Wakuu salaam,
Kuna hisia miongonni mwa watanzania kuwa uduni wao katika maendeleo umesababishwa na wazungu ambao pia huitwa mamepari.
Mimi nasita kukubaliana na hisia hizi kwa sababu sisi tumejaliwa akili kama wao na zaidi ya hapo tumezungukwa na raslimali tele na mazingira ambayo tukiyatumia hata kwa maarifa madogo tuliyo nayo tunaweza kuendelea sana tu. acha nichukue mifano michache kuthibitisha hoja yangu.
kwanza tuna ardhikubwa na nzuri na nyingine haijawahi kuguswa tangu kuumbwa. Kwangu mimi ardhi hii ni sawa tu na dhahabu kwani ni utajiri mkubwa unaoweza kutupa kila kitu. tujiulize tunaitumia kwa kiasi gani! ajabu vijana wanaikimbia na kwenda kuzamia meli, kugeuka machinga na hata ukabaji.
Pili tuna vyanzo vya kutosha vya maji kwa matumizi mbalimbali kama uvuvi, umwagiliaji,usafirishaji nk. nk. Ajabu watu walioko karibu na vyanzo hivi wanahangaika kutafuta mboga!
Tatu, tuna baraka ya mvua maeneo mengi ambayo maji yake licha ya kutumika kwa kilimo yanaweza kuhifadhiwa kwa matumizi mengi tu. Si ajabu mvua ikanenyesha na inapoisha tu ukamwona mama anabeba ndoo kutafuta maji ya kisima!
Nne tuna misitu ambayo ni vyanzo vya nishati, mvua, maji nk. lakin badala ya kuitumia kama kufuga nyuki na matumizi mengine endelevu ndo kwanza tunanunua mashoka kuifyekelea mbali na kuchoma mkaa! Maji na mvua vikikosekana tunaingia nyumba za ibada kukesha kuomba mvua badala ya kupanda miti.
Sasa wazungu wanainigiaje hapa kama hatuendelei?
Tunaenda kwa wazungu tunaomba watusaidie katika elimu, afya barabara, maji, umeme nk. Chukulia magonjwa mazito kama Ukimwi, kifua kikuu, Kannsa nk. yote haya tunapata madawa kama ARV kwa ufadhili.
Je, nikweli hatuendelei kwa sababu ya wazungu? Ni ipi nafasi yetu ya kuendelea bila kupeleka lawama kwa wazungu?
Inawezekana? Kuna haja ya kutoa boriti kwenue macho yetu badala ya kibanzi kwenye jicho la ...