Japo nchi ina kila mtaji unaotakiwa kujikwamua kimaendeleo mimi nadhani tatizo ni WANANCHI WA TANZANIA!

1. Wengi ni wazembe - hawafanyi kazi masaa mengi ya kutosha; wanapenda starehe kuliko kazi (rejea siku kibao za kupumzika na zingine zinazotangazwa kwa dharura, nk).

2. Wengi hawajui siasa - uelewa mdogo wa wajibu wao, umuhimu na majukumu ya viongozi.

3. Wengi hawafikirii maisha ya baadaye zaidi ya kesho.

4. Wengi wanaishi maisha ya "copy na paste" na wapenda sifa wasizostahili.

5. Wengi si wazalendo - unafiki umetamalaki, chuki - ukarimu ni kwenye salamu tu!

6. Wengi ni washirikina - watu wa nia mbili, jina dini fulani; imani nguvu za giza!

Sijaweka elimu moja kwa moja, kwa sababu binafsi sioni mchango wa elimu wanayopata watanzania kwenye mabadiliko ya fikra na mtazamo wao au hata maendeleo ya Taifa.......

Haya ni mawazo yangu. Karibuni kwenye mjadala!
 
Tanzania masikini kutokana na attitude za watu wake.

Watumishi wa umma wanatukwamisha sana.

Sasa hivi nchi inaendeshwa na private sector kwa kuchapa kazi , kulipa kodi n.k

Lakini wenzetu serikalini wamekunja nne tu wanaingia ofisini saa nne wanatoka saa saba mchana lunch time.

Na wish tupate kiongozi ambaye ataamsha hawa wenzetu nao wafanye kazi wasijione mungu watu utafikiri nchi yao wao peke yao!!!
 
Mkuu Maundumula

Shukran sana kwa hizi bayana zako.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu zangu wa Tanzania mara nyingi huwa najiuliza swali hili lakini sipati jibu kamili, hivo nategemea kulipata humu kwa wana jamvi. Pamoja na neema zote tulizo jaaliwa na mwenyezi MUNGU ndani ya taifa hili kwani nini tuitwe nchi masikini tena ya pili kutoka mwisho? Tatizo liko wapi? Tatizo nini hasa? Na unadhani nini kifanyike ili kuondokana na hali hiyo ya umasikini uliokithiri kwa wana wa Tanzania? Naomba tujadili pamoja watanzani wenzangu.
 
Kirogo...

 
Mkuu Sabanya' Hakika suali lako hapo juu zuri !!
Jibu lake ni hili hapa:- Siyo wa Aminifu !! hivyo la kufanya ni Tubadilikee!!
1+1 = 2
Blessings
 

At the red:Lazy guys wants to elect Lowasa expecting him to stop corruption
 
Mkuu, tangu nchi hii ipate uhuru imeongozwa na CCM tu lakini bado watu kama akina Ritz, Simiyu wanaipenda CCM. Nadhani hali hii ya umasikini inawaridhisha
 
1..wanasiasa kuiibia hela serikali
2...KUWA NA RAISI DHAIFU, ASIYEWAJIBIKA WALA KUWAJIBISHA ALIOWATEUA
3..katiba mbovu
4...ajira za kujuana..,
5...kuwa na jeshi la kipuuzi lisilo na wasomi linalotumiwa na wanasiasa
6....
7...
 
imani za kishirikina zimetawala sana kwa mfumo mzma wa viongozi wetu wanashndwa kuwajibika wana shdana kwenda kwa waganga wa jadi
 
Rasilimali zote hizo zinatumika na zinaingiza pesa lkn tu masikini mi najitahdi kutafakari sipati jibu mnisaidie wana jf,nikijarbu kujifananisha na majiran zetu kenya na rwanda wametuacha kwa mbali sana kimaendeleo na rasilimali zao kidogo ni kwann?
 
Tatizo ni hiki chama cha mafisadi.Bila ccm kutoka madarakani tutaendelea kulalamika siku hadi siku!
 
"Tanzania ni Nchi tajiri yenye watu maskini tokana na Nchi kukosa Elimu bora kwa watu wake,siasa bora,uongozi bora wenye viongozi bora wanaowajibika kwa nafasi zao,pamoja na sera mbovu za matumizi ya ardhi"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…