Watanzania ni maskini kutokana mambo makuu yafuatayo; Elimu, Siasa, Rushwa, Uongozi na idadi ya watu. Nitayajadili haya mambo makuu matano kila moja kwa nafasi yake.
Elimu ina mchango mkubwa sana wa kumtoa mtu kwenye umaskini. watanzania tutabaki kuwa maskini mpaka pale kwanza tutakapobadili mfumo wetu wa elimu na kuwa na elimu ya ushindani, elimu ya kujitambua, elimu itakayoweza badili mfumo wetu wa fikra. Elimu ya sasa ni elimu inayomwekea mazingira yule anayeipata ashindwe kujitambua yuko kwenye mazingira gani na afanye nini ili atoke pale alipo.
Mifano iko wazi sana, utaona mtu yuko tayari kutaja kiwango chetu cha elimu kwa majigambo bila kuweza kusema kiwango chake cha elimu kimemsaidiaje au amefanya nini kuikwamua Tanzania kutoka kwenye umasikini. Hii ni hatari sana kwa msomi kutokutambua elimu inamsaidiaje. Kuna wanaoitwa wasomi nchi akiliongelea au kulichambua jambo unaashindwa kupata tofauti ya mtazamo wake na yule kijana mchunga ng'ombe wa kule kijijini kwetu ......... . Kuna mwanaharakati mmoja wa India alishawahi sema kwamba kama elimu kama haijaijngia kwenye ufahamu wako, moyoni mwako na kubadili vile unavyofikiri na mtazamo wa dunia basi elimu hiyo haina tofauti na joho ulilolivaa asubuhi siku yako ya maafali na kulivua jioni yake.
Kiongozi wa Indonesia alishwahi kusema Afrika tunasoma tusivyovihitaji na tunavihitaji vitu tusivyovisomea. Indosea ilipata uhuru wake miaka karibu sawa na Tanzania lakini tazama leo wako wapi.
Siasa imetoa mchango mkubwa sana kwenye kufanikisha nchii inakuwa masikini mpaka leo. Ni wanasiasa wanaoshiriki kutunga kanuni na sheria za nchi. Wanatunga sheria ambazo zinazomkandamiza mtanzania asipate elimu itakayoweza kumfumbua macho au kupata ufahamu wa kujitambua ni mazingira gani anayoishi au yanayomzunguka. Kwa wasomi waliowengi wanaona njia pekee ya kujikomboa ni siasa inafanya mpaka wanasahau kuwa taaluma yao inaweza leta tofauti kimaisha. Wanasiasa mejitengenezea mazingira kwamba maendeleo ya nchi au sehemu hayawezi kuja bila kupitia wao na mbaya zaidi hii imekaa kwenye ufahamu wa watanzania walio wengi na kuwaona wanasiasa ni mungu watu.
Unaposikia mwanasiasa anaizungumzia Tanzania wenye fikra tunajua hali ni mbaya. Wanayozungumza kama Tanzania haina wenyewe, Tanzania ni kama mkate wa bofro basi wanastahili kugawana na yeyote Yule anayekuja kumuomba. Na mbaya zaidi ni wanasiasa ni wale wale, majina ni yale yale mawazo ni yale yale vina "mutate" tangu nchi hii inapata uhuru, hivyo unazani lini tutatoka kwenye umasikini.
Rushwa imechangia kwa kiasi kikubwa nchi kuwa maskini kwa kiasi hiki. Rushwa imekuwa ni tamaduni kwetu na kufanya swala uaminifu lisiwepo kabisa au lisipate nafasi kwenye mitazamo yetu ya ukombozi wa kimaisha. Hakuna sehemu yenye haki kila kona lazima utoe fedha ili mambo yaende hii ni kansa na inarudisha sana nyuma maendeleo ya nchi hii.
Uongozi bado tatizo kubwa kwenye nchi nyingi maskini za kiafrika. Watu wanaacha majukumu yao ya kuhudumia wananchi badala yake wanajinufaisha wao na familia zao. Tanzania tunaenda kupata katiba mpya lakini swala la kujiuliza ni muongozo gani mpya utakaotolewa na katiba utakao weza badili mfumo wa uongozi wa nchi hii kujikwamua kutoka kwenye janga la umasikini.
Katiba ni kama msingi tu wakufanya yaliyosahihi na kila kiongozi anakuja na ilani yake je ni mangapi yaliyotengenezeka kwenye hizo ilani zao iwe wawepo madarakani au wasiwepo madarakani.
Idadi ya watanzania walio wengi ni vijana je vijana wanatambuaje umuhimu wao kwa taifa hili. Kuna vijana wengi wamesomi ila siasa za nchi hii zimewafanya kusahau umuhimu wao kwenye nchi yao. Dini imekuwa kama ndiyo mkate na siagi wakati hivi vitu tumeletewa tu havikuanzia Tanzania. Unakuta vijana wanalumbana wewe muislamu! wewe mkristo! lakini wanashindwa kutambua wao ni watanzania sasa busara iko wapi hapo?
Tunaambiwa vijana ni taifa la kesho lakini matendo tunayoyapa mkazo kwenye maisha yetu ya kila siku yanawafanya wanasiasa waamini kuwa hatuko tayari hata kwa hiyo kesho. Tazama wastani wa umri wa viongozi wa Afrika linganisha na wastani wa nchi zilizoendelea utaona tofauti unajieleza wazi kuwa hatuthaminiwi na kutokana na kutojithamini sisi wenyewe.
Utathaminiwa kama na wewe unajithamini lakini kutwa nzima unakaa kupiga soga tu la siasa na dini nani atakukabithi majukumu hata ya uongozi wa wilaya ukiachilia mbali ya nchi. Tunapenda mambo ambayo hayana thamani kwetu wala kwa nchi yetu. Kama kila kijana angeamuwa kufanya kidogo kwa nchi hii Tanzania ingekuwa mbali sana. Mother Teresa "you do not have to do great things, do small things in a great way". Lakini tunategemea serikali tu ndiyo mkombozi wetu, hata kwenye vitu vidogo tu unasikia "tunaomba serikali itufanyie ......" ni up. umba .vu wa kutojitambua.
Tubadili mitazamo yetu tuanze kuiondoa ile sumu na kasumba tunayopandikiziwa na wanasiasa. Tuanzishe mijadala ya ufumbuzi wa matatizo ya nchi yetu, tunafanyaje ili tutoke hapa tulipo. Mfano mdogo huu uzi haujafika hata page kumi sababu hauna siasa au dini hivyo wao hauwahusu. Ni hatari sana, ni hatari sana
Hizi ndizo sababu kuu zinazotufanya tuwe maskini kwa mtazamo wangu. Lakini Mwl. Nyerere aliwahi kusema " It can be done play your part".