Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Attitude ya serikali kwa watanzania!Very negative!....kwa mfano; 1,Viwango vya riba ktk benki zetu ni juu mno...na serikali inaangalia tu! 2,Serikali haina mipango yeyote ya kuwawezesha wawekezaji wazawa....hata kauli za baadhi ya viongozi wetu ka mfano kuhusu gesi..eti kiongozi anadiriki kabisa kutoa kauli za kuudhi na kukatisha tamaa...hii inaonyesha wazi stinking attitude ya serikali yetu kwa wananchi wake. 3,...Wawekezaji wa nje hawjali maendeleo ya nchi...wanachojua ni kuchota rsilimali na kusepa zao...huku wakiacha umskini
 
Kwa mlinganyo wa kisekta, kilimo kina ~ 70% ya watu, hivyo 70% ya pato la mtz wa kawaida litakuwa linaenda kwenye chakula. Kupunguza wakulima kutaiendeleza nchi "wananchi kwa ujumla" vinginevyo ni sarakasi mwananchi anazidi kuumia.
Chanzo cha umasikini ni nini mkuu?
 
Chanzo cha umasikini ni nini mkuu?

umasikini ni kutokuishi ktk kiwango cha maisha kinachofikirika kinatimiza mahitaji ya binadamu. Viwango hivi vya kufikirika vinapishana baina ya sehemu, kuna $1, mpaka +$4, Tanzania kuna wakati ilikua 1000 tsh, kama matumizi ya mtu kwa siku.
Chanzo ni chochote kinacho kufanya usifikie lengo hapo juu.
Kwa mtazamo wa Tanzania unabaini kwa kuangalia, sera, mgawanyo wa rasirimali na mlinganyo wa kisekta kwenye kuchangia pato la taifa.
Kilimo hakiwezi kuongoza nchi, ila pesa na rasirimali nyingine zinavunwa kuendeleza sekta nyingine. Wakulima wanatakiwa wawe chini ya 10% ya raia.
Chakula kitakua si anasa kwa Mtanzania,
Sekta nyingine zikiongezeka ubora, gharama pia kwenye sekta hizo zitapungua.
Naomba kuwasilisha jibu rahisi fupi kwa swali gumu.
 
sababu kuu ni ujinga wa watanzania kuchagua viongozi wabovu sababu ndio waliotufikisha apa.
 
ushawahi kujiuliza kwanini wewe binafsi ni maskini?
mimi hakuna msemo nisioupenda kama huo utasemaje watanzania maskini wakati wakina mengi, bakhresa, dewji wapo kwenye top 50 ya mabilionea wa africa?

#kunjani kuti
 
Tanzania sio masikini...tuna rasilimali nyingi tu ambazo zinaleta faida kubwa taifa kama
  • UTALII,kitu ambacho nchi nyingi hakina...I AM PROUD OF IT
  • MADINI....Tatizo ni kwamba waliokuwa juu wanatumia vitu hivi kwa manufaa yao wenyewe na wanaoumia ni walalahoi ofcourse!
  • Tumejaaliwa watu wenye knowledge na ufahamu mkubwa lakini kuweka hizo ideas into actions ndio kazi kubwa kwasababu hawo magenius hakuna mtu/njia ya kuendeleza vipaji vyao.
  • Hatuna SYSTEM..Ukitaka nchi iende kwa ustaarabu lazima kuwe na system...hata kwenye foleni hakuna system watu washazoea shortcut..Ulaya watu wanalelewa kwa system bana hata basi likija automatic watu wanapanga foleni na abadani huoni mtu akajifanya mjanja kuwapita wenzake na hata akifanya hivo ataomba samahani aseme na sababu!
  • Lazima kuwe na system kuanzia nyanja ya chini kabisaaa....Uliza uambiwe nchi za watu kila mtu ana birthnumber...Ikiandikwa tu kwenye computer zinakuja information zako zote!!!
  • Sheria haifati mkondo wake...CORRUPTION EVERYWHERE....Tunarudi tena palepale hakuna SYSTEM,na hata ikiwekwa hio system itachukua decades mpaka kuwa established maana wananchi washazoea kuishi kiholela...Ni wabinafsi in general
 
Kuna sababu nyingi za kwanini Tanzania ni masikini lakini kwa upande wangu, tatizo kubwa zaidi ni kwa kiongozi mwenyewe, yeye ndio tatizo la kwanza.
Kwa kiongozi kutokujua kwanini Tanzania ni masikini ni tatizo kubwa zaidi.
Anyway, Tanzania ni masikini kwasababu zifuatazo (nifikiriavyo)
1. Kutojua thamani ya wananchi kwa upande wa viongozi.
Sio siri kua nchi yetu ina watu wengi zaidi. Baadhi ya watu hutoa sababu ya over population kama chanzo cha umasikini kwa nchi yetu. Binafsi naona kwenye ongezeko la watu pia kuna ongezeko la pato na maendeleo ya watanzania endapo kutakua na uhakika wa elimu bora kwa kila mtanzania bila kujali ana pesa ama la, pia ajira kutolewa kwa vijana sio mpaka wakafatwe watu nje ya nchi nk. China kuna watu wengi sana lakini si masikini.
2. Gonjwa la UKIMWI
Hili gonjwa ni janga la taifa. Vijana wadogo wanao tegemewa wamekua wakiathirika zaidi. Wengi hufa mapema. Ingawa kuna dawa za kupunguza makali ya gonjwa hili hutolewa mahospitalini (ARV) lakini naona haitoshi. Sijawahi kuona dawa zinatumika bila chakula kizuri. Watanzania wengi hawapati balance diet kutokana na bei ya vyakula. Nina imani wengi wanapenda sana kupata mlo kamili ila maswala ya pesa yanasumbua. Sitaki kusema kua watanzania hawapati mlo kamili sababu ya elimu duni sababu hata madocter wanao shauri balance diet kwa mgonjwa unakuta yeye mwenyewe hapati balance diet ingawa si wote. My point ni kwamba viongozi wangekaa chini na kujaribu kutatua mfumuko wa bei wa vyakula ili hata mwananchi mwenye hali duni aweze kupata balance diet ambayo ni dawa nzuri kwa waathirika ili waendeleze kusupport maendeleo ya nchi yetu.
3. Utumiwaji mbaya wa kodi za wananchi kwenye serikali yetu. Kodi ambazo zikitumiwa vyema hakutakua na kubabaika kimaendeleo. Kwasasa bado tunababaika tu.
4. Kutojitambua. Mwananchi anapaswa kujitambua na kujua wajibu wake ndani ya serikali vivo hivyo kwa viongozi. Mwananchi anapokosa uzalendo wa nchi yake ni tatizo kubwa sana lakini pia kiongozi ambae hajui maana ya kua kiongozi ni tatizo zaidi. Wengi wanaongoza wakiwa na ndoto za kulala ikulu bila kujua kua kiongozi ni mtu anae ongoza na kusimama kwaajili ya watu. Ni sawa na kujitoa sadaka kwaajili ya watu badala yake viongozi wanaishia kuficha pesa calling themselves leaders lol.
Kuna sababu nyingi ila naomba niishie hapo.
 
ushawahi kujiuliza kwanini wewe binafsi ni maskini?
mimi hakuna msemo nisioupenda kama huo utasemaje watanzania maskini wakati wakina mengi, bakhresa, dewji wapo kwenye top 50 ya mabilionea wa africa?

#kunjani kuti

Tuache majibu ya kisiasa. Wananchi wengi ni masikini ukiacha hao wachache uliowataja na wengine ambao hela ya kula haiwapigi chenga. Ila majority of tanzanians wako below poverty line. Je ni nini chanzo hasa?
 
Unafikiri kwa nini hawataki utajiri?

kwa kuchagua viongozi wenye maono madogo. Wataalamu wanatengeneza sera za kisekta, kisha 'strategic plan' mpango ekelezi ambayo inaungwa kupata mpango elekezi wa nchi, unaokutana na ilani ya chama tawala ambayo pia ni mpango elekezi wa matumizi ya rasilimali na vipaumbele. Ilani inayosema kilimo ni uti wa mgongo iogope kwani waliotengeneza wanataka kura toka kwa wakulima, mwisho wa siku watakuambia ilani haitekelezeki, akificha atakuambia sijui kwa nn Tz masikini.
 
kwa kuchagua viongozi wenye maono madogo. Wataalamu wanatengeneza sera za kisekta, kisha 'strategic plan' mpango ekelezi ambayo inaungwa kupata mpango elekezi wa nchi, unaokutana na ilani ya chama tawala ambayo pia ni mpango elekezi wa matumizi ya rasilimali na vipaumbele. Ilani inayosema kilimo ni uti wa mgongo iogope kwani waliotengeneza wanataka kura toka kwa wakulima, mwisho wa siku watakuambia ilani haitekelezeki, akificha atakuambia sijui kwa nn Tz masikini.
Je hawa wananchi wanao uelewa wa kutosha kabla ya kuchagua?
 
Je hawa wananchi wanao uelewa wa kutosha kabla ya kuchagua?

ni vigumu kwa mwananchi wa kawaida kutofautisha kiongozi mwenye maono madogo asiyeweza kujua kwa nini wananchi wake masikini, mwenye maono makubwa ya kujaza watu pesa huku akipunguza kodi 'haiwezekani', mwenye maono makubwa dokt 'Phd' fulani mwenye akili nyingi anae endeshwa na akili ndogo kisa chuo hakilipi > ulafi, ufisadi unawapofusha... Ni vigumu kwa mkulima kutabili 'motive' ya siasa kwa kuangalia ilani.
Hapa ndio wazalendo kama M. Amani anapohitajika kukomboa nchi. Si kwa vita. Si kwa kuangalia sura/jina bali sera ilani na msimamo wa kiongozi kwa jamii. Kisha kumpigia upatu.
Usisahau mgombea binafsi ni ukombozi pia.
 
Asilimia 70 ya waTanzania ni wakulima "duni" na wanaishi vijijini.

Kilimo huchangia zaidi ya 65% ya GDP. kama kilimo ni duni, taifa letu haliwezi kuendelea.

Zaidi ya asilimia 45 ya waTanzania wapo chini ya umri wa miaka 18 "walaji" siyo wazalishaji.

Taifa lina "import" zaidi ya ku-export. Tunatumia hela nyingi kununua bidhaa kuliko kuuza.

Tanzania haina viwanda vya kuzalisha au kuongeza thamani ya mazao au malighafi zetu. Tunazalisha pamba, zinaenda kuongezewa thamani nje tunaletewa pamba iliyothamishwa kwa bei juu. Tunauza bidhaa nje bei chee tunaletewa mali kwa bei ya juu.
 
(1)Fanya kazi kwa kujituma utauondoa umasikini kwenye maisha yako.
(2)chunga matumizi ya fedha unazopata.acha matumizi yasiyo ya lazima mfano
pombe kuhonga sherehe zisizo na ulazima n.k
(3)anza utamaduni wa kuweka akiba benki.
(4)Jiwekee malengo ya kuanzisha mradi.
 
Mambo ya yanayoleta maendeleo katika nchi (JK. Nyerere)
1.Watu, 2.Ardhi, 3.Siasa safi, 4.Uongozi bora.
Tanzania watu tunao 45 ml.,ardhi tunayo zaidi ya sq[SUP]2[/SUP].mt 900,000,
Lakini Tanzania in viongozi wabovu hakuna maelezo. Tanzania haina siasa bali kauli mbiu tu. Mifano: maisha bora kwa kila mtanzania, big results now, smart partnership, sullivan, kilimo kwanza, kasi mpya, nguvu mpya, ari mpya, nk.
 
(1)Fanya kazi kwa kujituma utauondoa umasikini kwenye maisha yako.
(2)chunga matumizi ya fedha unazopata.acha matumizi yasiyo ya lazima mfano
pombe kuhonga sherehe zisizo na ulazima n.k
(3)anza utamaduni wa kuweka akiba benki.
(4)Jiwekee malengo ya kuanzisha mradi.
(5)Acha nasema acha kulaumu upande mwingine kwamba umekusababishia umaskini bado mtanzania una nafasi kubwa ya kuhama toka kwenye umaskini zingatia hatua hizi tano nilizokupa.asante kwa kusoma paragraph hizi.
 
Back
Top Bottom