Hapo sio sahihi, Mjerumani aliwekeza reli inayopita sehemu zote muhimu, kulikuwa kuna central, south na north Routes. Mwingereza aliirithi reli na akahakikisha inafanya kazi vizuri kabisa, na wakati tunachukuwa Uhuru, kulikuwa kuna reli kila siku ya kwenda Mwanza, ya kwenda Tanga, Ya kwenda Arusha na ya kwenda mpaka Kenya. Ambapo hakuna reli kulikuwa kuna mabasi ya Railway na magari ya mizigo ya railway. Barabara ingawa zilikwa si za lami lakini wakati tunachukuwa Uhuru barabara zote kubwa zilikuwa zikipita misimu yote, si mvua si jua. Kulikuwa kuna PWD (Public Works Department) ikifanya kazi inavyotakiwa na mabarabara yote makuu yalikuwa na vituo vya TRM (Tanganyika Road Maintenance) hawa walikuwa wanahakikisha barabara zinapitika wakati wote.
Tanganyika haikuwa maskini wa mwisho, huo si ukweli kabisa, vipi uwe maskini wa mwisho wakati wa uhuru ambapo ulikuwa ndio exporter wa kwanza wa mazao ya shambani katika Afrika. Kumbuka katika Afrika nzima.
Ukweli ubaki kuwa ukweli, wakati anaondoka Nyerere kila kitu kilikuwa taabani. Nakumbuka sisi utotoni tukipanda treni kusafiri hadi unaona raha, vitanda vizuri, mashuka myeupe safi kabisa, chakula kizuri, hakuna kubanana, hakuna kuchelewa na ukienda Iringa hakuna reli unapanda basi la Railway. Aaaah, yule mzee katumaliza vibaya sana. Kila kitu kakiuwa, hakuna hata palipobaki na afadhali. Kubomowa ni rahisi kujenga ni tabu.
Ni miaka 120 tena hapo tusijidai ujanja, sisi wenyewe hatuwezi. Inabidi tupate wataalam wa uhakika kutoka huko walikoweza. La tunajidai kufanya wenyewe basi miaka 500 mingine, hata tusome tupindukie. Maawee! Kusoma pekee hakusaidii sana kunafuta baadhi ya ujinga lakini kuelimika ndio muhimu. Na kuelimika hakuji mkwa kusoma tu. Kuelimika kunakuja na "expirience".
Utashindana na mtu ambae ana Universities kwa miaka 800 iliyopita, wasomi wangapi wameyoka huko na wameacha "expience" ya kiasi gani, wewe ndio kwanza vyuo vyako vyote havijatiwa mpaka leo hata wahitimu 500,000 kwa miaka yoooote vilivyokuwepo. Halafu unafikiri utaweza tu? Maaaweee! Tazama wenzenu miaka yao vilipoanza vyuo vikuu:
The first universities in Europe with a form of corporate/guild structure were the
University of Bologna (1088), the
University of Paris (c. 1150, later associated with the
Sorbonne), the
University of Oxford (1167), the
University of Palencia (1208), the
University of Cambridge (1209), the
University of Salamanca (1218), the
University of Montpellier (1220), the
University of Padua (1222), the
University of Naples Federico II (1224), the
University of Toulouse (1229),[SUP]
[10][/SUP][SUP]
[11][/SUP] the
University of Siena (1240).