyo haitoshi, South Korea, Malaysia, Singapore na wengineo maeneo yale, kama wasipothibitiwa, watavutiwa Soviet Union na kuwa kama North Korea, Vietnam n.k. Hivyo Marekani akaendeleza Foreign Policy yake kushughulikia wakina South Korea n.k, ili wavutiwe na utamaduni pamoja na faida za ubepari, na waone Ukomunisti sio mali kitu. Wanasiasa wa South Korea kwa mfano, ndio walipewa jukumu la kuendesha ujarisiamali huu chini ya State Capitalism. Uzuri wa hawa watu ni kwamba, walikuwa wazalendo na walitaka nchi zao ziendelee, hivyo wakatumia fursa hii kikamilifu kujenga miundo mbinu, kuendeleza Sayansi na Teknolojia, Elimu, Afya n.k. Kama ilivyokuwa kwa Japan, South Korea na wengine pia wakapewa 100% access ya soko la marekani, kuuza bidhaa zao, kama njia ya kuwanogesha zaidi na Ubepari, na waone ukomunisti ni kama Ukoma.

Afrika hapakuwa na tishio lolote la maana, hasa kwa kuona kwamba Kaburu yupo, na ana mabomu ya nuclear to act as a deterrent against any activity za mkomunisti Afrika. Kwahiyo jukumu la kulinda maslahi yao Afrika akapewa kaburu. Lakini kwa bahati mbaya au nzuri, ukombozi Afrika ya Kusini ulitokea muda mmoja pamoja na kifo cha Soviet Union, vinginevyo kama Soviet ingeendelea kuwepo, na Afrika Kusini imekuwa huru na chini ya Mandela, taratibu tungeanza kuona Marekani akitafuta maeneo Afrika ya kuyaendeleza kama South Korea ili kujenga military bases zao kujilinda na ukomunisti, kuzipa nchi hizi 100% access ya bidhaa zao kuingia Marekani, n.k. Nchi zenye rasilimali Africa kama Tanzania, Zaire, Ghana, Zimbabwe, Angola.. zingekuwa "New African Tigers". Tukumbuke kwamba Chama Cha ANC kina orientation ya kijamaa, na ndio maana Marekani akahakikisha kwamba Afrika ya Kusini inaachana na mabomu ya nuclear baada ya uhuru.

Lakini mambo yameanza kubadilika tena, kwani China anaanza kuwatishia wakubwa wa magharibi na kuzalisha a new cold war. Hivi sasa, Wamarekani wanaiangalia China kwa jicho la karibu sana. Safari ya majuzi ya Hillary Clinton kuja Tanzania, Zambia n.k, ililenga kuja kuongea na Marais wetu kuhusu China. Ndio maana taratibu tutaanza kuona Marekani akianza ku-commit rasilimali na fedha zake nyingi sana katika nchi fulani fulani za Afrika, ili zione China ni kama ukoma. Tanzania tupo kwenye orodha hiyo, pamoja na wengine. Kuna miradi mingi sana inaendelea chini kwa chini ya kijeshi na kiuchumi.

Suala la kujiuliza hapa ni kwamba, kwavile wakubwa hawa hatuna uwezo wa kushindana nao katika hili, iwapo dunia itarudi tena kwenye vita baridi, na iwapo Tanzania tutakuwa moja ya nchi ambazo wakubwa watakuwa na interest nazo, JE, viongozi wetu wasisitize lipi la muhimu zaidi kutoka kwa wakubwa hawa?
  1. Trade – More access ya bidhaa zetu kwenye masoko ya US & EU?
  2. Aid – More Aid?
  3. Foreign Direct Investment – More FDI?
Hatuwezi pata vyote kwa uwiano tunaoutaka, lakini tunaweza chagua kimoja na ku negotiate vizuri na wakubwa ili chochote kile tutakachochagua kiwe na masharti tutakayoyataka sisi, sio wao.
 
Hujanielewa. Nimesema kiwanda cha sindano za charahani. Na siongelei viwanda vya Nyerere vilivyokufa toka mwenyewe yuko hai. Ambavyo havikutusaidia chochote zaidi ya kutuongezea umaskini.

Nnapotaja hicho kiwanda cha sindano nna maana kubwa sana. Nichambulie kidogo kabla ya kuweka kiwanda inatakiwa ufanye nini, ukifanya hivyo unaweza kunielewa nna maanisha nini.

Kwavile unatambua kwamba tokea Nyerere amevijenga viwanda hivi, ambavyo vilikufa akiwa hai kama unavyosema, kwanini awamu zilizofuatia hazijaweza jenga viwanda vingine? Wakubwa wanapotuonya kwamba ukosefu wa ajira kwa vijana ni 'timing bomb', kwanini hawategui bomu hili kwa kuanzisha viwanda? Kama vile vya nyerere vya Mwatex, Kiltex, Kilimanjaro Machine Tools, n.k vilivyotoa ajira nyingi sana kwa vijana miaka ile?
 
Tunajikita sana katika kutupia lawama wengine, lawama za nyerere zibekie kwenye historia, chakuangalia ni lawama za sasa na jinsi ya kujikomboa, njia za kujikomboa na namna za kujitoa kwenye umaskini. Kwa maana hiyo challenges zilizopo ni donors conditions, home policies and a sound approach to get out of the messy politics. Sitegemei mwanasiasa aje na mbinu nategemea wale jamaa wanaoojiita wasomi waje na solution baada ya kuangalia effects za outside world and what has to be implemented in order for us to advance. Sio tu kukariri hapa kunaitajika ubunifu maana msaada unahitajika na policies zetu zinahitajika therefore what do we have to do in our part?
 
Mkuu Mkandara, binafsi I disagree with the thesis framework. In my opinion the thesis should have been " Why is Tanzania rich, but the people do not benefit from its riches"

Haiwezekani nchi yenye Tanzanite ( The only one in the world), Gold ( one of the major producers in Africa), Diamond, Uranium, Natural Gas, Game Reserves ( Serengeti, Mikumi nk), Arable Land, population over 40 million, Major ports with landlocked countries as neighbors nk, NCHI HIYO IITWE MASKINI.....

Kusema Tanzania ni maskini ni ujinga tuliolishwa na wakoloni ambao viongozi wetu wanaamini bila kufikiria.

Tanzania ni underdeveloped, hiyo nakubali
Tanzania wananchi wake utajiri wa nchi unawapita pembeni, hiyo nakubali
Tanzania, resources zinaibwa na wajanja, hiyo nakubali
Tanzania, viongozi wameweka sera mbovu zinazoweka leakages za mapato zaidi ya $10Billion per yr, hiyo nakubali
Tanzania, wananchi na wafanyabiashara hawainvest kwenye manufacturing ambayo ingeongeza uchumi kwa haraka, hiyo nakubali
Tanzania, ni dampo la bidhaa cheap kutoka China zinazoua kabisa ability ya kuwa manufacturing power house, hiyo nakubali
Tanzania, budget yetu haiweki kipaumbele kwenye DEVELOPMENT ( Ni aibu hata kuweka % ya budget inayokwenda kwenye Dev)

NK NK NK NK

Kwa hiyo in concluding ni kuwa UMASKINI WETU sio wa UKWELI in real terms, NI WA KUJITAKIA, ni kama vile Saudi Arabia OIL inawasaidia wanachi wake kuwa na utajiri, lakini NIGERIA OIL haiwasaidii wananchi wake kuondokana na umaskini, lakini huwezi kusema Nigeria ni maskini. Kwa hiyo in SHORT, TATIZO NI Namna keki inavyogawanjwa na sio ukosefu wa keki.

Tanzania kama Rais angekuwa KAGAME, ndio tungejua ukweli wa UTAJIRI WETU, lakini hapa tulipo ni miujiza ya Mwenyezi Mungu tu ndio inayoweza kutukomboa in the near future sababu UONGOZI HAKUNA, SERA za UCHUMI ni MBOVU zinawabenefit wajanja na foreigners, MANUFACTURING BASE HAKUNA, KILIMO kinapewa LIP SERVICE NK

May God Bless Tanzania.
 
Tunajikita sana katika kutupia lawama wengine, lawama za nyerere zibekie kwenye historia, chakuangalia ni lawama za sasa na jinsi ya kujikomboa, njia za kujikomboa na namna za kujitoa kwenye umaskini. Kwa maana hiyo challenges zilizopo ni donors conditions, home policies and a sound approach to get out of politics. Sitegemei mwanasiasa aje na mbinu nategemea wale jamaa wanaoojiita wasomi waje na solution baada ya kuangalia effects za outside world and what has to be implemented in order for us to advance. Sio tu kukariri hapa kunaitajika ubunifu maana msaada unahitajika na policies zetu zinahitajika therefore what do we need to do in our part?

Sell Gold, Diamonds & Tanzanite in TZS to strengthen the currency and reduce the price of imported petrol?
 
Watanzania kwa ujumla wake hatujitambui,hatujui sisi ni nani,tunatofautiana vipi na watu wengine,tuna malengo gani,na tuyaendee vipi malengo yetu kwa mujibu wa uhalisia wetu.

Even identical twins are not exactly the same,the same applies: asili yetu,nchi yetu,historia yetu,..haifanani na wengine/zingine.
Kwa mfano,China yenyewe ni "civilization state" na siyo "national state" kama zilivyo western countries,kwa maana kwamba huwezi kuwa mchina unless you are Chinese,lakini unaweza kuwa Canadian just by nationality...na ndo maana kama tunataka kuelewa China in western perspective utakuwa unatwanga maji kwenye kinu.

Nchi nyingi zinazoendelea barani Asia zina misingi kama ya China.Wanajitambua wao ni nani na wanataka nini,na njia ipi MUAFAKA/MAALUM kwa mujibu wao walivyo itumike kufikia lengo.

Lengo ni kujiondoa katika umaskini,tukichukulia nchi za Asia kama mfano,waliatambua kuwa jamii inahitaji elimu ili kujikomboa na ujinga from which itakuwa ni template ya kuweka mambo mengine sawa,na walielewa wazi kwamba ili elimu iwe rahisi kwa jamii inatakiwa itolewe kwa lugha yao ya taifa,walichokifanya ni ku translate materials kutoka katika lugha mbalimbali duniani na kupeleka katika lugha zao,pia kupeleka wasomi nchi zilizoendelea na kurudi nyumbani kuleta maendeleo.Uzuri ni kwmba Kiingereza ni rahisi kujifunza kuliko lugha zao,hivyo wao ni rahisi kuisoma west lakini west ni ngumu kusoma wao.Literacy rate ya China ni above 90%,computer applications zipo kwa Kichina,yeyote anayejua kusoma anaweza ku access

FaizaFoxy
Mathematical description uliyotoa is not relevant when it comes to development,in eighties,Kenya ilikuwa inapeleka msaada wa chakula South Korea,angalia wa Korea wako wapi sasa hivi.China imeanza kufanya economical reform 30 years ago...suala la msingi ni kujitambua who are we,our current status,the world status...what shud we do in our own perspective to reach the very same goal....ofcourse it will with cost...kama China,ukileta magumashi unanua risasi mwenyewe...na kuwa excluded

Mkandara
Kwa nini Tanzania ni maskini: Kwa sababu hatujitambui sisi ni nani kama taifa,hatutambui misingi yetu kama taifa hivyo hatuji tuchukue hatua ipi stahiki kujikwamua na hali hii ya umaskini.
 
Tulipopata Uhuru hatukuwa maskini, nani aliokudanganya? tulipopata uhuru tulikuwa the largest exporters of agriculture products in Africa. Tukabomolewa. Na nani? unamjuwa sana.

Miaka 24 baada ya Uhuru tukawa the largest importer wa misaada katika Afrika.

Kuhusu miaka 94 na Malaysia hapana, tutakuwa sawa au kupita wao kwa siku hizo. Kabla ya hapo no way, hiyo ni kwa uchache.

Ni muhimu ukarudia kuzitazama tena takwimu zako. Tanzania mwaka 1961 ilikuwa ni moja ya nchi maskini kuliko zote za Afrika kwa sababu kadhaa, moja ikiwa ni kwamba Mjerumani alikaa muda mfupi sana kwahiyo hakupata muda wa kuendeleza uchumi, miundo mbinu n.k. Mwingereza akachukua tanganyika toka kwa mjerumani, lakini tofauti na Kenya kwa mfano, sisi hatukuwa koloni per se chini ya mwingereza, bali protectorate, kwahiyo mwingereza hakuwa na interest sana na tanganyika, ukifananisha na kenya, zimbabwe n.k, ambako alidhania ataishi kule milele - kumbuka maeneo kama Zimbabwe, Kenya, yalikuwa ni settler economies; sasa how can a protectorate under plantations export more than settler economies?

Literature yote inayozungumzia historia ya uchumi wa Tanganyika inaelezea kwa kirefu sana jinsi gani Tanganyika ilibakia nyuma kimaendeleo kutokana na sababu hizi. Na hata moja ya sababu kubwa za kufa kwa jumuiya ya afrika mashariki wakati ule ni kutokana na Tanzania kuona itapunjwa, kwani Kenya walikuwa mbali sana kiuchumi, hata kabla ya Ujamaa Tanzania.
 
Sell Gold, Diamonds & Tanzanite in TZS to strengthen the currency and reduce the price of imported petrol?
Unless you're thinking we have enough mineral resources to fund an expensive welfare system, the proposal is valid other wise we still do need to find means to make 46million happy. That requires creating employment (through a command or market economy), technological advances and a better way to utilize our resources. All those challenges need to be addressed in relation with the current context of global and home politics, finance, economical approaches etc, etc etc ........
 
what I mean is to start to exploit the true value of the mineral deposits and of course invest the proceeds to buy fuel which will be relatively cheaper than prices paid today, re-vamp education, health, infrastructure, agriculture and so on. This would result in the government being able to run its affairs independent of foreign aid?...
 
Wadau, what if the minerals mined here are sold in TZS to strengthen the currency and make petrolium imports cheaper?

The US Dollar ndio major trading currency duniani kwa sababu ipo more stable na kwa ushahidi wa kihistoria, kwahiyo mataifa mengi sana (tajiri na maskini)lingependa kuwa na reserve ya dollars kuliko their own currency ambazo value zake hazitabiriki kesho zitakuwa vipi. Hata nyumbani Tanzania, mtu upo more comfortable kuwa na a dollar account kama una uwezo kuliko a T.sh account kwani unlike T.sh account, ambazo thamani yake sana sana itashuka siku zinavyozidi kwenda mbele, dollar thamani yake itabakia pale pale if not kuongezeka.

Lakini swali lako linalenga kuzuri - to strengthen shillingi yetu; lakini ujue pia kwamba, Gold yetu inakuwa exported ikiwa rough, not processed; hawa wazungu wajanja sana; huko kwao, ukipeleka processed gold, wanakuchaji kodi kubwa sana, nia yao ikiwa kuhakikisha kwamba processing inafanyika kwao ili kutoa ajira n.k.

One of the best ways za ku strengthen our currency ni kuongeza mahitaji ya shillingi katika uchumi; mfano, Kenyan shilling ina nguvu kwasababu ukiwa mle ndani, hauhitaji dollar, lakini hapa kwetu, kodi za nyumba inachajiwa kwa dollar, tarriff za simu zinachajiwa kwa dollar, kodi za wawekezaji kwa dollar, hoteli zinachajiwa kwa dollar; nguo madukani, kina dada na kina kaka wanaenda kutuletea kutoka china kwa kutumia dolllar; Panadol za kenya, zinafuatwa kule na dollar, sio shillingi; BlueBand hivyo hivyo, kwahiyo unakuta mwisho wa siku, watanzania wenyewe tunaitupa shilllingi kwenye pipa la taka in exchange for a dollar, hivyo kushusha thamani ya sarafu yetu. Na sasahivi hata kununua juice ya bhakheresa dukani na kulipia shilllingi elf tatu, dollar imetumika kuifikisha pale dukani kwani kutokanana uhaba wa matunda Tanzania, Bhakhera ananunua matunda nje kwa dollar, na kuja kututengezea juisi humu; Kenya mambo yao mengi sana wanajitosheleza wenyewe kwani wana viwanda vingi vya basic goods, kwahiyo hawahitaji kutupa shillingi yao ya kenya kwenye pipa, ili impatie dollar akalete dawa za kichwa, dawa za kuua mende kutoka nje; Sisi hata maumivu ya kichwa, hata siagi, hatuna viwanda vya nyumbani vya kutuwezesha kutumia dollar kuvifuata katika maduka yetu, bali kubadilisha shillingi into dollars ili tuvuka mpaka wa kenya kwenda kununua vitu hivi; Mwisho wa siku shillingi inakua useless, whether kwa kujijua au kutojijua.
 
Back
Top Bottom